WAZO: Wamiliki wa mabasi fungeni kamera ulinzi (CCTV Camera) japo kwenye lango la kuingilia abiria

WAZO: Wamiliki wa mabasi fungeni kamera ulinzi (CCTV Camera) japo kwenye lango la kuingilia abiria

Chivundu

Platinum Member
Joined
Dec 17, 2012
Posts
7,781
Reaction score
6,966
Kwa hali ilivyo sasa madereva kupigwa mpaka kuuwawa, abiria kushushwa kwenye mabasi kimafia na kuuwawa na matukio mengine mengi ya kiharifu, ni bora wamiliki wa mabasi mkafunga Camera hizi kwenye mabasi.

Kama mnafunga ving'amuzi inashindikanaje kufunga Camera japo kwenye lango la kuingilia abiria na upande wa dereva?

Pia, nashangaa Mchina na Scania, wanatengeneza mabasi ya anasa "luxury" wanauza bei ghali wanashindwa kweli kuyawekea mifumo ya ulinzi "cabin surveillance cameras and alerts". Mbona mabasi nchi zingine yana hii mifumo?

Wamiliki fungeni hata CCTV camera za bei rahisi, mbele nyuma na kwenye lango la kuingilia, sitasaidia kuokoa mali na abiria na kukamata waharifu.

Hali inatisha.
 
Mabasi yote ya kisasa yana camera sema hazitumiki na ni cctv kabisa unaweza hata kuzi monito ukiwa mbali
 
Kwanini hawazitumii mkuu?
Uswahili na kutofatilia wao wanafatikia hesabu tuu lakini mbasi yote ya kisasa kitoka china yana camera zaidi ya tatu ndani

Mbele kulia inamulika eneo la mlango na mbele juu kumulika upande wa bus zima na dereva chini ya staff carrier na nyuma mwisho ipo camera
 
Mkuu kweye mabasi tu haitoshi.

Zingatia hili ni moja tu lililotokea hivi kwenye basi.

Miji mingi Ina CCTV mabarabarani na sehemu zote nyeti.

Hata Nairobi, Kigali, Kampala ni mfano wake kulikoni sisi?
 
Mimi nataka tuanze kampeni hii, mabango yote ya Samia yatoke, ziwekwe CCTV. Tunakuwa na kiongozi anajijali yeye kuchafua mji kwa mabango ya sura yake, ya kila aina. Wakati hizo fedha za mabango zingetosha kufungwa CCTV kila kona ya huu mji wenye purukushani.
 
Back
Top Bottom