Wazoefu wa biashara ya boda boda na bajaji, njoo mtujuze changamoto mnazokumbana nazo

Wazoefu wa biashara ya boda boda na bajaji, njoo mtujuze changamoto mnazokumbana nazo

Erick Richard R-Madrid

JF-Expert Member
Joined
Oct 3, 2014
Posts
399
Reaction score
282
Salamu wana Jukwaa....

Nimepata wazo la kuanzisha biashara ya Boda boda na Bajaji kuanzia mwezii wa 11 jijini Dar es salaam, naanza biashara hii baada ya kujibana kwa kipindi cha miaka 3 sasa.

Nimewekeza kiasi cha Milioni 10, nitaanza kwa Bajaji 1 na Boda boda 1. Nipata wazo hili huku nikiamini suala la usafiri kwa jiji la Dar es salaam bado ni Changamoto kwa ujumla.

Nimeshaanza mchakato wa kutafuta vijana wawili kutoka mtaa ninao toka, Changamoto nilizonazo kwa sasa ambazo ningependa mawazo wakuu na utatuzi ni:

1. Kwa wale wazoefu ni changamoto/ hasara gani mnakumbana nazo?

2. Mfano wa mkataba kuweza kuwapatia wafanyakazi kabla ya kuanza kazi.

3. Makusanyo ya hela yafaa kwa muda gani hasa (wiki au siku)?

4. Mbinu za kumbana dereva aweze kuleta hela kwa wakati unaotakiwa.

5. Pikipiki (boda boda) & Bajaji za kampuni gani ndo bora zaidi?

Asanteni Wakuu...
 
Hio biashara siku hizi ni stress tupu, labda uendeshe mwenyewe boda au bajaj. Kama hutaweza basi tafuta mtu anayeweza kufanya kazi kwa mkataba wa miezi kadhaa akimaliza marejesho yake basi boda inakuwa yake.

Hio formula itakupunguzia maumivu ya kichwa sababu mkataba wa hivyo hutasikia matatizo ya hapa na pale.. wewe ni kukinga pesa yako kila mwisho wa wiki
 
Mimi pikipiki miezi 11 mkataba tunasaini kwa mwanasheria kila mtu copy yake, mwisho nakupa kadi ubadili umiliki.

Mfano nakununulia Kinglion 150 kama 2 mln, bima 59,000,Sumatra 22,000 then mimi kila wiki unaleta 70,000 tu, service juu yako na kama ukikamatwa kwa makosa ya uzembe wako.

Miezi 11 ni shs 3,300,000 faida yangu kama milioni moja kwa hiyo miezi 10.
 
So ina maana kwa mwezi faida yako ni LAKI 1????
Mwezi mzima?
 
Mimi mwaka 2013 hadi 2014 mwishoni, nilikua na boda boda 5, mwanzoni tulienda vzr sana, boda 3 zilikua mkataba ndani ya miez 10, kila siku elfu 10 na baada ya hapo ni yake. Niliamini na kutegemea baada ya hapo ntazungusha pesa ktk kitu chengine, kumbe niliingiza pesa ktk tanuri la moto.....nilichojifunza ktk biashara za vyombo vya moto usimuamini mtu hata kama ndugu yako, kubwa fanya mwenywe utaona faida yake.....

April 2015 sarakasi zilikua nyingi, hatimae nikajikuta nahudhuria polisi na mahakamani kwa kuwashitaki madereva wangu wakiwa wao ndio wanachora michoro ya pikipiki kuibiwa.....Mungu saidia, polis mmoja ambae alikua mpelezi wng akanifungua kuwa pesa nilizoweka kwa biashara ya pikipiki nizitoe, mana kwa muda huo nilikua nimeweka 12 mil na tayari pkpk 2 zimeporwa kwa njama. ......mambo ni mengi, ila kama mtoa mada unataka mafanikio ktk biashara ya vyombo vya moto fanya mwenywe.
 
Biashara ya boda boda ni nzuri sehemu yenye mishe mishe nyingi,

Nilinunua Tvs kwa 2,050,000 nikamkabdhi mtu per day aniletee 10000,
Tulienda vizuri miez miwili,baadae akalishwa maneno,
Nikachkua chombo changu,nikaendesha mwenyewe,nikawa daily skosi 25' kwa wastani hapo nimekula kijiweni mchana,

Baada ya muda wa miez 9 hela yangu ilirudi na faida Juu,

Niliwaza niongeze nyingine but,uaminifu ndo shida nikachkua faida na Mapato nikafukia ardhini(kununua kiwanja)
Nikauza ile tvs,sasaivi nipo kwene biashra nyingine tu,

Shida kubwa Ipo kwenye kuexpand hiyo business,
Na matatizo kama kifua,kukabwa na kuporwa,
Hivo.
 
Biashara ya boda boda ni nzuri Sana, ila inachangamoto zake km zilivyo biashara zingine tu. Chamoto kubwa kabisa ni uaminifu kwa hao vijana wanao tufanyia kazi. Ili kukabiliana na changamoto hizo yafuatayo uyazingatie.

