Sababu hata wewe unazijua mkuu usivunge. Hivi mkuu una mtoto?
Kama una mtoto na kama unampenda kweli unaweza mficha urithi wake uliko
Ili iwe nini sasa?
Hivi mkuu kwani Mungu hakujua shetani atakuja kumdanganya Hawa? Maana bibilia kwa mfano inasema ndo mwanzo wa dhambi, nyoka kumdanga hawa na kumpa tunda , na kwanini sasa hakumwangamiza shetani na hawa wote aumbe mwingine wapya? Ona tunavyoteseka sasa,, ee hakujua?
Nasikitika kuudhuri hospital moja na wachungaji wangu wa kanisani na watoto wao na wake zao , tena watumishi wengine wanaumwa magonjwa ya hatarii kwani Mungu haonagi huruma hata kwa Walisha kondoo zake?
Makanisa yamekuwa mengi mno mno , misimiti nayo wana madhebu yao.
Kwanini Mungu asijitokeze wote atupe Njia ya kumuombea? Aje kwa wazi kabisa sii kwenye ndoto aje kabisakabisa kila mtu ajue bwana ee Njia ya mbinguni ni hii kuwepo na kitabu kimoko sasa mara kurani mara bibilia aah nachanganyikiwa mkuu
Sababu ni nyingi ila tumerithi na kulishwa uoga na hofu kuu