salam tele kwa mwenye mada hii! kwa uhakika nimeisoma mada yako na kuelewa ushauri unaumba. nami katika udogo wangu na jambo la kukuchangia kimawazo.
katika maisha, wengi huwa tumafanya kosa moja! nalo ni kuchanganya kati ya kufuata ushauri wa watu uwe mzuri au mbaya na kufanya maamuzi yetu wenyewe. kwa sababu hii watu waliowengi huwa wanaomba ushauri na kuufuata bila kuchambua kwa makini eti tuu kwa sababu fulani alifanya na akafanikiwa! nimesoma ushauri wa watu wengi kwenye thread hii na nikaona iwepo haja ya kukutahadharisha kwa hili.
ili mmoja afanye maamuzi sahihi katika kila jambo yampasa kwanza aangalie lengo la kile akifanyacho, mazingira na muda. na kwa mantiki hii hata akili ya kawaida ya mtu hupimwa! wengi wamesema mengi tayari kwenye thread yako na kwa kutumia uzoefu wao. je! wewe mwenyewe umeingia ndani ya moyo wako na kutafakari kwa kina kuhusiana na jambo unalotaka kulifanya, hasara na faida zake? kama hilo umefanya ukagundua faida ni kubwa kuliko hasara, hakuna shida waweza songa mbele wewe na huyo mwenzi wako!
ilifaa pia wewe na huyo mwenzi wako mliangalie hili kwa kina, kama kweli mnadhani inawezekana wote kwa pamoja, bila kuvutiwa zaidi na hisia zenu za mapenzi. wakati fulani mapenzi yanaweza kuwanogea mpaka mkadhani kila kitu kinawezekana! kumbe suala la kuishi wawili lataka heshima kuu na bidii isiyokoma.
kuna mahali nimeandika angalia wingi wa faida na hasara kisha uamue, ndio, nimeandka hivyo makusudi kwa kuwa hakuna maamuzi yoyote yaliyo chanya tuu chini ya jua! hasi haiepukiki kwa kila jambo!
mwisho nasema "ningelikuwa wewe", ningejipa mda kwanza wa kuishi na kuyatathmini maisha bila kuwa na mtu yeyote wa aina hiyo, maana katika utulivu mkuu watu huweza kufanya maamuzi sahii, miezi sita au mwaka mzima ungenisaidia kuliko kufanya maamuzi bila upembuzi yakinifu bila practical, ndio maan walatini wanasema, "experiensa docet" so go and get a pure lived experience and then enter into the real decisions without being biased by any sort of illusions! mind u kwamba, wanafunzi wengi huwa na alot of illusions 'ideas' wanapokuwa chuoni wakifikiri kuwa maisha ni kama wanavyofikiri na ni rahisi kama wanapokuwa wanafunzi kumbe ndivyo sivyo!
sor kama ntakuwa nimekuboa mzee, huo ni ushauri tuu mzee!