Wazo; TRA marathon,jukwaa rafiki la kuwakutanisha tra na walipa kodi!!!

Wazo; TRA marathon,jukwaa rafiki la kuwakutanisha tra na walipa kodi!!!

pumbuka

Member
Joined
Dec 15, 2025
Posts
9
Reaction score
14
Someni wazo mtoe maoni yenu!!

Maendeleo ya taifa lolote hujengwa juu ya mshikamano na ushirikiano kati ya Serikali na wananchi wake. Ushirikiano huu hujidhihirisha kupitia ushiriki wa wananchi katika kulinda amani, kushiriki katika shughuli za maendeleo, pamoja na kutekeleza wajibu wao wa kikatiba wa kulipa kodi.

Kodi ni nyenzo muhimu na ya msingi inayoiwezesha Serikali kutekeleza majukumu yake kwa wananchi. Ujenzi wa barabara, reli, hospitali, shule, miradi ya nishati na maji, pamoja na utoaji wa huduma nyingine za kijamii, kwa kiasi kikubwa hutegemea ulipaji wa kodi wa wananchi.

Pamoja na mafanikio yaliyopatikana katika ukusanyaji wa mapato, ulipaji wa kodi kwa hiari bado ni changamoto. Baadhi ya walipa kodi bado hulipa kodi kwa shuruti na kwa hofu ya adhabu, badala ya kulipa kwa uelewa, uwajibikaji na hiari.
 

Attachments

Back
Top Bottom