Ninataka kuuza mchele kwenye pakeng. Kuanzia kilo hadi kilo 25kg, ila sijui wapi nianzie, na mtaji wangu sio mkubwa sana, mwenye kuweza kunisaidia kwa hili, aniambie.
Ukiwa na nia haswa ya dhati kufanikiwa ni wewe kuingia chimbo kusaka habari ..
Usiogope kuingia gharama ..hizo gharama zitarudi tu baadaye.
Anza kupata info kwa wanaofanya hizo mishe..ikiwezekana muungishe then muulize ameanzaje. Ingawa hawatakupa dondoo zote..Changamoto zake na mzigo mzuri unapatikana wapi...
Nafahamu wateja wako ni kina nani..(uswazi hatununui mchele ulopakiwa mkuu)..
Ukishamaliza hayo ndo uje humu ujazilizie tu...
ninawazo la biashara, ninataka kuuza mchele kwenye pakeng. kuanzia kilo hadi kilo 25kg, ila sijui wapinianzie, na mtaji wangu sio mkubwa sana,.. mwenye kuweza kunsaidia kwa hili, aniambie..
-> Fanya tafiti kujua bei za mchele pale unapotarajia kuuza
-> Fanya tafiti ya bei za jumla unapotaka kununulia au wauzaji wenzio wanapochukulia
-> Angalia faida yako ni kiasi gani baada ya kujua gharama za uendeshaji kwa kila kilo ya mchele
- > Nunua mchele wa jumla, gunia kadhaa ulete unapofanyia biashara, nunua mzani na vifungashio, paki aanza kujitangaza mitandaoni kwenye simu, kwa wanunuzi wa mara kwa mara kama wapishi/mama ntilie, migahawa nk na kuwajulisha wateja bidhaa ipo....
- > 'Brand' vizuri vifungashio vyko na upeleke kwenye mini/super-market kama wanakubali
-> Huduma ya 'delivery' iwepo ili kuwafikia wateja wengi zaidi
-> Ongeza bidhaa zinazoendana kama maharagwe, mafuta ya kula n.k...
Ni muhimu kujua wanaofanya biashara eneo unalokusudia wanauzaje