Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 34,256
- 44,597
Nilikuwa sijawahi kuutafakari sana huu msemo. Sikuelewa kwanini kwa waoga wacheke na mashujaa walie. Sasa nimeelewa.
Wapo wanaochekeana na kupongezana..wanapigiana saluti na kugongeana "high five". Tunawaona wanacheka lakini nyuso zao zimejaa hofu..hoja zao zimejaa vitisho...kauli zao ni za kibabe..nguzo zinategemea risasi. Wanataka kulazimisha kupendwa na kukubaliwa...hawataki wahojiwe au waulizwe...ni waoga.
Ila kwa mashujaa ni kilio. Wataliliwa na kukumbukwa. Nakumbuka vita ya Uganda...tulilia..lakini bado watu walijiandikisha...waliona fahari kwa ajili ya nchi yao..
Tuliimba.."askari eeeh vitani eeh" tuliposonga mbele kwenye hatua kumi na tano za Gwaride tulipiga kelele.."hima hima...!!" Sikuelewa. Sasa naelewa. Misiba imeenda kwa familia za vijana na watoto wetu..waoga wanaogopa hata kutoa miili...
Lakini bado wanacheka...wanatishia kuua tena...waoga wamejifunza kuua na mashujaa wamejifunza kufa... mmoja atapeleka kilio na mwingine kicheko..kwa kuwaangalia unajua yupi ni yupi.