Wazo la biashara

Wazo la biashara

preciouse

Member
Joined
Nov 6, 2012
Posts
46
Reaction score
12
Hi Bandugu,
kutokana na hali ilivyo ya ajira kutoeleweka najaribu kufikiria cha kufanya kujikimu kimaisha sipati jibu, eti kwa mfano una shilingi milioni moja hapo unaweza anzia biashara gani?
 
Zinazidi 1000. Swali lazima lianze na wewe unajua au unaweza nini? Je, unajua kuosha magari? Kuuza nyanya? kulima? kufundisha chekechea, shule ya msingi, au nk. TUKIJUA UNAWEZA, UNAJUA NA UNAPENDA NINI? Tunaanza kukushauri kuanzia pale. Huwezi kufanya biashara kwenye kitu usichokijua kabisa. Utaumia. Wewe unapenda na unajua nini? Tuanzie hapo.
 
Hi Bandugu,
kutokana na hali ilivyo ya ajira kutoeleweka najaribu kufikiria cha kufanya kujikimu kimaisha sipati jibu, eti kwa mfano una shilingi milioni moja hapo unaweza anzia biashara gani?

kanda chapati zina wateja sana.
 
...Fikiria kuhusu kufungua mgahawa mdogo. Daima dumu ni Lazima watu wale. Tafuta eneo lenye shughuli shughuli. muambie shemeji ama tafuta mtu apike chai ya rangi, maziwa, vitumbua, andazi, chapati, supu, maharage. ukiweza mchana pika ugali, wali na ndizi. kama una ka-friza, weka maji, soda, juisi, maziwa nk. Ukizingatia usafi ni lazima utatoka tu ndugu hata kama itachukua muda mrefu kidogo...:smiling:
 
Hili limekuwa ni tatizo kubwa sana katika ustawi wa jamii yetu; mfumo wetu wa elimu hautuandai katika kujitegemea na badala yake unaelekeza sana kuajiriwa. Kulingana na tatizo hili tumeanzisha programu ya kusaidia watu kuanzisha na kuendeleza biashara ambapo kwa majaribio tunaanza mkoani Dodoma. Programu hii ni kwamba mtu anapokea mafunzo ya mbinu za biashara kwa mwezi mmoja na baada ya hapo atatakiwa kufungua biashara ambayo itapata usimamizi kwa miezi 11. Programu hii imeanzia Afrika ya kusini na kwa sasa imekuwa na mafanikio makubwa nchini Kenya ambapo kati ya washiriki 600 waliopitia programu hii asilimia 80 biashara zao zinaendelea vizuri.

attachment.php
 

Attachments

  • Flyer2.png
    Flyer2.png
    41.8 KB · Views: 294
Back
Top Bottom