Wazungu tusaidieni kukabiliana na demokrasia ya kupita bila kupingwa

kavulata

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2012
Posts
18,154
Reaction score
17,491
Wazungu wanadhani kuwa Waafrika hatujafikia hatua ya kuwa watu kamili kama wao, hasa kutokana na namna tunavyofikiria na tunavyofanya. Bahati mbaya huwa tunawakasirikia sana wale wanapotusema vibaya kama hivyo. Lakini kusema ukweli matendo yetu ndiyo yanayosababisha watuseme hivyo. Wazungu walipitia hatua kama hizo miaka mingi iliyopita, walipigana na kuuana sana ili kuondoa tabia kama hizo kwenye jamii. Kwakuwa sisi hatujapigana kwa kiwango chao pamoja na uwepo wa sintofahamu nyingi ndani ya jamii ndiyo maana wanadhani hatujafikia ngazi ya kuwa binadamu kamili.

Sisi hatuhitaji kupigana na kuana ili kuondosha tabia za ujanjaujanja kwenye jamii, kwani tunayo fursa ya kujifunza kutokana na makosa ya watu wengine yaliyosababisha wauane wenyewe kwa wenyewe.

Kupita bila kupingwa ni demokrasia ya aina gani? Kama mgombea amekosea kujaza form kwanini asielekezwe ajaze tena vizuri? Kama mgombea hana sifa kwanini chamba kisiambiwe kiteue mgombea mwingine mwenye sifa ili demokrasia ya uchaguzi itendeke?

Kusema mgombea kapita bila kupingwa ni kitendo cha kulazimisha wananchi waongozwe na wasiomchagua, kitu ambacho sio sana leo na haitakuwa sawa kesho. Kukosekana kwa mgombea wa pili haimaanishi kuwa mgombea wa kwanza anakubalika kwa wananchi. Haidhuru basi mgombea aliyebaki angepigiwa kura za ndiyo au hapana.

Inavyoonekana wananchi tumeshindwa kuindoa kadhia hii kwa midomo yetu, hivyo tutalazimika kuomba msaada nje ya boksi.

Msaada tunaouomba ni wazungu kutusaidia:
1. Kupaza sauti zao dhidi ya aina hii ya demokrasia ambayo ina viashiria vibaya huko mbeleni.
2. Kuwazuia wote waliopita bila kupingwa na familia zao kuingia kwenye nchi zenye demokrasia
3. Kutoa elimu ya demokrasia kwa Afrika

Hapo tutakuwa tumesaidiwa sana kuliko kusubiri hadi mambo yamezorota kabisa.
 
Ni bora tumkabidhi nchi mbatia kuliko saccos
Apewe nchi yeyote yule baada ya kumsikiliza na kumchagua sisi wenyewe kwenye kisanduku cha kupigia kura. Mtu anayefanya kinyume chake anafahamu hata yeye kwamba ujanjaujanja hauwezi kuwa kila siku. Kuwadanganya watu walewale mara zote na siku zote haijawahi kutokea duniani, kwanini sisi tujidanganye wenyewe kuwa itakuwa hivyo milele bila chochote kutokea?

Tusisubiri hadi siku raia, wageni, wanajeshi, wanasheria na taasisi za kidini na taasisi za kimataifa wagawanjike kwenye mtazamo wa mambo ya kidemokrasia na utawala bora, tutakuja kujilaumu wote.
 
Wakurugenzi waliowapitisha wabunge na watendaji kata waliowapitisha madiwani kupita bila kupingwa wanatetea matumbo yao wasimkorofishe jiwe maana baada ya uchaguzi kama jiwe atapita atawatumbua wote ambao wamepitisha wabunge na madiwani wa vyama pinzani ili kuondoa mtu kutokuwa na msimamo wakuamua na kusimamia haki katiba mpya inaitajika maana njaa zinawasumbua viongozi
 
Wazungu wanadhani kuwa Waafrika hatujafikia hatua ya kuwa watu kamili kama wao, hasa kutokana na namna tunavyofikiria na tunavyofanya. Bahati mbaya huwa tunawakasirikia sana wale wanapotusema vibaya kama hivyo. Lakini kusema ukweli matendo yetu ndiyo yanayosababisha watuseme hivyo. Wazungu walipitia hatua kama hizo miaka mingi iliyopita, walipigana na kuuana sana ili kuondoa tabia kama hizo kwenye jamii. Kwakuwa sisi hatujapigana kwa kiwango chao pamoja na uwepo wa sintofahamu nyingi ndani ya jamii ndiyo maana wanadhani hatujafikia ngazi ya kuwa binadamu kamili.

