Wazoefu wa Open University (OUT) naomba ufafanuzi juu ya hili

Wazoefu wa Open University (OUT) naomba ufafanuzi juu ya hili

Mshua's

JF-Expert Member
Joined
May 22, 2013
Posts
804
Reaction score
553
Wakuu habari zenu!

Nilikuwa na ndoto siku nyingi ya kusomea nje ya nchi hasa nchi za wenzetu za ughaibuni. Nimehitimu masomo yangu katika Chuo Kikuu Huria almaarufu kama 'OUT', na sasa nataka nikachukulie masters huko ughaibuni almaarufu kama 'mamtoni'. Sasa swali langu kwa waliopitia mfumo wa elimu kama huu wa OUT, je scholarships kwa wahitimu wa OUT huwa zinapatikana kirahisi? Na je vyeti vya kuthibitisha kuwa uko-compitent kwenye English language vya IETL na TOEFL vinapatikana wapi? Nimeangalia vyuo vyote wanahitaji hivi vyeti. Nina Upper Second katika social science subjects.

Natanguliza heshima katika michango yenu!

Mshua
 
ili mradi una First Degree from any kind University iwe OUT au vyovyote unakua na sifa ya kupata scholarships kwa kutegemea vipaumbele vilivyoko ndani ya Taasisi husika.

kuhusu vyeti vya kuthibitisha u-Compentency wako ktk English Language kama uko DSM fika kwenye Office za BRITISH COUNCIL zilizoko City Centre.

Hongera kwa kupata Upper Second kwenye Digrii yako ya kwanza.
 
Mkuu nashukuru kwa ushauri wako na pongezi pia! Sasa Mkuu kama nikienda hapo British Council, ni particular gani zinahitajika kwenda nazo? Na je, ni malipo kiasi gani yanahitajika?
 
Why unataka mamtoni?

Kwa uzoefu wangu, wahitimu wa nje ya nchi wanapewa kipaumbele zaidi kuliko wahitimu wa ndani ya nchi aidha katika ajira serikalini, taasisi binafsi na hata za serikali, pia katika usajiri wa biashara kubwa kubwa wanafikiriwa kwanza. Vilevile, napenda kujifunza mbinu mbalimbali za kimaendeleo kutoka kwa wenzetu ili nije nizitumie katika kuiendeleza nchi yangu. Hata hivyo, kwa vyuo vya hapa nchini ni vigumu kupata ufadhili kwa masomo ya masters. Au unaweza kunifahamisha ni programme gani na chuo gani zina ufadhili kwa hapa nchini ili nichague kama zitakidhi mahitaji yangu.
 
Upper second ya open we ni kichwa shule ya pale ni ngumu sana, umejitahidi. Anyway unauliza sana maswali cha msingi umeshaambiwa nenda British Council utapewa maelezo yote. NB Open university ni chuo cha serikali ya jamhuri ya muungano ya Tanzania hivyo kina hadhi sawa na vyuo vingine na hakipo kibiashara kama ilivyo vyuo vingine hivyo taaluma yake ni ya kiwango cha kuridhisha sawa na ile apatikanao mhitimu wa NBAA
 
Nashukuru kwa ufafanuzi wako na pongezi pia! Maswali yanakuwa mengi sababu nahitaji kujua ili nikija Dar nije na vielelezo vyote vinavyohitajika kwani nisipovijua halfu kumbe ninavyo, itakula kwangu kwani nipo huku mikoani
 
si lazima uje Dar unaweza kujisajili mahali popote ulipo online ila utahitajika utume particulars within a week plus ada, kwa maelezo zaidi google British Council Tanzania tafuta link ya IELTS
labda kwa msaada tu ada ya mtihani ni 350000, vingine ambavyo ni optional.. materials 50000, mafunzo mafupi khs hiyo test 150000.. Ingia kwny website yao kwa maelezo ya ziada
 
Mkuu nashukuru kwa ushauri, nikitoka JF naingia British Council Tanzania kufanya uchunguzi zaidi.
 
Back
Top Bottom