1. Anza pikipiki mpya but zile za Bei nafuu
2. Fanya utafiti wa tabia za hao vijana unaotaka kuwapatia.
3. Zingatia umri wa hao vijana above 18 age na ikwezekana awe ameoa.
3. Malipo yawe kwa kila wiki
4. Fanya kwa mkataba(miezi 11)
5. Kila siku akuletee 10000 chukua malipo kwa wiki
6. Funga GPS kwenye hizo boda hiyo itakurahisishia kuzifuatilia popote utakapokuwepo.
7. Hakikisha pikipiki umeikatia vibali vyote mhimu km vile bima, Sumatra n.k
8. Hakikisha kijana unaemkabidhi hicho chombo lazima awe na leseni ya drive. pia km anafamilia yake karibu ni vyema kuishirikisha familia yake na ikiwezekana wamzamini.

Nafikiri kwa kuanzia hayo yanatosha mengine, utapa izoefu huko mbele ya Safari
 
Mkuu mimi nafanya kazi ya Bajaj toka nimalize chuo kikuu mwaka 2016, mpaka sasa mafanikio ni makubwa sana. Kama ilivo kawaida changamoto ni nyingi mno lakini jitahidi uzikabili wala usikate tamaa! Bajaj nunua TVS King+ ni nzuri sana...zingatia Service kila week, mwaga oil kama ilivoelekezwa! hiyo ni ajira ya kudumu na wala hutatamani tena zile zingine kutoka Tamisemi. Mwisho kabisa itakuwa vyema ukiendesha mwenyewe na sio kumpa mtu mana wataila kabla hata haijarudisha pesa
Asante sana ndugu kwa ushauri, nitazingalia uliyoniambia[emoji120]
 
Mimi mwaka 2013 hadi 2014 mwishoni, nilikua na boda boda 5, mwanzoni tulienda vzr sana, boda 3 zilikua mkataba ndani ya miez 10, kila siku elfu 10 na baada ya hapo ni yake. Niliamini na kutegemea baada ya hapo ntazungusha pesa ktk kitu chengine, kumbe niliingiza pesa ktk tanuri la moto.....nilichojifunza ktk biashara za vyombo vya moto usimuamini mtu hata kama ndugu yako, kubwa fanya mwenywe utaona faida yake.....april 2015 sarakasi zilikua nyingi, hatimae nikajikuta nahudhuria polisi na mahakamani kwa kuwashitaki madereva wangu wakiwa wao ndio wanachora michoro ya pikipiki kuibiwa.....Mungu saidia, polis mmoja ambae alikua mpelezi wng akanifungua kuwa pesa nilizoweka kwa biashara ya pikipiki nizitoe, mana kwa muda huo nilikua nimeweka 12 mil na tayari pkpk 2 zimeporwa kwa njama. ......mambo ni mengi, ila kama mtoa mada unataka mafanikio ktk biashara ya vyombo vya moto fanya mwenywe.
Asante ndugu kwa ushauri
 
Biashara ya boda boda ni nzuri sehemu yenye mishe mishe nyingi,

Nilinunua Tvs kwa 2,050,000 nikamkabdhi mtu per day aniletee 10000,
Tulienda vizuri miez miwili,baadae akalishwa maneno,
Nikachkua chombo changu,nikaendesha mwenyewe,nikawa daily skosi 25' kwa wastani hapo nimekula kijiweni mchana,

Baada ya muda wa miez 9 hela yangu ilirudi na faida Juu,

Niliwaza niongeze nyingine but,uaminifu ndo shida nikachkua faida na Mapato nikafukia ardhini(kununua kiwanja)
Nikauza ile tvs,sasaivi nipo kwene biashra nyingine tu,

Shida kubwa Ipo kwenye kuexpand hiyo business,
Na matatizo kama kifua,kukabwa na kuporwa,
Hivo.
Nadhani kuendesha mwenyewe kama ulivyoni shauri nitapata faida mara mbili zaidi ya nitakavyo mpatia dereva mwingine
 
Nimewasoma karibu wote,

Biashara ya boda boda ina stress zake, mke wangu alikuwa na bodaboda kadhaa,akawakabidhi vijana kwa mikataba kwenye serikali za mtaa, hesabu kwa siku 10000/- wanampa kwa wiki ndani ya miezi 13 boda inakuwa ya dereva, kila dereva alikuwa anapatana naye na anaenda mwenyewe kuchagua aina ya pikipiki anayotaka,boda boda mbili hazikurudisha pesa, moja ilianguka na dereva ikiwa mpya na ikawa na usumbufu akaiuza kwa hasara, nyingine ilikaangwa injini, nyingine alilazimika kubadili madereva mara 3,mwishowe aliiuza.

Lakini hakukoma kanunua tena yumo, safari hii anachukua pesa kila baada ya siku 3,Mkataba ni uleule wa miezi 13, Bado madreva ni wasumbufu balaa, ataleta hela ya siku 3 baada ya siku 5.Angalau kidogo ugomvi umepungua kwa kuwa wakati ule kila inapofika siku ya hesabu aidha wanafiwa,kukamatwa na Polisi au kuuguliwa, hesabu ndani ya siku tatu sababu zimepungua kidogo japo ugomvi haujaisha.
 
Dah! Ni shida balaa, changamoto za bodaboda ni nyingi sana
 
Nunua Noah nenda kusini huko kapige root Za Kilwa masoko to Lindi au Kilwa masoko to kilwa Pande miezi sita hela isharudi ila fanya mwenyewe
 
Back
Top Bottom