Wazo juu ya vijana kujikwamua na kuushinda umasikini

kipoma

JF-Expert Member
Joined
Aug 27, 2012
Posts
370
Reaction score
296
Habari wanajf,
Mimi ni kijana kwa umri 27,

Leo ninalo wazo juu ya vijana kujikwamua na kuushinda umasikini. Kwanza niseme yafuatayo;
  • Kijana kwa asili yake hupata pesa ndogo ndogo ambazo huwa hawezi kuona kama ni mtaji.
  • Kijana hutumia pesa hizo kwa mambo madogo madogo kutokana na thamani ya pesa hiyo.
  • Kijana hawezi kuwa na fikra juu ya kuanzisha biashara au kuwekeza kokote.
  • Kijana huwa hana mpango wowote na bajeti juu ya matumizi ya pesa yake hiyo.
Note; Vijana ninawozungumzia hapa ni wale tuishio na tunaotoka familia masikini na ambao hatuna msaada wowote toka kila kona, vijana ambao hakuna wa kutupazia sauti.

KUUNGANA NA KUSHINDA

Kuungana kuna nguvu kubwa sana katika kukabiliana na jambo lolote lile na katika mambo ya pesa / fedha ni kuaminiana na kuwa wote waminifu.

Kuungana si lazima muwe kumi au mia hata mukiwa wawili mnaweza kufika mbali sana na kuushinda umasikini.

Angalia dondoo hizi;
  • Muungano ni kundi/kikundi/ makundi.
  • Kikundi kizuri kwa vijana kisizidi watu wanee, kwahiyo watu wawili, watatu au wanne wanatosha kwa kundi nzuri na lenye nguvu kubwa.
  • Kundi lazima liwe ni la watu wenye mahusiano fulani ,mfano Rafiki, ndugu au mtu ambaye mmeaminiana.
  • Umbali kisiwe kikwazo kwenu kufikia mafanikio, munaweza chagua eneo la kufanyia shughuli yenu kutokana na shughuli yenu muitakayo. Mfano kilimo ni shambani tena kijijini pia ufugaji huko, biashara kidogo inahitaji center nzuri hivyo ni mjini .
  • Kundi lazima mkae kwa pamoja na kujadili vyanzo vya mtaji wa shughuli yenu
  • Kundi lazima mkae na mpange au mbuni shughuli ambayo mnaweza kuifanya kwa ufanisi na yenye tija kwenu wote.
Kwa kuzingatia hayo vijana lazima tuushinde umasikini.

NJIA RAHISI YA KUPATA MTAJI

Neno mtaji si lazima ziwe malaki, mamilioni au mabilioni kumbuka Tilioni huja kutoka kwa cent 5 , kijana mtaji si kitu kikubwa hivyo.
  • Vijana katika kundi lenu changishaneni kiasi kidogo cha pesa ambacho mna uwezo nacho na kama nilivyosema awali kuwa vijana huwa na pesa ndogondogo.
  • Vijana ombeni pesa kutoka kwa watu wa karibu yenu ambapo najua pesa hiyo bado itakuwa ni kidogo.
Hizo ni njia mbili za uhakika kwa vijana kujipatia mtaji katika kundi lenu tofauti na mikopo hutesa sana na kuua kundi haraka.

Kwa biashara au mishe yoyote kwa kipindi hiki unatakiwa kuwa na mtaji wa sh 50000 hadi 100000. Hiki kiwango ni kwa vijana ambao hakika wanataka kuushinda umasikini , kiwango kikubwa kinatakiwa ila kulingana na uwezo wa kundi lenu.

Nahitaji kijana mwenzangu moja wa kushirikiana nami ila awe anatoka mkoa wa Iringa mjini, Nduli au Ismani.

Nawasilisha

Asante.
M
K
P
Iringa.
 
Mtaji wa elfu 50 au laki ndio umeandika uzi wote huu
Kwa kweli nimejitahidi kusoma mwanzo mwisho lakini nimerudia hapo kwenye mtaji.

Nasubiri na wadau wengine labda nina waza tofauti kwa huu mtaji
 
Mtaji wa elfu 50 au laki ndio umeandika uzi wote huu
Kwa kweli nimejitahidi kusoma mwanzo mwisho lakini nimerudia hapo kwenye mtaji.

Nasubiri na wadau wengine labda nina waza tofauti kwa huu mtaji
heshimu pesa mkuu mzee wangu ambae sasa ana pesa yake nzuri tu ali nisimulia jinsi alivyo anza utafutaji mtaji wake haukufika hata hio elf 50
 
heshimu pesa mkuu mzee wangu ambae sasa ana pesa yake nzuri tu ali nisimulia jinsi alivyo anza utafutaji mtaji wake haukufika hata hio elf 50
Mwaka gani huo?
Na amefika hapo kwa miaka mingapi kuwa na hiyo so called pesa nzuri

Hiyo miaka ya nyuma wengi tunaijua na gharama zilikuwa ndogo
Wazo la kuanza biashara mkiwa wengi ni zuri sana na wengi sana wanafanya hivyo siku hizi na nchi nyingi vijana wanafanikiwa hivyo.
Lakini kufanikiwa huko vijana wanafanya kazi kwa waajiri wao kwa lengo la kufanya kitu labda tuseme mmeweka lengo baada ya miaka minne kila mmoja aje na kiasi kadhaa cha fedha ili mfanye big project
Lakini mtaji wa kununua samaki mwanza kwa elfu 70 na kupata faida ya elfu 30 mkoa mwingine utoe na gharama za usafiri hapo utapata lakini utafikia malengo makubwa au ni hand to mouth
Well maisha ya sasa yana gharama na changamoto nyingi kuanzia watu feki mpaka bidhaa feki yaani kila kitu feki inabidi uwe na makini sana na kupata hiyo au hao genuine ndio kazi
 
Mtaji wa elfu 50 au laki ndio umeandika uzi wote huu
Kwa kweli nimejitahidi kusoma mwanzo mwisho lakini nimerudia hapo kwenye mtaji.

Nasubiri na wadau wengine labda nina waza tofauti kwa huu mtaji


Soma vizuri mkuu
 
mkuu dunia ni ile ile zina badilika tarehe tu, miaka ya nyuma maisha yalikua cheap lkn soko lilikua changamoto tofaut na sasa idadi ya watu imeongezeka so changamoto ya gharama za maisha ina ongeza thamani ya bidhaa pia formula ni ile ile tu
 
Mtaji wa elfu 50 au laki ndio umeandika uzi wote huu
Kwa kweli nimejitahidi kusoma mwanzo mwisho lakini nimerudia hapo kwenye mtaji.

Nasubiri na wadau wengine labda nina waza tofauti kwa huu mtaji
Asiye na akili huwa haoni pia.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…