Wazo la Leo: Tatizo ni Hatujui Watafanya Nini...

Wazo la Leo: Tatizo ni Hatujui Watafanya Nini...

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Joined
Mar 10, 2006
Posts
33,771
Reaction score
41,027
Kilichoahidiwa na CCM na kutekelezwa kwa miaka siting na kitu kinajulikana. Uzuri na Ubaya wa sera zake unafahamika. Watanzania wanajua maisha chini ya CCM. Hakuna kiongozi wa CCM kwa sasa (awe serikalini au chamani) ambaye hajulikani na Watanzania...

Hapa ndipo kilipo kibarua cha upinzani Tanzania. Wanawezaje kuwashawishi walikatae jini walilolizoea na kulijua halafu walifungulie mlango wa nyumba lile wasilolijua...
 
Tulimiss uchambuzi makini wa kibabe kutoka kwako mwamba kabisa mzee mwanakijiji. Huwa ukosei maono yako yanaishi nakumbuka ulichosema wakati wa dili haramu la kuiuza chadema iliyofanywa na mbowe na tundu lissu ulinyooka matokeo tunayaona baada ya miaka 8
 
Upinzani wapaswa kujitambua wajibu wao.

Huu ni wakati wa upinzani kuketi na kufanya tathmini na kutengeneza stratejia ingine.

Lakini wapiga kura hawana shida wao wataka kusikiliza upinzani wasema nini kipya na sera zao ni zipi na je zauzika?

Upinzani uache danadana kulumbana kupotezeana muda ni lazima uwe makini ni aina ya siasa inazozifanya.

Wapiga kura waondolewe hofu ya upinzani na kisha wapewe uhakika wa maisha baada ya CCM.

Matatizo wanoyaona wananchi ni uchumi ulodorora, mfumuko wa bei, ukosefu wa ajira, mishahara duni na kuzidi kupanda kiwango cha ukiukwaji wa haki za binadamu.
 
Kilichoahidiwa na CCM na kutekelezwa kwa miaka siting na kitu kinajulikana. Uzuri na Ubaya wa sera zake unafahamika. Watanzania wanajua maisha chini ya CCM. Hakuna kiongozi wa CCM kwa sasa (awe serikalini au chamani) ambaye hajulikani na Watanzania...

Hapa ndipo kilipo kibarua cha upinzani Tanzania. Wanawezaje kuwashawishi walikatae jini walilolizoea na kulijua halafu walifungulie mlango wa nyumba lile wasilolijua...
kwamfano viongozi wa upinzani badala ya kushawishiana na kuungana mkono, mpinzani mlevi moja wa chama ndani ya upinzani huohuo ana chochea chuki na uhasama dhidi ya vyama vingine vya upinzani badala ya kuhubiri umoja.

Nadhani leo waTanzania wamefahamu kwamba hakuna chama cha upinzani nchini chenye nia ya kushika dola 🐒
 
Back
Top Bottom