kijana13
JF-Expert Member
- Sep 24, 2013
- 1,981
- 3,631
Habarini wakuu, kutokana na tatizo la upatikanaji wa mitaji na Ajira kuwa ngumu kwa vijana,kuna wazo nataka toa, kama lilishawahi tolewa humu mnaweza nipa comments au kama halifai pia nahitaji maboresho.
Maana baadhi yenu mmekuwa mkisema hapa jujwaani nina 1,2,3 mill etc nishaurini nifanye biashara gani? Baadhi huwa mnapata mawazo mnayafanyia kazi na wengine mnakosa mawazo ya kufanya.
Upande wa pili wa shillingi kuna Baadhi ya vijana wanamawazo mazuri ya biashara na wengine wanafanya biashara katika kilimo,utengenezaji bidhaa za vyakula na vya matumizi ya nyumbani etc.lakini hawana mitaji.
Nyie mlio na fedha hamjui mtazifanyia biashara gani kuna vijana wenzenu wa wanamawazo mazuri au pia wengine wapo kwenye biashara.
Nashauri mfanye partneship ya namna ntakayoieleza hapa chini ambayo mtakuwa na uhakika wa kipato kila wiki au mwezi.
Katika biashara ndogo ndogo na za kati baadhi ya watu wanafanya partnership yaan watu wawili etc wote wanakuwa wasimamizi na waendeshaji wa biashara , Dhana hii imekuwa ikileta changamoto ya partners kuwa na migogoro hasa pale Mmoja anapokuwa active na mwingine hayuko active etc na kujikuta uhusiano wa kibiashara unakufa. Why jukumu la uendeshji na usimamizi wa biashara asiachiwe Mmoja.?
MAPENDEKEO
Uwepo mkataba wa kuandikishana kukopeshana vifaa kwa makubaliano yenye terms kwa kuangalia thamani ya kifaa plus interest, muda wa malipo, na utaratibu wa malipo (mwezi au wiki etc) na mtoaji kifaa lazima ujiridhishe na viability ya business. Na masharti mengine.
Mbona boda boda wameweza mmiki anamkabidhi mwendesha bodaboda baada ya muda fulani pikipiki inakuwa ya mwenye boda boda??
Naamini hata kwa biashara zingine inawezekana.
Mfano.
1).car wash.kuna baadhi ya vijana wanamaeneo au wanauwezo wa kupata eneo la ajili ya biashara hiyo lakini wanakosa fedha za kununulia vifaa kama compresor.etc
2). Saluni ya kunyoa na kutengeneza nywele.
3).watengenezaji wa keki na mikate, ice cream,clips,etc
4).wafugaji wa mifugo na ndege
5).wakulima wa mazao,mboga mboga,matunda etc..
6).wafugaji wa samaki.
7).na biashara zingine ambazo sijaorodhesha.
Hitimisho
Napendekeza watu wajitokeze zaidi kutafuta mabusiness Patner kwa biashara wanazozipenda na kuingia makubaliano ya mkataba wa vifaa vya uzalishaji biadhaa na huduma.
Nakaribisha michango, maboresho na kukosolewa.Asnteni.