kipoma
JF-Expert Member
- Aug 27, 2012
- 370
- 296
Habari wanajf,
Mimi ni kijana kwa umri 27,
Leo ninalo wazo juu ya vijana kujikwamua na kuushinda umasikini. Kwanza niseme yafuatayo;
KUUNGANA NA KUSHINDA
Kuungana kuna nguvu kubwa sana katika kukabiliana na jambo lolote lile na katika mambo ya pesa / fedha ni kuaminiana na kuwa wote waminifu.
Kuungana si lazima muwe kumi au mia hata mukiwa wawili mnaweza kufika mbali sana na kuushinda umasikini.
Angalia dondoo hizi;
NJIA RAHISI YA KUPATA MTAJI
Neno mtaji si lazima ziwe malaki, mamilioni au mabilioni kumbuka Tilioni huja kutoka kwa cent 5 , kijana mtaji si kitu kikubwa hivyo.
Kwa biashara au mishe yoyote kwa kipindi hiki unatakiwa kuwa na mtaji wa sh 50000 hadi 100000. Hiki kiwango ni kwa vijana ambao hakika wanataka kuushinda umasikini , kiwango kikubwa kinatakiwa ila kulingana na uwezo wa kundi lenu.
Nahitaji kijana mwenzangu moja wa kushirikiana nami ila awe anatoka mkoa wa Iringa mjini, Nduli au Ismani.
Nawasilisha
Asante.
M
K
P
Iringa.
Mimi ni kijana kwa umri 27,
Leo ninalo wazo juu ya vijana kujikwamua na kuushinda umasikini. Kwanza niseme yafuatayo;
- Kijana kwa asili yake hupata pesa ndogo ndogo ambazo huwa hawezi kuona kama ni mtaji.
- Kijana hutumia pesa hizo kwa mambo madogo madogo kutokana na thamani ya pesa hiyo.
- Kijana hawezi kuwa na fikra juu ya kuanzisha biashara au kuwekeza kokote.
- Kijana huwa hana mpango wowote na bajeti juu ya matumizi ya pesa yake hiyo.
KUUNGANA NA KUSHINDA
Kuungana kuna nguvu kubwa sana katika kukabiliana na jambo lolote lile na katika mambo ya pesa / fedha ni kuaminiana na kuwa wote waminifu.
Kuungana si lazima muwe kumi au mia hata mukiwa wawili mnaweza kufika mbali sana na kuushinda umasikini.
Angalia dondoo hizi;
- Muungano ni kundi/kikundi/ makundi.
- Kikundi kizuri kwa vijana kisizidi watu wanee, kwahiyo watu wawili, watatu au wanne wanatosha kwa kundi nzuri na lenye nguvu kubwa.
- Kundi lazima liwe ni la watu wenye mahusiano fulani ,mfano Rafiki, ndugu au mtu ambaye mmeaminiana.
- Umbali kisiwe kikwazo kwenu kufikia mafanikio, munaweza chagua eneo la kufanyia shughuli yenu kutokana na shughuli yenu muitakayo. Mfano kilimo ni shambani tena kijijini pia ufugaji huko, biashara kidogo inahitaji center nzuri hivyo ni mjini .
- Kundi lazima mkae kwa pamoja na kujadili vyanzo vya mtaji wa shughuli yenu
- Kundi lazima mkae na mpange au mbuni shughuli ambayo mnaweza kuifanya kwa ufanisi na yenye tija kwenu wote.
NJIA RAHISI YA KUPATA MTAJI
Neno mtaji si lazima ziwe malaki, mamilioni au mabilioni kumbuka Tilioni huja kutoka kwa cent 5 , kijana mtaji si kitu kikubwa hivyo.
- Vijana katika kundi lenu changishaneni kiasi kidogo cha pesa ambacho mna uwezo nacho na kama nilivyosema awali kuwa vijana huwa na pesa ndogondogo.
- Vijana ombeni pesa kutoka kwa watu wa karibu yenu ambapo najua pesa hiyo bado itakuwa ni kidogo.