Wazo la Kujenga mabwawa kila kata linaweza kutuvusha kwenye kilimo cha umwagiliaji

Wazo la Kujenga mabwawa kila kata linaweza kutuvusha kwenye kilimo cha umwagiliaji

mgt software

JF-Expert Member
Joined
Nov 1, 2010
Posts
13,778
Reaction score
7,145
Wana JF

Kuna wakati fulani mtu alikuja na wazo la kujenga mabwawa kila wilaya lakini kiuhalisia kuna wilaya kubwa sana zinakaribia kuitwa mkoa kutokana na ukubwa wa eneo lakini wakazi wachache.

Naona hili linaweza kufeli na serikali isipate kinachokusudiwa. Ili kuwa na kilimo chenye tija, tunatakiwa kujenga mabwawa mengi kila kata , kwingine kata zinazokaribiana zinaweza kushea maji hayo.

Tatizo la lishe nalo linaweza kupungua kama tukipandikiza samaki kwenye mabwawa hayo. Tayari serikali inaweza kutengeneza miundo mbinu ya umwagiliaji tukaepuka kukauka kwa mazao.

Tanzania tumechoka lulialia eti tumepews maji mengi lakini tunayaachia yanamwagilia Bahari badala ya kumwagilia mimea yetu.
 
Wana JF

Kuna wakati fulani mtu alikuja na wazo la kujenga mabwawa kila wilaya lakini kiuhalisia kuna wilaya kubwa sana zinakaribia kuitwa mkoa kutokana na ukubwa wa eneo lakini wakazi wachache. Naona hili linaweza kufeli na serikali isipate kinachokusudiwa. Ili kuwa na kilimo chenye tija, tunatakiwa kujenga mabwawa mengi kila kata , kwingine kata zinazokaribiana zinaweza kushea maji hayo. Tatizo la lishe nalo linaweza kupungua kama tukipandikiza samaki kwenye mabwawa hayo. Tayari serikali inaweza kutengeneza miundo mbinu ya umwagiliaji tukaepuka kukauka kwa mazao. Tanzania tumechoka lulialia eti tumepews maji mengi lakini tunayaachia yanamwagilia Bahari badala ya kumwagilia mimea yetu.
Hizi zote ni mbwembwe..serikali inapaswa inanzishe kongani za viwanda kila wilaya...watu waanze kuongeza thamani bidhaa zao.

Tuwe kama china.

#MaendeleoHayanaChama
 
Hizi zote ni mbwembwe..serikali inapaswa inanzishe kongani za viwanda kila wilaya...watu waanze kuongeza thamani bidhaa zao.

Tuwe kama china.

#MaendeleoHayanaChama
Tusipoanza na kilimo cha umwagiliaji lawmaterial tutapata wapi? Tutachakata nini. Mikoa mingi kilimo cha alizeti kinawezekana sana na ngano lakini kukosekana kwa maji ndio shida. Gharama za kujenga mabwawa sio kubwa ukilinganisha na kitakachoenda kutokea
 
Huu uzi unastahili kuwa uzi bora kabisa wa wiki.
Haya yanayoandikwa hapa kama yatafanyiwa kazi,hakika maendeleo yatapatikana kwa muda mfupi.
1. Mabwawa kila kata kwa ajili ya kilimo cha umwagiliaji na kunywesha mifugo.
2. Viwanda kila wilaya kwa ajili ya kuprocess mazao yapatikanayo sehemu husika.
3. Masoko ya bidhaa zinazozalishwa.
 
Wana JF

Kuna wakati fulani mtu alikuja na wazo la kujenga mabwawa kila wilaya lakini kiuhalisia kuna wilaya kubwa sana zinakaribia kuitwa mkoa kutokana na ukubwa wa eneo lakini wakazi wachache. Naona hili linaweza kufeli na serikali isipate kinachokusudiwa. Ili kuwa na kilimo chenye tija, tunatakiwa kujenga mabwawa mengi kila kata , kwingine kata zinazokaribiana zinaweza kushea maji hayo. Tatizo la lishe nalo linaweza kupungua kama tukipandikiza samaki kwenye mabwawa hayo. Tayari serikali inaweza kutengeneza miundo mbinu ya umwagiliaji tukaepuka kukauka kwa mazao. Tanzania tumechoka lulialia eti tumepews maji mengi lakini tunayaachia yanamwagilia Bahari badala ya kumwagilia mimea yetu.
Watu wangu wanaangamia kwa kukosa maarifa.
 
