Usijidanganye kuwa mzungu kakuletea ustaarabu.
Basi bata neno "ustaarabu" halistuwi akili yako?
Wazungu wamekuletea ushetani.
Kweli kabisa mkubwa wangu.Ingekuwa kwenye hii jamii forum unaweka na mwaka wa kuzaliwa tungekuja kugundua wengi humu ni watoto wetu.Inasikitisha sana kizazi cha sasa mtu anashabikia mambo ya upinde.
Hata Marekani nako Donald Trump hii kitu amesema hawezi ruhusu nchini kwake amesema hili jambo sio jambo la kawaida na ndio kilichompa kura nyingi dhidi ya Democrat.Raisi Putin mwenyewe walijaribu wamarekani kuchomekea hii sera ya upinde akasema hawezi ruhusu nchini kwake.Watakao kamatwa yeye kama raisi chini ya utawala wake watu wa hivyo atamsaidia MUNGU kumfikishia huko mbinguni yeye mwenyewe MUNGU atatoa hukumu.
Raisi wa Korea Kaskazini wanayemwita Kiduku alipata kusema nashangaa nchi za Africa nchi za magharibi wanawafundisha kuwa wasizaane sana lakini hapo hapo wawashawishi kuwa ndoa ya jinsia moja ni haki za binadamu.
Nashangaa sana mtu ana comment kuwa wazungu wana hesabu kali unakuta mtu anaona ni sawa.
Mbona nchi za Kiarabu huu ujinga wanashindwa kuupeleka huko?
Hawa ndio vijana wetu wa kizazi hiki unaandika kitu cha logic wanakikandia inasikitisha sana.Hawa ndio watoto wetu tuliowasomesha na kuwategemea kuvusha kizazi hiki.Wengi humu wana elimu kubwa sana na nzuri tatizo wamekorogwa na hali ya maisha mtu anasoma vizuri shahada yake anakuja mtaani anakuta ajira hamna akili haziwezi kufikiria vizuri na wengine wanajiingiza kwenye nganda na ushoga inaumiza sana.
Kwa mtu muelewa na muadilifu hawezi shabikia huu ushetani ambao mataifa ya magharibi wanataka kutuletea.
Babu zetu mmoja wapo mfalme Mangungo wa Msovero walikubali kuuza nchi zao kwa kupewa shanga na pombe kali.Hawa babu zetu tunaweza wasamehe kwamba hawakuelimika lakini vijana wetu ni watu wenye elimu lakini wamepinda kiakili.
Najua nitapigwa mawe sana lakini sijali hata chembe maana nimeeleza ukweli hata MUNGU yuko na mimi siku ya mwisho akanihukumu kwanini hukuwaweka vijana wako sawa.