Wazo la biashara linapotea kila nikiwa na pesa

kaligopelelo

JF-Expert Member
Joined
Jun 20, 2013
Posts
2,832
Reaction score
4,070
Naombeni msaada nifanyeje niweze kudhibiti wazo la biashara?
ninakuwa na malengo ya biashara kabla sijawa na mtaji. Lakini kila nikipata hela najikuta nachanganikiwa nisijuwe nifanye biashara gani. Kila biashara nahisi nitaangamiza pesa.
 
Kwakweli nilikua siandiki vipaumbele vyangu,nilikuwa nategemea kutunza kila kitu kichwani. Naanzia hapa kuufanyia kazi ushauri wa kuweka kumbukumbu kwa maandishi.
 
Kwakweli nilikua siandiki vipaumbele vyangu,nilikuwa nategemea kutunza kila kitu kichwani. Naanzia hapa kuufanyia kazi ushauri wa kuweka kumbukumbu kwa maandishi.
 
anza na saving kwanza achana na biashara ukiwa na uwezo wakusave someday utaizuia biashara yako isianguke lakini kama huna tabia ya saving hata ukianzisha biashara itakufa and by saving lazima upunguze matumizi yasiyokuwa na ulazima ...pia usisahau kuweka record ya matumizi yako mali bila daftari hupotea bila habari....nisamehe kwenye uandishi wangu sijatulia

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Haina shida mkuu nimekuelewa sana
 
Kwanza, anza kufanya Dua kwa Mwenyezi Mungu, ili akuepushe na hiyo hali katika siku zijazo.

Pili, tafuta wazo la biashara, kisha lifanyie analysis like SWOT, Marketing...and set target(s).

Tatu, be committed kwenye hilo wazo lako....mwisho ingia mzigoni.

I wish you all the best....God bless you.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu unahitaji mentor wakukuongoza kupata focus.

Nikwambie tu.

Hadi sasa wala huamini katika wazo lako la biashara ndiyo maana haupo na msukumo wakuanza NOW.

Ukiona wewe ni mtu wa excuses kila mara hiyo maana yake hauna burning desire kwenye ujasiriamali.

Ili uwe successful kwenye business unahitaji uwe na focus ya hali ya juu sana.

Na haiishii hapo.

Unahitaji uuze.

Usipojua kuuza you are wasting time.

Biashara ni wateja.
 
Nahisi kuna mengi kwako ambayo yatanifaa,naomba ukipata muda uweze kunifungua zaidi mkuu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…