Sisi hatuhitaji kupigana na kuana ili kuondosha tabia za ujanjaujanja kwenye jamii, kwani tunayo fursa ya kujifunza kutokana na makosa ya watu wengine yaliyosababisha wauane wenyewe kwa wenyewe.

Kupita bila kupingwa ni demokrasia ya aina gani? Kama mgombea amekosea kujaza form kwanini asielekezwe ajaze tena vizuri? Kama mgombea hana sifa kwanini chamba kisiambiwe kiteue mgombea mwingine mwenye sifa ili demokrasia ya uchaguzi itendeke?

Kusema mgombea kapita bila kupingwa ni kitendo cha kulazimisha wananchi waongozwe na wasiomchagua, kitu ambacho sio sana leo na haitakuwa sawa kesho. Kukosekana kwa mgombea wa pili haimaanishi kuwa mgombea wa kwanza anakubalika kwa wananchi. Haidhuru basi mgombea aliyebaki angepigiwa kura za ndiyo au hapana.

Inavyoonekana wananchi tumeshindwa kuindoa kadhia hii kwa midomo yetu, hivyo tutalazimika kuomba msaada nje ya boksi.

Msaada tunaouomba ni wazungu kutusaidia:
1. Kupaza sauti zao dhidi ya aina hii ya demokrasia ambayo ina viashiria vibaya huko mbeleni.
2. Kuwazuia wote waliopita bila kupingwa na familia zao kuingia kwenye nchi zenye demokrasia
3. Kutoa elimu ya demokrasia kwa Afrika

Hapo tutakuwa tumesaidiwa sana kuliko kusubiri hadi mambo yamezorota kabisa.
Tunavyo andika Yule waziri wa majalala ameitwa na mabalozi toka nchi za mabeberu, ameonywa na serikarili yake kuhakikisha wagombea walioenguliwa wanarudishwa haraka. Vinginevyo ????
 
Mkuu hii ni ya kweli? Weka nyama kidogo hii habari yaweza kuwa njema sana
 
Wazungu wanadhani kuwa Waafrika hatujafikia hatua ya kuwa watu kamili kama wao, hasa kutokana na namna tunavyofikiria na tunavyofanya. Bahati mbaya huwa tunawakasirikia sana wale wanapotusema vibaya kama hivyo. Lakini kusema ukweli matendo yetu ndiyo yanayosababisha watuseme hivyo. Wazungu walipitia hatua kama hizo miaka mingi iliyopita, walipigana na kuuana sana ili kuondoa tabia kama hizo kwenye jamii. Kwakuwa sisi hatujapigana kwa kiwango chao pamoja na uwepo wa sintofahamu nyingi ndani ya jamii ndiyo maana wanadhani hatujafikia ngazi ya kuwa binadamu kamili.

Sisi hatuhitaji kupigana na kuana ili kuondosha tabia za ujanjaujanja kwenye jamii, kwani tunayo fursa ya kujifunza kutokana na makosa ya watu wengine yaliyosababisha wauane wenyewe kwa wenyewe.

Kupita bila kupingwa ni demokrasia ya aina gani? Kama mgombea amekosea kujaza form kwanini asielekezwe ajaze tena vizuri? Kama mgombea hana sifa kwanini chamba kisiambiwe kiteue mgombea mwingine mwenye sifa ili demokrasia ya uchaguzi itendeke?

Kusema mgombea kapita bila kupingwa ni kitendo cha kulazimisha wananchi waongozwe na wasiomchagua, kitu ambacho sio sana leo na haitakuwa sawa kesho. Kukosekana kwa mgombea wa pili haimaanishi kuwa mgombea wa kwanza anakubalika kwa wananchi. