Upinzani wapaswa kujitambua wajibu wao.
Huu ni wakati wa upinzani kuketi na kufanya tathmini na kutengeneza stratejia ingine.
Lakini wapiga kura hawana shida wao wataka kusikiliza upinzani wasema nini kipya na sera zao ni zipi na je zauzika?
Upinzani uache danadana kulumbana kupotezeana muda ni lazima uwe makini ni aina ya siasa inazozifanya.
Wapiga kura waondolewe hofu ya upinzani na kisha wapewe uhakika wa maisha baada ya CCM.
Matatizo wanoyaona wananchi ni uchumi ulodorora, mfumuko wa bei, ukosefu wa ajira, mishahara duni na kuzidi kupanda kiwango cha ukiukwaji wa haki za binadamu.