Wazo la biashara ya mazao na mifugo

Wazo la biashara ya mazao na mifugo

MC RAS PAROKO

JF-Expert Member
Joined
Feb 14, 2013
Posts
623
Reaction score
606
Wazo la biashara ya MAZAO na MIFUGO

Niende moja kwa moja katika mada, nimekuwa nikifuatilia kwa muda mrefu masuala ya mazao na mifugo na katika hayo nimepata taarifa muhimu sana na nikaona nisiwe mchoyo niweze kushiriki nanyi kwa pamoja tuinue hali zetu za kiuchumi.

Ukiangalia katika mwaka kuanzia miezi ya 7, 8 na 9 bei ya mazao (mahindi) inashuka sana maeneo mengi katika nchi, hii ni kutokana na wakulima wengi kuwa wanavuna na kitaalam supply ikiwa juu zaidi ya demand bei hushuka na ndio kinachotokea kwa wakati huo, yaani wauzaji ni wengi kuliko wanunuzi.

Kulingana na mtegemeano uliopo katika sekta ya kilimo na ufugaji bei za mifugo (ng'ombe) zitapanda, bei ya mahindi itashuka hii ni kwa sababu majani ni mengi kipindi cha mavuno na hupelekea wanyama kunona vizuri. Wakati mahindi yanapanda bei kuanzia mwezi wa Nov,Dec,Jan tarajia bei ya mifugo kushuka sana sababu ni ile ile kiangazi kinakua kimekausha malisho mengi ya wanyama na kupelekea mifugo kukonda na wauzaji ni wengi kuliko wanunuzi wachache.

Utaweza kutengeneza pesa kwa njia hii wakati mahindi yameshuka bei, nunua ya kutosha na uweke store, yakipanda bei ukaona tayari ukiuza itakupa faida uza na ununue mifugo na kuilisha kwa miezi michache na bei itaporudi juu tena uza mifugo rudisha mtaji kwenye mazao. Utaendelea na mzunguko wa hivi mara kwa mara na utajikuta unatengeneza faida nzuri kwa kipindi cha mwaka mzima. Naomba kuwasilisha. TIA
 
Akili sana wewe jamaa
 
Back
Top Bottom