Wazungu nao wana wivu mwenzao akiwa tajiri

Wazungu nao wana wivu mwenzao akiwa tajiri

Machame Juu

JF-Expert Member
Joined
Jul 25, 2013
Posts
1,514
Reaction score
3,363
Likija suala la utajiri utachukiwa tu uwe mzungu ama mswahili kutakuwa na wivu na chuki. Tumeshuhudia Diamond alivyonunua Rolls-Royce.

Malaki ya watu wamesaini petion dhidi ya Jeff Beezos tajiri namba moja duniani wakinuombea kesho tarehe 20 akipaa anga za juu asirudi duniani tena abaki na apotelee daima hukohuko.

Jeff, kaka yake, mwanamke mzee miaka 80 na kijana miaka 18 kesho tarehe ishirini watapaa kwenda anga za juu kwenye chombo new shepherd ambapo watakaa dakika 15 na kurudi duniani.

Huyo kijana miaka 18 ni mtoto wa billionaire Muholanzi ambaye baba yake alilipa dollars za Kimarekani million 28 kupata seat na ilikuwa mnada. Baadaye akamuachia kijana wake.

Dogo darasani zinachaji sana kwenye physics na hisabati.

Ila wasirudi tu kwasababu kuna watu duniani mlo mmoja kwa siku ni shida
 
Sasa mkuu wasiporudi hao mlo mmoja kwa siku ndio utaongezeka?
 
Kwamba mchizi kachukua pesa za milo yao kaenda kula bata mwezini?
Mkuu huoni kuna walakini watu kuchezea na kuteketeza mabilion kwa mambo ya kipuzi wakati binadamu wenzao hata mlo mmoja kwa siku ni shida. Haileti mantik na uhiwuano kabisa.
 
Mkuu huoni kuna walakini watu kuchezea na kuteketeza mabilion kwa mambo ya kipuzi wakati binadamu wenzao hata mlo mmoja kwa siku ni shida. Haileti mantik na uhiwuano kabisa.
Mambo ya kipuuzi kwa mujibu wako ila kwake ni jambo zuri na la kupendeza.

Usimhukumu mtu kwa matumizi ya pesa alizotafuta mwenyewe bna, hata wewe kuna vitu unafanya ni kama unakua umepoteza pesa kijinga lakini ww vinakufurahisha.
 
Likija suala la utajiri utachukiwa tu uwe mzungu ama mswahili kutakuwa na wivu na chuki. Tumeshuhudia Diamond alivyonunua Rolls-Royce.

Malaki ya watu wamesaini petion dhidi ya Jeff Beezos tajiri namba moja duniani wakinuombea kesho tarehe 20 akipaa anga za juu asirudi duniani tena

Ila wasirudi tu kwasababu kuna watu duniani mlo mmoja kwa siku ni shida
Dunia haina usawa mazee.

Kama kuna mtu huko machakani hana hata mlo mmoja ilhali Jeff na wadau wengine wanatumia mamilioni ya dola kupaa anga za juu, then hilo ni lao na maisha yao. Duniani shida na wivu vitaisha iwapo tu "You mind Your own business"
 
Kwa wazungu kuna standard fulani ya maisha ambayo wote wanaishi, matajiri na maskini, kwa hiyo sio rahisi kujua utajiri wa mtu.
 
Kuna mzungu mmoja alinipa kazi ya kufanya utafiti kwenye sekta fulani. Sasa ilipofika kwenye kipengele cha malipo akasema watanilipa kwa Dollar je haitaleta ugumu kuingia kwenye akaunti yangu ya Tsh? Nikamwambia, no problem; I have a dollar account. Yule mzungu alishtuka sana na inaonekana hakufurahia mimi ngozi nyeusi kumiliki akaunti ya Dollar. Yani ilibaki kidogo ile deal ife pale pale tu kisa namiliki akaunti ambayo niliifungua kwa kutumia Dollar tano!
 
Mkuu huoni kuna walakini watu kuchezea na kuteketeza mabilion kwa mambo ya kipuzi wakati binadamu wenzao hata mlo mmoja kwa siku ni shida. Haileti mantik na uhiwuano kabisa.
Vipi mkuu kwenye kunywa bia & kununua papuchi zenye maji hayo sio matumizi ya kipuuzi
 
Mkuu huoni kuna walakini watu kuchezea na kuteketeza mabilion kwa mambo ya kipuzi wakati binadamu wenzao hata mlo mmoja kwa siku ni shida. Haileti mantik na uhiwuano kabisa.
Tutafute pesa, ili tusiwapangie wengine matumizi ya pesa zao.

Mkuu binadamu haridhiki, hata umpe vyote, kuna siku ataitaka roho yako.

Acha tajiri afanye apendalo,mladi havunji sheria.
 
Mkuu huoni kuna walakini watu kuchezea na kuteketeza mabilion kwa mambo ya kipuzi wakati binadamu wenzao hata mlo mmoja kwa siku ni shida. Haileti mantik na uhiwuano kabisa.
Ulitaka wafanyeje, hizo hela zitarudi kwenye mzunguko.
 
Back
Top Bottom