Wazo kwa serikali; Daraja la Busisi likianza kazi tulipie magari na waenda kwa miguu bure

Wazo kwa serikali; Daraja la Busisi likianza kazi tulipie magari na waenda kwa miguu bure

Hili ni wazo tu kwa serikali yangu kuhusu daraja la busisi kwanza nipongeze serikali pili naomba hili daraja liwe la kulipia ila isiwe hela nyingi kiwekwe kiwango kiasi kama kuchangia maendeleo ya serikali yetu Ila iwe kwa magari tu baskeli pikipiki na waenda kwa miguu iwe bureeeeee

Mfano gari ndogo now nalipa 5000 kwanini nisilipie kwa 1000ikaenda kwenye shughuli za maendeleo
Waweke bakuli pale wazalendo wanaotaka kulipia walipie, walipa kodi wanaosema washalipia kwa kupitia kodi zao wapite bure.

Kila mtu apate anachotaka.
 
Tunalipiaje wakati Kodi zetu ndio zimefanya kazi hapo. Hata kama ni mkopo sisi ndio tutalipia kupitia Kodi mbalimbali tunazolipa
 
Mleta mada utapingwa sana lakini uhalisia ndio tunakoelekea ,na dunia ya kwanza iko huko.
Hata hapo Kenya barabara unalipia,achilia mbali Uchina
 
Hakuna Barabara au daraja likajengwa kwa kodi za wananchi likawa la kulipia hizo mnazotaja ni PPT. Hivyo hapo kigongo busisi ni Free labda mtunge sheria Mpya za kuruhusu hilo
 
Katika kitu CCM wamewaweza ni kuwanyima Elimu. Yani hapo anahisi hilo daraja ni hisani serikali imefanya.
 
Tangu lini kivuko cha Busisi watu na magari vikapita bila kulipia? Kama ferry inalipiwa SHS 500 kwa nini daraja lïsilipiwe?
 
Hili ni wazo tu kwa serikali yangu kuhusu daraja la busisi kwanza nipongeze serikali pili naomba hili daraja liwe la kulipia ila isiwe hela nyingi kiwekwe kiwango kiasi kama kuchangia maendeleo ya serikali yetu Ila iwe kwa magari tu baskeli pikipiki na waenda kwa miguu iwe bureeeeee

Mfano gari ndogo now nalipa 5000 kwanini nisilipie kwa 1000ikaenda kwenye shughuli za maendeleo
Bwana tajiri umesikika Ila kina sisi wengine majority ni pangu pakavu
 
Mleta mada utapingwa sana lakini uhalisia ndio tunakoelekea ,na dunia ya kwanza iko huko.
Hata hapo Kenya barabara unalipia,achilia mbali Uchina
Tusipende kujilinganisha na wenzetu inapofika kwenye kukamuana mbona kwenye unafuu hatusemi tuwe kama wenzetu mfano bando wenzetu ni cheap na faster kutumia Data
 
Back
Top Bottom