wazoefu wa kukwea pipa

wazoefu wa kukwea pipa

@kongosho
Mitaa yetu ni rahisi sana kupotea kuliko ya baadhi ya miji ya wenzetu!
 
I learned everything the hard way, no ready made.

Kwani sijui mie mambo yenu, kitu kidogo mnakompliketiii.

We nenda hata hapo sweat Easy au Osaka Masaki, unaagiza chakula, unaletewa makabrasha ya kujisomea.
Menyu yenyewe Chickeni breast, nimekua nikifuga kuku kijijini sijawahi ona matiti ya kuku.

Niliwatukana mgahawa mzima nikasepa zangu, nikaenda gonga chips kuku kwa Edo.
Pesa yangu mwenyewe inipasue kichwa lol.
hahahah...lol,
Umenivunja mbavu! But hicho ndicho chakula changu mbona...
 
Haya, mie nimemtahadharisha lakini.

Namtakia safari njema!

Ndugu msafiri, huhitaji mpagazi?😛eace:

@kongosho
Mitaa yetu ni rahisi sana kupotea kuliko ya baadhi ya miji ya wenzetu!
 
Umeona sasa, simdanganyi msafiri.
Atanikumbuka, lazima aplan kila kitu vizuri ahead of the game.

Vinginevyo, ndo mkasa wa kuagiza pemba(udongo unaopendwa na akina mama) na pilipili.

hahahah...lol,
Umenivunja mbavu! But hicho ndicho chakula changu mbona...
 
Niandalie kumbi kumbi, ntakuja na pepsi mbili.
Karibu sana,
Preta atakuandalia kitu cha nyara ya taifa........Mishkaki ya mdudu pori!~! hasa hiyo mizigo yake hapo nyuma!

1.jpg
 
Ha ha ha ha, dah nikila huo mzigo
Lazima nitavumbua kitu
Maana unaonekana 'juicy' sana.

Nitavumbua hata baskeli ya kuendeshwa na maji.
Tena nataka ya kuoka.

Karibu sana,
Preta atakuandalia kitu cha nyara ya taifa........Mishkaki ya mdudu pori!~! hasa hiyo mizigo yake hapo nyuma!

1.jpg
 
I learned everything the hard way, no ready made.

Kwani sijui mie mambo yenu, kitu kidogo mnakompliketiii.

We nenda hata hapo sweat Easy au Osaka Masaki, unaagiza chakula, unaletewa makabrasha ya kujisomea.
Menyu yenyewe Chickeni breast, nimekua nikifuga kuku kijijini sijawahi ona matiti ya kuku.

Niliwatukana mgahawa mzima nikasepa zangu, nikaenda gonga chips kuku kwa Edo.
Pesa yangu mwenyewe inipasue kichwa lol.
Kongosho umepinda kama klorokwini.

Nimekuongeza kwenye list yangu ya watu naotaka kuonana nao haraka sana....Khaa!
 
Sijapinda babu ODM, wananichanganya sana hawa watu, tena kwa makusudi.
We jaribu tu utaona, kwanza ukifika wanaku-terrify kwa kukufunika na kitambaa shingoni ili baadae akunyonge.

Akikuhurumia anakiweka mapajani, unadhani ni coincidende kuwekwa mapajani? Kinapunguza nguvu.

Ukishaogopa, wanaanza kuleta makabrasha mjisomee, hivi kweli mie kuagiza soda au maji au bia hadi uniletee daftari?

Ugali samaki nao hadi niletewe madaftari?

Wizi mtupu.

Kongosho umepinda kama klorokwini.

Nimekuongeza kwenye list yangu ya watu naotaka kuonana nao haraka sana....Khaa!
 
Ulaya huwezi potea SHERIA FUATA ALAMA ukifika amsterdam utaambiwa wanaunganisha ndege wataelekea transfer desk kwenye boarding pass watakayokupa kuna namba ya GATE, FUATA MSHALE. On arrival fuata mshale kama unataka kupanda basi, train, tram, Metro vyote utaviona!
 
Sijapinda babu ODM, wananichanganya sana hawa watu, tena kwa makusudi.
We jaribu tu utaona, kwanza ukifika wanaku-terrify kwa kukufunika na kitambaa shingoni ili baadae akunyonge.

Akikuhurumia anakiweka mapajani, unadhani ni coincidende kuwekwa mapajani? Kinapunguza nguvu.

Ukishaogopa, wanaanza kuleta makabrasha mjisomee, hivi kweli mie kuagiza soda au maji au bia hadi uniletee daftari?

Ugali samaki nao hadi niletewe madaftari?

Wizi mtupu.
Vyote naweza kufikiria lakini bia nayo niletewe daftari? Manina!

Ngoja tuendelee kugida huku kwa kina Esther wa Fyatanga bar. Manake akiona ODM kaingia wala haulizi, huyoo anawahi kaunta analeta Tusker Malt baridiiii we kazi yako kugida tu. Ukilewa ukaondoka bila kulipa wala haahangaiki anajua kesho ukija utalipa. Kuku wake manati ya nini?
 
Niko hapa pembenifyatanga nasuburia Nyama ya mbuzi
 
mkuu sio uoga nataka kupata details kwa wazoefu ili nisije nikwama nikaingia hasara kwa kutoelewa vitu vidogo.
Kwani unataka kabisa kutoka nje utembee kidogo kwenye mataa mekundu au??, au shida ni kutokomea ukishafika Amsterdam? maana husomeki
 
usisahau kulizia
Red Light District in Amsterdam unafikaje?

