Wazo langu...

Wazo langu...

AkiliMingi AM

Member
Joined
Jul 5, 2020
Posts
88
Reaction score
60
Habari wana JF

Mimi ni mkazi wa moshi elimu yangu kidato cha sita, kuna wakati nikiwa shule nilikuwa nasumbulia kichwa na mambo kadha ambayo nataka niyaweke hapa leo.

Kwanza kabisa ni kupoteza muda, niliishi nikiamini kuwa shule inanipotezea muda kwa kuwa nimejikuta nikitumia muda mwingi kupambana na shule, na kupambana kwenyewe na shule ni kwa sababu ya mzazi anataka uwe kama mtoto wa fulani ambaye mtoto wake ni dactari labda sasa unakuta akina sisi hatuna ndoto na shule kwaio tunasoma mpaka unafikisha miaka 30 unamaliza chuo akili imedumaa kiutafutaji hujui kupambana na maisha unaanza kukaa kwenu alafu inakuwa fedhea mtaani.

Jambo lingine ni biashara gani niweze kufanya yenye kuleta matokeo mazuri,niliwahi kuwaza kufanya biashara zifuatazo,

1) Saluni ya kiume.
Kwamba hapa ninakuwa namlipa msimamizi wa iyo saloon na kulipa kodi ya frame ya biashara.

2) Kufungua banda wired money
Hapa nitasimamia pekeyangu, nitakacho lipa ni kodi ya frame ya buashara.

3) Kuuza vinywaji (Pombe).
Hapa nitaeka mdasa wa kuhudumia hivyo nitamlipa, nitalipa pia sehemu ya biashara bado kuna kodi ya mapato nk.

Hapo ushauri wenu na idea zenu mpya ambazo zinaweza nijenga ki namna fln.

Je, ni kweli shule inapoteza muda?
 
Nenda shule kasome wewe ukiyumba utaishia kuwa barmaid/bartender. Shule shule shule ndio mengine yaendelee.
 
Sasa kuna haja gani ya kuacha shule wakati biashara zenyewe unaweka watu wasimamie, acha ujinga wewe soma kwanza!
 
Achana na shule fanya biashara..

Kwenye business utaboa fasta, kama utakuwa mvumilivu.

Mimi niliacha chuo mwaka wa pili, now na make c chini ya 2.5M kila mwezi, nina biashara c chini ya tano mjini hapa.

Ila nilianza kwa ku struggle sana.
 
Back
Top Bottom