Umuhimu ni uaminifu kati yenu.malengo ni mengi na pia kuyafikia ni mipango ya mungu.Nlikuwa na galfnd wangu.tulimaliza chuo pamoja.mimi nkapata kazi songea,yeye kapata dar.2liendelea kuwasiliana,mipango mingi,lakini ilifika wakati kila mtu akapata company ya watu wengine huko alipo.Malengo yetu yalipotea.Natarajia kuoa mwakani.kaolewa mwaka jana.Ni kweli,kwenye swala la ajira ni tete hapo.Especially,ikitokea long distance.Ila kama mungu amepanga,no matter what,mtafanikisha.
ndo yule aliekuzidi umr?si ulisema mnapendana sana,sasa vp tena?
ukweli ni kwamba ni ngumu kidogo kutoka na mpenzi chuo paka huku duniani,mara nyingi kuna vikwazo vinatokea hapo katikati mkuu,imagine unapangia kazi kigoma demu anabaki dar, pamoja na hayo yote jipe moyo ka ni mpango wa Mungu ni possible mkuu!
Hali uliyonayo sidhani kama utavuka salama coz ushaanza kujiwekea mashaka kama utaweza kuachieve your dream na mpenzi wako, au kuna hoja umeificha kuhusu misingi ya mapenzi yenu? Kuna uwezekano umetoa ahadi nyingi kipindi cha mahusiano yenu au umejiuza kwa sifa zisizo zako.
Yote uliyosema yanawezekana, kama mna mipango ya kuja kuishi nyote maishani cha msingi ni kusimamia ahadi yenu na kukumbushana wapi mmetoka na nini malengo yenu, kufanikiwa kimaisha baada ya kumaliza chuo ni mipango ya mwenyezi mungu yeye ndo mpangaji wa riziki za wanadamu, usilazimishe.
Nilipita kwenye dillema kama yako, nilijiingiza kwenye mapenzi na mtu ambaye leo ni mke wangu nyakati za elimu ya sekondari, nikamaliza chuo udsm 2007 tupo together, nikapita msoto wa more than a one year bila kazi nipo nae by that time yeye ndo alikuwa chuo so ata hela ya misele ya town kuhustle alikuwa akinipa yeye but suddenly nkapata the best job with the best pay, two years nkaachieve kila kitu cha maisha ya kisasa na kwa kijan wa kileo anachostahili kuwa nacho, 2010 tukafunga ndoa takatifu st Joseph, leo ni ndoa yenye loved baby boy.
My take: aidha badili stori au ahadi hewa ulizoingia nazo kwa binti wa watu, onesha rangi yako halisi ili binti ajue anamove na mtu wa kariba ipi then wekeni malengo na muwe mnakumbushana, mwisho mungu atawasaidia kufikia ndoto yenu.
We sema usha pata mchuchu mwingine acha kuzingua...
Ulikuwa unamuhonga boom kwa sana?
Asikwambie mtu kaka piga mimba kwanza halafu mambo mengine yatanyooka yenyewe.Usipofanya hivyo utajuta maisha yako yote.
salam tele kwa mwenye mada hii! kwa uhakika nimeisoma mada yako na kuelewa ushauri unaumba. nami katika udogo wangu na jambo la kukuchangia kimawazo.
katika maisha, wengi huwa tumafanya kosa moja! nalo ni kuchanganya kati ya kufuata ushauri wa watu uwe mzuri au mbaya na kufanya maamuzi yetu wenyewe. kwa sababu hii watu waliowengi huwa wanaomba ushauri na kuufuata bila kuchambua kwa makini eti tuu kwa sababu fulani alifanya na akafanikiwa! nimesoma ushauri wa watu wengi kwenye thread hii na nikaona iwepo haja ya kukutahadharisha kwa hili.
ili mmoja afanye maamuzi sahihi katika kila jambo yampasa kwanza aangalie lengo la kile akifanyacho, mazingira na muda. na kwa mantiki hii hata akili ya kawaida ya mtu hupimwa! wengi wamesema mengi tayari kwenye thread yako na kwa kutumia uzoefu wao. je! wewe mwenyewe umeingia ndani ya moyo wako na kutafakari kwa kina kuhusiana na jambo unalotaka kulifanya, hasara na faida zake? kama hilo umefanya ukagundua faida ni kubwa kuliko hasara, hakuna shida waweza songa mbele wewe na huyo mwenzi wako!
ilifaa pia wewe na huyo mwenzi wako mliangalie hili kwa kina, kama kweli mnadhani inawezekana wote kwa pamoja, bila kuvutiwa zaidi na hisia zenu za mapenzi. wakati fulani mapenzi yanaweza kuwanogea mpaka mkadhani kila kitu kinawezekana! kumbe suala la kuishi wawili lataka heshima kuu na bidii isiyokoma.
kuna mahali nimeandika angalia wingi wa faida na hasara kisha uamue, ndio, nimeandka hivyo makusudi kwa kuwa hakuna maamuzi yoyote yaliyo chanya tuu chini ya jua! hasi haiepukiki kwa kila jambo!
mwisho nasema "ningelikuwa wewe", ningejipa mda kwanza wa kuishi na kuyatathmini maisha bila kuwa na mtu yeyote wa aina hiyo, maana katika utulivu mkuu watu huweza kufanya maamuzi sahii, miezi sita au mwaka mzima ungenisaidia kuliko kufanya maamuzi bila upembuzi yakinifu bila practical, ndio maan walatini wanasema, "experiensa docet" so go and get a pure lived experience and then enter into the real decisions without being biased by any sort of illusions! mind u kwamba, wanafunzi wengi huwa na alot of illusions 'ideas' wanapokuwa chuoni wakifikiri kuwa maisha ni kama wanavyofikiri na ni rahisi kama wanapokuwa wanafunzi kumbe ndivyo sivyo!
sor kama ntakuwa nimekuboa mzee, huo ni ushauri tuu mzee!