Wazo: Kuthibiti ajali magari kugongana,tutumie 2+1

Mathias Byabato

JF-Expert Member
Joined
Nov 24, 2010
Posts
1,055
Reaction score
781
Ndugu wanabodi. Nimefikiria mbinu inayoweza punguza sana ajali za magari kugongana hasa katika Barbara zetu kuu. Hapa chini ni mapendekezo ambayo nafikiri yakitumiwa na Tanroad,Serikali kuu na polisi kuna uwezekano mkubwa kupunguza hizi ajali.



Mfumo wa 2+1 ni nini.

Mfumo wa 2+1 Road System ni mbinu ya usanifu wa barabara inayolenga kupunguza ajali na kurahisisha magari kupishana bila kujenga barabara ya njia nne.

Kwa sababu ukitazama na kusikiliza ajali nyingi zinazochukua maisha ya watu nyingi ni makosa ya gari kugongana hasa wakati WA ama kupishana au overtaking. Sasa mfumo huu wa 2+1 umesaidia sana baadhi ya nchi duniani palipokuwa na shida kama hii ya kwetu.

MFUMO WA BARABARA ZA 2+1

Barabara za 2+1 ni mfumo wa ujenzi na usimamizi wa barabara unaotumia njia tatu za magari, ambapo njia mbili zinatumika na magari yanayoelekea upande mmoja, huku njia moja ikitumika na magari yanayoelekea upande wa pili.

Mfumo huu umeanzishwa na kutumika nchini Sweden kwa lengo la kuongeza usalama barabarani, kupunguza ajali za kugongana uso kwa uso na kurahisisha magari kupita magari mengine yanayotembea kwa mwendo mdogo.

Mfumo unavyofanya kazi

Barabara hugawanywa katika sehemu ambazo idadi ya njia kwa kila mwelekeo hubadilishana.

Katika sehemu ya kwanza, magari yanayoelekea upande A yanakuwa na njia mbili, wakati magari yanayoelekea upande B yanakuwa na njia moja.

Katika sehemu inayofuata, magari yanayoelekea upande B yanapata njia mbili, huku magari yanayoelekea upande A yakibaki na njia moja.

Mpangilio huu huendelea kubadilishana kwa umbali uliopangwa kulingana na usanifu wa barabara, kiasi cha magari na mahitaji ya usalama.

Jinsi magari yanavyopita

Wakati upande mmoja una njia mbili, madereva wanaweza kutumia njia ya ziada kuyapita magari yanayotembea polepole.

Mwisho wa sehemu hiyo, alama za barabarani huwaelekeza madereva kurudi kwenye njia moja kabla ya eneo la kubadilisha mwelekeo wa njia mbili.

Madereva wanapaswa kufuata alama za barabarani na hawaruhusiwi kuendelea kutumia njia ya ziada baada ya kuisha kwa sehemu iliyoruhusiwa.

Kizuizi cha usalama katikati ya barabara

Moja ya vipengele muhimu vya mfumo huu ni kuwekwa kwa kizuizi cha usalama katikati ya barabara, mara nyingi kinachotengenezwa kwa waya imara za chuma (wire-rope safety barrier).

Kizuizi hiki hutenganisha magari yanayotembea katika mielekeo tofauti na kusaidia kuzuia magari yasivuke na kugongana uso kwa uso.

Hii ni faida kubwa ya mfumo huu katika kupunguza ajali zinazoweza kusababisha vifo na majeraha makubwa.



Faida za mfumo wa 2+1

* Kupunguza ajali za kugongana uso kwa uso.

* Kurahisisha kupita magari yanayotembea polepole.

* Kuongeza usalama wa watumiaji wa barabara.

* Kuboresha uwezo wa barabara kuhudumia magari bila kuhitaji kujenga barabara pana yenye njia mbili kwa kila mwelekeo.

* Kutoa fursa ya kuboresha barabara zilizopo kwa gharama ambayo inaweza kuwa ndogo kuliko kujenga barabara mpya ya njia nne.

Mambo muhimu katika utekelezaji

Ili mfumo huu ufanye kazi vizuri, unahitaji usanifu sahihi wa barabara, alama zinazoeleweka, mistari ya barabarani inayoonekana vizuri, kizuizi cha usalama katikati na maeneo yenye nafasi ya kutosha kwa magari kubadilisha njia kwa usalama.