Usitake ndugu yetu apotelee huko kwa makahaba wa Amsterdam maana akitoka huko watamwambia aende "coffee shop" akijua anaenda kununua kahawa kumbe ni kwa wauza madawa ya kulevya na mitaa hiyo ina wahuni wanaweza kumtoa ngeu wakimwona mweusi anazungukia mitaa yao.
 
wakuu naomba mnijulishe ni vitu gani vinahitajika mfano labda nafanya booking ya flight from Dar to Paris via amsterdam,au nataka kufika paris lakini lazima nipitie amsterdam,wale wazoefu naombeni msaada wenu.

Rafiki kama unaona kuita Amsterdam ni shida, kata tiketi ya Kenya Airways. Unatoka DAR hadi nairobi kisha unapanda ndege moja kwa moja hadi Paris, simple. Sasa ukiwa njiani popote usikubali mtu akuachie mzigo wake umwangalizie au akuombe umsaidie kuu-check inn kama yeye kazidisha kilo maana unaweza kuchomekewa madawa ya kulevya.
 
Niko hapa pembenifyatanga nasuburia Nyama ya mbuzi
Hayo majamaa yanachoma mbuzi sijapata ona. Yaani mbuzi wakikatiza maeneo hayo wanajikuta wanaachia ushuzi bila kupenda.
 
Kongosho sijaona cha maana alichomshauri muulizaji zaidi ya kumtia hofu tu ili aone ulaya ni sehemu ya ajabu sana, sijaipenda hiyo tabia, na kwa bahati mbaya wabongo wengi tuko hivyo.

Mkuu mimi nakushauri kwanza kabisa usipaniki kwa hiyo safari, chukulia kama ni ya kawaida sana. Usafiri wa ndege ni wa kawaida tu tofauti ni kuruka angani. Kwa kawaida kila shirika la ndege ukisafiri nalo mara nyingi ni lazima upitie kwenye uwanja wa nyumbani then wanaconnect ndege ingine to final destination, na mara nyingi hata ile company ya wasafiri ulotokanao mwanzo wa safari yako hubadilika kabisa na kupata wapya.

Mfano ukipanda Ethiopian lazima upite a.ababa, vilevile kenya airways lazima ipite nairobi, SA airlines lazima ipite joberg, egypty air lazima upite cairo, klm lazima upite amsterdam, turkish airlines lazima upite istanbul, Qatar vilevile..na bei zimetofautiana kwa the same destination.

Ukienda kukata tikiti ya ndege ya kwenda nje ya nchi lazima uende na passport, tena kuna mashirika mengine huhitaji na visa kabisa ili kuondoa usumbufu wa kudai marejesho ya pesa pale ukosapo visa.

Siku ya safari hakikisha unakuwa na documents zote muhimu kwa safari, passport na ticket zikiwa ni muhimu zaidi kwani hata visa hubandikwa kwenye passport. Fika airport saa moja au nusu saa kabla ya muda wa kukaguliwa kwa safari, baada ya kukaguliwa utaenda mule ndani kwenye meza ya airline unayosafiria, utakuta staffs na maandishi pia ya kukuelekeza kuwa hiyo meza ni ya klm au atc n.k.

Ukishawapa ticket na passport na mzigo kuweka kwenye mzani ili kupima mzigo, watakagua ticket na pass yako then watakupa vicard viwili vyenye kukuonyesha mzigo wako na seat number utakayokaa. Sasa inategemea, kuna wakati wanaweza kukupa moja utaconnect flight, watakwambie card au boarding pass nyingine utaipata ukifika amsterdam kwenye bench la klm hiyo ni kwa ajili ya ndege ya kutoka pale kwenda paris.

Ukiona unababaika ni bora uwe mwepesi kuuliza hata police mule ndani au information desks itakuwa ni salama sana kwako. Epuka kabisa kuzoeana na watu usiowajua au kuuliza mtu hovyohovyo. Kimbilio lako liwe ni police yeyote au staff yeyote wa klm.

Epuka kukubali mtu akuombe umshikie mzigo wake au wewe kumpa mtu akushikie. Epuka sanasana hii ngozi yetu nyeusi kwani wengi ndio huleta matatizo na kuvunja sheria. Epuka sana watu wa Africa magharibi, mara nyingi huwa ni weusi wa kwanza kukutana nao hata ukiwa Iraq japokuwa kuna baadhi yao ni watu wema sana trust me.

Mzigo wako ukishakabidhi airport ya dar utakuja kuupata paris hata kama utabadili ndege kumi, isipokuwa tu ule wa mkononi utakuwa nao mwenyewe. Kuhusu chakula kongosho asikutishe kwani mule ndani ya ndege huwa lazima kuwe na kiingereza. Ukiona wanakuchanganya we sema sema tu checken au sema beaf ataelewa hata kama anazungumza kiarabu.

Kumbuka mzigo uzito free kwa ndege nyingi siku hizi huwa ni kg 40. Ikizidisha hapo watakucharge zile extra dollar kadhaa kwa kilo.

Zaidi ya hapo sina bali nakutakia safari njema sana na maandalizi mema ya safari. Kama bado kuna jambo linakutatiza plse usisite kuuliza.
 
Back
Top Bottom