Wazungu kila kona...!

Wazungu si waliwafukuza tena kwa mbwe mbwe tukasahau kuwa wao wameshika mpini sisi makali. Sasa ni miaka 49 bado tunawaomba omba. Tumelamba matapishi.
 
Ukoloni unarudi kwa nguvu, kasi na ari mpya. Sintoshangaa kama miaka ishirini ijayo itatubidi tuanzishe vita vya ukombozi kama enzi zileee!
 
Halafu viongozi wetu wanachekelea kama mazuzu.
 
Hivi kila mtu mweupe ni mzungu nauliza
 
na ajenda zao kwa bara la Afrika hazijabadilika tangu enzi za Mfalme Leopold wa Ubelgiji.
 
Na kibaya sana, wanarudi wale wale ambao wamerithi mikoba ya Carl Peters. Pamoja na usomi wote tulionao, hapo kwenye suala la wazungu tumezidiwa maarifa. Tumeuza yote bila ya bunduki wala uvamizi wa kijeshi.
 
MMhhh!

Hapo kwenye Mchuchuma negotiations; wazungu upande wetu ni nani washauri?.......nielewavyo ilikuwa ni watz na wachina
 
Ni kweli kabisa.

Acheni waje, sisi wengine ndio tukua na uhakika wa pombe ya kulewa. mfano sasa hivi tunalipa madeni, dowans na mengineo? Unategemea nchi inabakiza hela hii!!!!!! Acheni waje banaaaaaaaaaaa!
 
Viongozi wetu ndo wanatuzingua hawajui kuwaza ila kujipendekeza tu,kwani hao wazungu ndo wanajua kuwaza kuliko sisi?Watu hatuja pata xposure tuna wezafany maajabu.
 
hivi ni nini maana ya mzungu eti?

Ni kama vile ulikuwa kwenye mawazo yangu. Maana naona kila mtu mweupe anayeonekana kwenye hizo picha ameitwa mzungu. Mfano ukiangalia picha ya mwisho ina wachina ndani yake.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…