Wazo langu

Wazo langu

kassamali

JF-Expert Member
Joined
Jan 11, 2010
Posts
214
Reaction score
40
Habari zenu waTanzania wenzangu
Hivi juzi juzi nimepata bahati ya kufuatilia mienendo ya safari za Mtanzania mwenzetu Kinana japo mimi si mfuatiliaji sana wa mambo ya siasa ni juzi tu nimepata kumfahamu kabla ya hapo siku jua yeye ni nani katika nchi hii ok si suala langu ila baada ya hapo nimegubikwa na wingu kubwa la maswali yasiyo na majibu.Nimejaribu kupiga hesabu ya safari zao chache nilizobahatika kuziona kwa mfano moja ya safari ambao wanaonekana kutumia ngege binafsi ya kukodi nilipo piga hesabu nikaona safari ya kwenda na kurudi kwa ndege tu imegharimu dola 6000 kwa ngege ya kukodi hapo sijajumlisha malazi,na mengine chungu mzima inaonekama kwa siku wanatumia kama milioni 20 au zaidi.

MASWALI YANGU:
Kwa nini tunatumia pesa yingi kiasi hicho kutangaza siasa kuliko kufanya yale ambayo siasa imeahidi kuyatimiza????hivi akina nani wanachongia hizi siasa?Wanapata wapi pesa hawa?Wiki mbili nilikuwa natoka Dodoma kwa basi kuelekea Singida mbele ya macho yangu mtoto mdogo kafariki akiwa na mama yake kwa kile kilichojulikana mama mtu hakuwa na shilingi 1500 ya kitanzania kumtibia mtoto.Je maisha yetu yanathamani gani???shilingi elfu moja mia tano????

Yangoswe mwachie ngoswe...sitaki kugusa nini kinafanya ndani ya siasa manake tatizo si CCM au Chadema au Cuf tatizo lipo na lazima litafutwe liweke hadharani.Je adui wetu ni nani na yupo wapi na kwa nini tusimtafute???

Mi sijali wewe msomaji unanifikiriaje,kama utanitukana we tukana tena vizuri tu,kama utanicheka we cheka,kama utanitisha we nitishe manake hautanifanya chochote...ila kabla hujapanua mdomo wako nataka uelewe kitu kimoja muhimu sana kuwa nchi yetu haina mbele wala nyuma GDP ya Taifa ni dola za kimarekani 599 kwa kifupi naweza kusema ni moja kati ya nchi masikini sana duniani

Je tatizo liko wapi???
Tatizo lipo kwa serikali?na kama ni Serikali tatizo HILI tunahiitaji?Kwa nini tusiipindue??
Au tatizo ni elimu yetu ambayo inalenga kumfaidisha mzungu na kumdidimiza Mtanzania?Kama tatizo ni elimu kwa nini tusibadili mfumo mzima?
Au tatizo ni wabunge tuliowachagua ambao hakuna hata mmoja anajaLI wapiga kura wake?Kama tatizo ni hao kwa nini tusifukuzie mbali manake kama ninavyojua mbunge ni kama mfanyakazi wa ndani wa watanzania sasa kama tunaruhusu mfanyakazi wa ndani kuwa na sauti kuliko mwenye nyumba basi kuna tatizo?Je kuna umuhimu wa kushikilia tatizo?fukuzia mbali kama mbunge ni tatizo
Au tatizo ni sisi wenyewe waTanzania???Na kama tatizo ni sisi wenyewe tunasubiri nini kujipindua wenyewe?Manake hata kama tutapindua serikali kama tatizo ni sisi basi tutapindua serikali zote na mwisho tatizo lipo palepale lakini kama tatizo ni sisi basi tujipindue fikra zetu na hayo ndo mapinduzi makubwa kuliko yote...tusipojipindua wenyewe kifikra amini usiamini siku moja watoto wetu watakuwa watumwa kwenye ardhi yao wenyewe....watatembea wamefungwa minyororo ambayo kamwe hata wao wenyewe hawatajua na hawataweza kuiguza manake haionekani kwa macho...tutalia na kusaga meno manake siku zaja ambazo watoto wetu watachinjana wao kwa wao kwa kutojua nini wanavanya kwa nini???kwa sababu tunajenga ukuta bila msingi.AMKA AMKA Mtanzania unakula bata ..kula na kusaza wakati dunia nzima ipo vitani?

Umri wa Mtanzania wa kuishi kwa sasa ni miaka 50..mbona hakuna anayehoji kwa nini?Jibu rahisi sana ugumu wa maisha unaamka asubuhi mtoto wa miaka mitatu uso umemkakamaa kama ana miaka 10 ukihoji kwa nini unaambiwa anawaza jinsi ya kukipata kitumbua wakati lilikuwa ni jukumu la mzazi.

Kazi maofisi zinaanza saa tatu mchana wakati Mtanzania wa kawaida ameamka saa tisa usiku ili kuwahi foleni kapanda kwenye daladala anatumia masaa matano hadi sita na hapo hapo anachelewa kazi..Je tunapoteza masaa mangapi njiani kwa ajili ya foleni?Je unategemea huyo Mtanzania achangie vilivyo pato la Taifa???Kwa nini hatuhoji ??
Au tatizo lipo kwenye ukusanyaji wa kodi ni mbovu?Tuachane na ndoto sijui za umoja wa Afrika mashariki ya kazi gani ifikie kipindi tuangalie interest zetu kama watanzania ..hao sijui wakenya nawengine wao hawatuhusu...AMKA AMKA

Nawakilisha kama unamajibu hebu tusaidiane
 
Back
Top Bottom