Wazo - Mgahawa wa Vyakula Asilia

Fighter23

Member
Joined
Sep 22, 2019
Posts
41
Reaction score
131
Kwa wale wenye mitazamo na ndoto za kufanya biashara ya kuuza vyakula hasa waliopo kwenye miji ya mikubwa ya kibiashara, unaweza pitia wazo hili pengine linaweza kukufaa.

Ni kwamba kwenye miji mikubwa yenye watu wengi, Ni sehemu chache sana ambapo kuna migahawa ambayo mtu anaweza kupata vyakula asilia kama alivyozoea kula kijijini kwao. Kuna watu hutumia muda mrefu kuishi na kukaa kwenye miji hii bila kurudi makwao kutokana na shughuli wanazozofanya hivyo kwa namna moja au nyingine huwa wanakosa sehemu nzuri na nadhifu pa kuweza kupata vyakula vya asili yao vilivyopikwa kama vile wanavyokula wakiwa kwao.

Unaweza kutumia fursa hii kufungua Mgahawa hasa sehemu yenye Garden ukawa na walau nafasi ya kukaa meza 10 au zaidi Kisha ukawa unauza vyakula vyenye asili ya makabila yaliyopo nchini kwetu Tanzania na nchi za jirani. Nakuhakikishia watu wengi wanatamani sana kitu hiki na sehemu nyingi hakuna migahawa wanauza vyakula hivi.

Nawasilisha wazo.
 
Wazo zuri..nishawahi kuwaza kitu kama hiki..unapeak traditional dishes za kila kabila(Popular)
 
Mji wenyewe mkubwa unamaanisha Dar es Salaam?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…