Crocodiletooth
JF-Expert Member
- Oct 28, 2012
- 20,561
- 24,428
Nipo kitalii zaidi kwa kasi ya rais wetu, yakhee!Wazo zuri sana, una kitu utafika mbali..!
Mkuu upo sahihi kwa 100%,hapo kitambo kidogo tulikwenda kustaftahi pale kila jioni, na palikiwa na viti vya zege, lile bomba la maji taka lilikuwa limerefuka kidogo lakini palivyokuja kuharibika nashindwa kuelewa, na akili za kibunifu kwa hawa viongozi wa sasa ni shida kidogo!Kulikuwa na bustani ufukweni ikiwa imepambwa na nyasi za ukoka, maua na viti vya kupumzikia. Kulikuwa na "Promenade" ya nguvu kuanzia ile Terminus ya kwenda Zanzibar hadi maeneo ya mahakama ya kivukoni. Hadi kufika miaka ya 1980 eneo lile pamoja na bustani ya pale posta ilikuwa sehemu nzuri za kubarizi enzi hizo.
Kuanzia miaka ya 1985 kuendelea, mambo yalianza kubadilika huku wauza mihogo ya kuchoma, machungwa na wauza kahawa wakijimilikisha maeneo yaliyoanza kujaa uchafu hadi siku ya leo.
Lakini wakajenga kwa ubunifu wa kipekee na unique!Haswaa, wanapaswa mamlaka za jiji la Dar kuiga ile ya Zanzibar (Forodhani) na Tanga (karibu na Maktaba kabla ya kuelekea deep sea). Ni maeneo yenye kufanana sana.