Wazo kwa serikali; Daraja la Busisi likianza kazi tulipie magari na waenda kwa miguu bure

ommytk

JF-Expert Member
Joined
Jul 30, 2015
Posts
520
Reaction score
1,143
Hili ni wazo tu kwa serikali yangu kuhusu daraja la busisi kwanza nipongeze serikali pili naomba hili daraja liwe la kulipia ila isiwe hela nyingi kiwekwe kiwango kiasi kama kuchangia maendeleo ya serikali yetu Ila iwe kwa magari tu baskeli pikipiki na waenda kwa miguu iwe bureeeeee

Mfano gari ndogo now nalipa 5000 kwanini nisilipie kwa 1000ikaenda kwenye shughuli za maendeleo
 
Unapoleta maendeleo kwa kodi za wananchi halafu tena waendelee kulipia unafanya double taxation. Lengo la daraja hili ni kuwapunguzia wananchi garama za safari na kuwapunguzia umbali wa safari. Sasa wewe unataka tena garama ziendelee kuwepo. Kigamboni wanalia garama za kuvuka kwenye daraja ziondolewe wewe unataka na huku ziwepo.Hayo magari tayari yanakatwa kodi kwenye mafuta na kama ni la kukodi pia analipia kodi ya mapato bado unataka na kutumia daraja ambalo ni kodi yake alipe tena. Tuwaonee huruma watumiaji watarajiwa wa daraja hili. Itafika mahali watu hawataona umuhimu wa miundo mbinu.
 
Kwani la busisi na kigamboni tu? Labda ungependekeza yote nchi nzima yawe ya kulipia?
 
Wasomi maneno mengi ndio maana doto magari uwa anapiga spana
 
Unapoleta maendeleo kwa kodi za wananchi halafu tena waendelee kulipia unafanya double taxation. Lengo la daraja hili ni kuwapunguzia wananchi garama za safari na kuwapunguzia umbali wa safari. Sasa wewe unataka tena garama ziendelee kuwepo. Kigamboni wanalia garama za kuvuka kwenye daraja ziondolewe wewe unataka na huku ziwepo.Hayo magari tayari yanakatwa kodi kwenye mafuta na kama ni la kukodi pia analipia kodi ya mapato bado unataka na kutumia daraja ambalo ni kodi yake alipe tena. Tuwaonee huruma watumiaji watarajiwa wa daraja hili. Itafika mahali watu hawataona umuhimu wa miundo mbinu.
Unajua kwa sasa kivuko tunalipia na hivi kuchangia maendeleo ya serikali yako ni dhambi hii pesa ikipatikana si inaenda kufanya mambo mengine
 
Kuna expenses za kutunza daraja hilo
 
Kwani la busisi na kigamboni tu? Labda ungependekeza yote nchi nzima yawe ya kulipia?
Nenda Dubai hapo kuna daraja na barabara za kulipia na maisha yanaendelea hakuna kudeka kudeka
 
Mada ya hovyo kabisa tangu jamiiforum ianzishwe
 
Kuna expenses za kutunza daraja hilo
Mfano expenses zipi? Hata barabara tunazopita Kuna expenses za kuzituza, mbona hatulipii?

Pia daraja la salendar hakuna expenses? Mbona hatulipii? Daraja la malagarasi hakuna expenses za kutunza? Daraja la kilombero hakuna expenses? Daraja la mkapa rufiji hakuna expenses?

Kichwa ako haina kitu?
 
Unajua kwa sasa kivuko tunalipia na hivi kuchangia maendeleo ya serikali yako ni dhambi hii pesa ikipatikana si inaenda kufanya mambo mengine
Kivuko naelewa kwani kina tumia mafuta na matengenezo ya hapa na pale sasa daraja kweli ?
 
Kuna expenses za kutunza daraja hilo
Hizo garama sitayari kuna kodi iliyotozwa kwenye mafuta hapo awali ilikuwa inatozwa kwenye namba za magari? Kuna madau kauliza hapa salenda, Jangwani,Ruvu,Kilombero,Wami,Mto Pangani, Mto Kagera ,mtwara kule Mtambaswala, Malagalasi ,Mbuyuni pale mpaka wa Iringa na Morogoro, huko hakuna garama?
 
Nenda Dubai hapo kuna daraja na barabara za kulipia na maisha yanaendelea hakuna kudeka kudeka

Kwanini twende Dubai ndugu wakati Burundi tu kumetushinda?

Pendekeza zote hapa hapa nchini ziwe za kulipia!
 
tusi
Nenda Dubai hapo kuna daraja na barabara za kulipia na maisha yanaendelea hakuna kudeka kudeka
we wepesi wa kulinganisha na nchi za wenzetu upande mmoja? je umekutana na vijana wakiosha vioo vya magari dubai? je umekutana na shimo barabarani au matuta? je umeme unakatika katika? Tukilinganisha tuangalia pande zote siyo kwenye kukamua tu. Dubai wanabandari Sharja hakuna mfano, wana airport hakuna mfano, wana jengo refu duniani, kodi ni kama hakuna nchi yao kwani wanategemea utalii na bandari pamoja na usafiri wa anga. Bei ya mafuta ni ndogo sana na ndiyo maana magari yao engine kubwa na ni petroli. Dubai wamekausha bahari na kujenga majengo ya kifahari ambapo matajiri toka pande mbali mbali za dunia wamenunua huko. Dubai kuna joto kali lakini huwezi lisikia labda utoke nje ya jengo au gari maana ni full aircondition na umeme full time. Dubai barabara hakuna foleni ni fly overs za nguvu. Sasa sisi kajamba nani huku hela ya mkate tu ni shida ndiyo unataka tulinganisha na wenzetu? come on.
 
Back
Top Bottom