Huu uzi unastahili kuwa uzi bora kabisa wa wiki.
Haya yanayoandikwa hapa kama yatafanyiwa kazi,hakika maendeleo yatapatikana kwa muda mfupi.
1. Mabwawa kila kata kwa ajili ya kilimo cha umwagiliaji na kunywesha mifugo.
2. Viwanda kila wilaya kwa ajili ya kuprocess mazao yapatikanayo sehemu husika.
3. Masoko ya bidhaa zinazozalishwa.
Kuna nchi kama Vietnam mara nyingi viongozi wetu wanaitumia kama mfano bora wa maendeleo ya kilimo lakini mipango yote inahishia kwenye makaratasi. Mimi ni mdau sana wa kilimo changamoto ya ukame jinsi inavyonitesa, laiti kama ningepata maji, hakuna siku ningekosa kuzalisha kitu. Mama ametoa fedha nyingi karibu mara nne alizokuwa wanazitoa watangulizi lakini hizi zitaliwa na wajanja bila kuwafikia walengwa. Lengo kuu linaweza lisitimie ikiwa ADB Bank (benki ya kilimo) isiporekebisha masharti ya ukopeshaji. Na masharti ya benk husika karibu yanafanana na yale ya Bank za biashara. Bond security inayohitajika haina uhalisia na maendeleo ya mkulima wa chini. Ili ulime kwa faida lazima pia ufuge. Kuna mmimea nyingine samadi ni ya lazima sana.
Pia watu wengi wemegundua mbolea ya kuku ni bora zaidi kuliko hizi za madukani lakini upatikanaji wake ni shida. Tukiwa na mabwawa tukapata mahindi ya kutosha, alizeti na mabaki ya samaki tiyari tunaweza fuga kuku bila tatizo. Na kuku wenye tija ni kuroiler ni wepesi kufungwa.
 
Kaa ujue serikali haitaki wananchi wake wapate maendeleo adi wajisahau kama hamna shida ,wanatengeneza shida Ili mjue Kuwaomba misaada ndio pale viongozi Wana omba kura wakipata wanakimbia .
 
Point nzuri Sana hio tusisahau na kuhifadhi mazingira yetu kwa kupanda miti mingi.
likifanyika hilo hata mm nitarudi kijijini kulima ila wasitupangie tukauze wapi na kwa bei gani.pia nitahamasisha watu kuongeza nyororo wa thamani wa mazao hayo.
 
Wana JF

Kuna wakati fulani mtu alikuja na wazo la kujenga mabwawa kila wilaya lakini kiuhalisia kuna wilaya kubwa sana zinakaribia kuitwa mkoa kutokana na ukubwa wa eneo lakini wakazi wachache. Naona hili linaweza kufeli na serikali isipate kinachokusudiwa. Ili kuwa na kilimo chenye tija, tunatakiwa kujenga mabwawa mengi kila kata , kwingine kata zinazokaribiana zinaweza kushea maji hayo. Tatizo la lishe nalo linaweza kupungua kama tukipandikiza samaki kwenye mabwawa hayo. Tayari serikali inaweza kutengeneza miundo mbinu ya umwagiliaji tukaepuka kukauka kwa mazao. Tanzania tumechoka lulialia eti tumepews maji mengi lakini tunayaachia yanamwagilia Bahari badala ya kumwagilia mimea yetu.
Sio kila kata bali kila sehemu yenye potential ya kilimo cha umwagiliaji..

Serikali inaanza mwaka huu kujenga mabwawa ya kilimo kwenye maeneo ya kimkakati,zaidi ya bil.230 zimetengwa kwa Kazi hiyo kupitia Wizara ya Kilimo..

Wizara ya maji na mifugo nao Wana miradi yao ya mabwawa.
 
Tusisahau isimamizi mzuri wa hayo mabwawa, yasije yakawa pahali pa kuzalisha mbuu wengi na ongezeko la maradhi ya malaria na mengineyo.
 
Sio kila kata bali kila sehemu yenye potential ya kilimo cha umwagiliaji..

Serikali inaanza mwaka huu kujenga mabwawa ya kilimo kwenye maeneo ya kimkakati,zaidi ya bil.230 zimetengwa kwa Kazi hiyo kupitia Wizara ya Kilimo..

Wizara ya maji na mifugo nao Wana miradi yao ya mabwawa.
Kama Mama kapata wataalum wa kufanya hivyo basi atakuwa rais bora kila wakati. Nchi nyingi zimejikomboa kitokana na kilimo ndio maana hata matajiri wengi wanaojua fursa wametajirika kama wachuuzi wakilangua vitu kwa wakulima. Tukilima pia Mama angeweka kwenye mikakati ya ufugaju
Kwa maana mbilea hii ya viwandani inatesa sana wakulima
Lakini ukiwa na mifugo unaweza ukafanya mengi. Nilikuwa nikifuatilia wakulima wa mbiga mboga kwa sasa hawatumii kabisa mbolea za viwandani. Wanatumia mbilea ya kuku. Ndio maana hata mavhicha na maranda ya mbao yamepanda bei kwa sababu wafugaji wanayatandazq ndani ili kutengeneza mbolea nyingi inayotokana na kinyesi cha kuku
 
Back
Top Bottom