Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Ndio aende vijiji vya kilombero huko kuna fursa nyingi. mfano tuliani, mngeta, mlimba, Chitamlela, mang'ula n.k akiwa na mil 3 inatosha kwa kuanzia.
Baada ya miaka miwili aje hapa kutupa mrejesho.
mkuu fanya biashara ya samaki wabichi unatoa mtera unapeleka kweny mabucha hapo mawenzi utanishukulu
Hii unamaanisha kuwauzia machinga auKwa huo mtaji kama unataka kuishi nao mjini basi kodi kibanda cha machinga kingalu sokoni, weka bidhaa tofauti tofauti, weka kipaza sauti... Hukosi ya kula na kuendeleza mtaji mpaka kuja kumiliki fremu
Nimeipenda hii..unataka shughuli ya kukuingizia kipato kila uchwao au una utayari iwe inakuingizia baada ya muda Fulani ..
Kama ni ya kila uchwao ( biashara asubuhi jioni mahesabu ) jaribu biashara zifuatazo
1. Bodaboda - comes with highest risk
2. a) Goli la chips/ndizi/mishikaki/kuku - mwanzoni kulingana na eneo utakalojiset itakuwa ngumu mpaka pakishazoeleka
2. b) Goli la chapati/maharage/supu ya ng'ombe ...bado kwa Moro mjini na viunga vyake vijiwe hivi havijasambaa sana
Kama unataka ya msimu nunua nafaka kipindi cha mavuno weka store then uza baadae, hii inataka umakini wa quality checking unaponunua, nafaka kama mpunga, mahindi, maharage , mtama (mweupe au mwekundu) n.k
Biashara nyingine kwa mtaji wako nenda minadani nunua mbuzi safirisha kupeleka Dar, (Anza na mbuzi wachache) ila kwanza pata taarifa na maarifa namna ya kuwafikisha, vibali, n.k