Kongosho sijaona cha maana alichomshauri muulizaji zaidi ya kumtia hofu tu ili aone ulaya ni sehemu ya ajabu sana, sijaipenda hiyo tabia, na kwa bahati mbaya wabongo wengi tuko hivyo.
Mkuu mimi nakushauri kwanza kabisa usipaniki kwa hiyo safari, chukulia kama ni ya kawaida sana. Usafiri wa ndege ni wa kawaida tu tofauti ni kuruka angani. Kwa kawaida kila shirika la ndege ukisafiri nalo mara nyingi ni lazima upitie kwenye uwanja wa nyumbani then wanaconnect ndege ingine to final destination, na mara nyingi hata ile company ya wasafiri ulotokanao mwanzo wa safari yako hubadilika kabisa na kupata wapya.
Mfano ukipanda Ethiopian lazima upite a.ababa, vilevile kenya airways lazima ipite nairobi, SA airlines lazima ipite joberg, egypty air lazima upite cairo, klm lazima upite amsterdam, turkish airlines lazima upite istanbul, Qatar vilevile..na bei zimetofautiana kwa the same destination.
Ukienda kukata tikiti ya ndege ya kwenda nje ya nchi lazima uende na passport, tena kuna mashirika mengine huhitaji na visa kabisa ili kuondoa usumbufu wa kudai marejesho ya pesa pale ukosapo visa.
Siku ya safari hakikisha unakuwa na documents zote muhimu kwa safari, passport na ticket zikiwa ni muhimu zaidi kwani hata visa hubandikwa kwenye passport. Fika airport saa moja au nusu saa kabla ya muda wa kukaguliwa kwa safari, baada ya kukaguliwa utaenda mule ndani kwenye meza ya airline unayosafiria, utakuta staffs na maandishi pia ya kukuelekeza kuwa hiyo meza ni ya klm au atc n.k.
Ukishawapa ticket na passport na mzigo kuweka kwenye mzani ili kupima mzigo, watakagua ticket na pass yako then watakupa vicard viwili vyenye kukuonyesha mzigo wako na seat number utakayokaa. Sasa inategemea, kuna wakati wanaweza kukupa moja utaconnect flight, watakwambie card au boarding pass nyingine utaipata ukifika amsterdam kwenye bench la klm hiyo ni kwa ajili ya ndege ya kutoka pale kwenda paris.
Ukiona unababaika ni bora uwe mwepesi kuuliza hata police mule ndani au information desks itakuwa ni salama sana kwako. Epuka kabisa kuzoeana na watu usiowajua au kuuliza mtu hovyohovyo. Kimbilio lako liwe ni police yeyote au staff yeyote wa klm.
Epuka kukubali mtu akuombe umshikie mzigo wake au wewe kumpa mtu akushikie. Epuka sanasana hii ngozi yetu nyeusi kwani wengi ndio huleta matatizo na kuvunja sheria. Epuka sana watu wa Africa magharibi, mara nyingi huwa ni weusi wa kwanza kukutana nao hata ukiwa Iraq japokuwa kuna baadhi yao ni watu wema sana trust me.
Mzigo wako ukishakabidhi airport ya dar utakuja kuupata paris hata kama utabadili ndege kumi, isipokuwa tu ule wa mkononi utakuwa nao mwenyewe. Kuhusu chakula kongosho asikutishe kwani mule ndani ya ndege huwa lazima kuwe na kiingereza. Ukiona wanakuchanganya we sema sema tu checken au sema beaf ataelewa hata kama anazungumza kiarabu.
Kumbuka mzigo uzito free kwa ndege nyingi siku hizi huwa ni kg 40. Ikizidisha hapo watakucharge zile extra dollar kadhaa kwa kilo.
Zaidi ya hapo sina bali nakutakia safari njema sana na maandalizi mema ya safari. Kama bado kuna jambo linakutatiza plse usisite kuuliza.