Pia, mwendo wa magari, kiasi cha trafiki, umbali wa sehemu zenye njia mbili na hali ya mazingira lazima vizingatiwe wakati wa kupanga barabara.

Mfumo wa barabara za 2+1 ni njia ya kuboresha usalama na ufanisi wa usafiri kwa kutumia njia tatu zinazobadilishana mwelekeo wa njia mbili kwa vipindi maalumu.

Tanroad,Serikali wafanye nini.
Wataalam wetu. Wafanye kwanza uchambuzi Kwa maeneo yenye changamoto kubwa. Watembelee mojawapo ya nchi hizi zenye barabara hizo..maana nao walipitia kipindi Cha ajali kama kwetu hasa Morogoro Road nk.

Nchi kama Sweden, Finland, Ujerumani,Denmark,Norway, Poland, Ireland,Ufaransa,Italia,Hispania,Uholanz,Uingereza (pamoja na Scotland),Lithuania, Israel, Korea Kusini

Sweden ndiyo mfano maarufu zaidi wa mfumo huu, hasa kwa matumizi ya kizuizi cha waya za chuma katikati ya barabara ili kupunguza ajali za magari kugongana uso kwa uso.

Walipitia Hali kama yetu mpaka kuwa na kauli mbiu iitwayo Vision Ziro KATIKA mpango huo.

M.Byabato
0754527358
 
Mwafrika hata umwekee nini, bado atavunja sheria tu na kusababisha ajali.

Tatizo letu kubwa si barabara tu.

Tatizo letu ni kutotii sheria na utaratibu uliowekwa.
 
Mwafrika hata umwekee nini, bado atavunja sheria tu na kusababisha ajali.

Hakuna mfumo duniani unaweza ondoa kabisa ajali bali unaolazmisha kupunguza uwezekano wa ajali badala ya kutegemea sheria na busara.
 
Hakuna mfumo duniani unaweza ondoa kabisa ajali bali unaolazmisha kupunguza uwezekano wa ajali badala ya kutegemea sheria na busara.
Ajali nyingi zinasababishwa na uzembe wa binadamu.

Kwa hiyo shida kubwa si barabara bali binadamu.

Kama sheria hazifuatwi.

Hata uweke huo mfumo wa 2+1

Kuna mapimbi tu, yatafosi kupita kwenye njia mbili wakati ni muda wao wa kupita kwenye njia moja.

Wewe angalia njia za mwendokasi. Zilitengenezwa specifically kwa ajili ya mabasi ya mwendokasi.

Lakini kuna mapimbi yanatumia njia za mwendokasi. Kupita na magari yao. Wakati kisheria ni kosa.

Kwa hiyo shida yetu kubwa waafrika si barabara bali ujinga wa kutotii na kufuata sheria zilizowekwa.
 
Umeniwahi yaani. Self discipline inaitwa.

Inabidi waafrika wengi wapate exposure waone jinsi wazungu wanazingatia sheria za barabarani.

Yani ukifika zebra cross hata kama ni usiku wa manane na hakuna watu wanavuka, ila red light imewaka lazima usimame.

Sasa sisi huku, taa nyekundu imewaka mchana kweupe kabisa ila kuna mapimbi ndio kwanza yanakanyaga mafuta, wanapita kibati.

Shida kubwa sisi waafrika wala si barabara. Bali ni ujinga wetu wa kutotii sheria za barabarani.

Hata uwekwe mfumo gani, kama watu hawatii sheria za barabarani, ajali zitakuwa ni kila siku na vifo ni daily.
 
KWA TULIPOFIKIA MIAKA 60+ TANGU UHURU,INAFAA;

1. BARABARA ZOTE KUU NCHINI KUWA NJIA NNE AU SITA.

2.MIZIGO YOTE IBEBWE NA TRENI YA SGR.

📌📌TUACHE KUTENGENEZA MATATIZO NA KUANZA KUJIFANYA TUNAYATATUA.SOLUTIONS ZIPO PLAIN AND CLEAR!!!
 
Duh . Hakika. Katikati ya jiji unaweza fikiri ni eneo la kila Mmoja anafanya lake..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…