Wazo: Tanzania iwe shirikisho la nchi nne. Tanzania kusini, Tanzania Kaskazini, Tanzania Magharibi na Tanzania Mashariki

Una mawazo ya kijinga sana. Kuwa na mfumo wa majimbo haina maana kila jimbo lita miliki peke yake rasilimali zilizo katika eneo lake. Mfumo huu unatumika ktk mataifa meni mfano Kenya, Nigeria, SA, Brazil, Japan, US, Germany etc.
 
Kuna kanda hazito faidika na rasilimali za taifa kabisa, na mwisho tutatengeneza umasikini kwenye kanda zisizo na rasilimali za asili na huo ndio utakua mwanzo wa vita baina ya kanda na kanda

..hebu tupe mfano wa kanda ambazo unadhani zitaingia vitani na tueleze zitakuwa zinagombea nini.

..mbona sasa hivi kuna mikoa lakini hakujatokea vita kati ya mkoa mmoja dhidi ya mwingine?
 
Kwaiyo na wewe ukoo wako ukiugawa ndio maendeleo yatakuja haraka?

Sasahivi ni muda wa kuwaza kuiunganisha Afrika iwe nchi moja, na sio kuvunja nchi zetu

..basi tuondoe mikoa na hata wilaya ili tusiigawe nchi.
 
Suluhisho ni kuunda Serikali za Majimbo
 
..basi tuondoe mikoa na hata wilaya ili tusiigawe nchi.
Mikoa yetu na wilaya zetu zina marais wake, zina sarafu zake, zina bendera zake, zina mabalozi wake wanazoziwakilisha nje.

Ungesema tugawe kwenye majimbo ingekuwa na mashiko zaidi.
 
Kuna baadhi ya kanda hapo zitakufa njaa.
 
Hapo tutakwama tu, asilimia kubwaya mapato inapatikana Dar es Salaam pekee kuanzia viwanda, mitaji mpaka shughuli za nje hivyo kuna baadhiya kanda zitafanikiwa zaidi kuliko nyingine

Bado tuna kila sababu ya kuendelea hivi ila ni muhimu tukisambaza maendeleo na sehemu nyingine pia
 
Tupeni kanda yetu ya maghalibi Tabora,kigoma, simiyu, shinyanga, Mwanza, Mara, Geita na Kagera. Tutajuana wenyewe .
 
Halafu wale wa kuvuka kwa mashua watakuwa kwenye ipi
 
Halafu wale wa kuvuka kwa mashua watakuwa kwenye ipi
Lindi, Mtwara, Njombe, Iringa, Mbeya, Ruvuma, Morogoro.
Dar es salaam, Pwani, Tanga .
Mara, Bukoba, Mwanza, Simiyu, Shinyanga, Geita.
Dodoma, Singida, Kigoma, Tabora.
Mikoa mingine iingize humo ndani ya Mikoa hiyo
 
Jambo ni moja tuu, Zanzibar kuwa mkoa wa Tanzania, iwe kwa vita au amani.
 
Kuna kanda hazito faidika na rasilimali za taifa kabisa, na mwisho tutatengeneza umasikini kwenye kanda zisizo na rasilimali za asili na huo ndio utakua mwanzo wa vita baina ya kanda na kanda
Zitabuni njia nyingine akili itakuja wakati wa matatizo akili uja
 
Mikoa yetu na wilaya zetu zina marais wake, zina sarafu zake, zina bendera zake, zina mabalozi wake wanazoziwakilisha nje.

Ungesema tugawe kwenye majimbo ingekuwa na mashiko zaidi.

..mimi sijasema mikoa au wilaya iwe na Maraisi, sarafu, etc.

..hata majimbo hayatakuwa na mambo hayo, ambayo kwa kawaida na yanawekwa ktk serikali kuu.
 
Nchi saba
Tanganyika
Tanzania Unguja
Tanzania Pemba
 
Kwahiyo CCM wamejimegea kanda ya kati! Mbona umeificha!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…