Wazo: Serekali yetu ya mkoa wa Dar, Posta mbele ya NBC bank panafaa kwa utalii wa kula pweza

Crocodiletooth

JF-Expert Member
Joined
Oct 28, 2012
Posts
20,561
Reaction score
24,428
Asalaam aleykum,

Hapo Posta panagadeni nzuri mno mno ambayo ikipangiliwa vizuri inaweza kugeuka sehemu nzuri ya kustaftahi, kula ngisi, urojo juice, soda na katu pombe zisiwepo kamwe!....
Itapendeza mno hasa baada ya ubunifu mahususi kufanyika.
 
Kulikuwa na bustani ufukweni ikiwa imepambwa na nyasi za ukoka, maua na viti vya kupumzikia. Kulikuwa na "Promenade" ya nguvu kuanzia ile Terminus ya kwenda Zanzibar hadi maeneo ya mahakama ya kivukoni. Hadi kufika miaka ya 1980 eneo lile pamoja na bustani ya pale posta ilikuwa sehemu nzuri za kubarizi enzi hizo.
Kuanzia miaka ya 1985 kuendelea, mambo yalianza kubadilika huku wauza mihogo ya kuchoma, machungwa na wauza kahawa wakijimilikisha maeneo yaliyoanza kujaa uchafu hadi siku ya leo.
 
Mkuu upo sahihi kwa 100%,hapo kitambo kidogo tulikwenda kustaftahi pale kila jioni, na palikiwa na viti vya zege, lile bomba la maji taka lilikuwa limerefuka kidogo lakini palivyokuja kuharibika nashindwa kuelewa, na akili za kibunifu kwa hawa viongozi wa sasa ni shida kidogo!
-Rais wetu anapenda mambo mazuri mazuri ya kibunifu yenye kusaidia kukuza uchumi wa taifa na mtu mmoja mmoja!
Hasa utalii, pia watalii wanaofikia kwenye mahoteli jirani watapata sehemu za kupumua na kustaftahi kabla ya kurudi vyumbani.
 
Haswaa, wanapaswa mamlaka za jiji la Dar kuiga ile ya Zanzibar (Forodhani) na Tanga (karibu na Maktaba kabla ya kuelekea deep sea). Ni maeneo yenye kufanana sana.
 
Lakini wakajenga kwa ubunifu wa kipekee na unique!
 
Back
Top Bottom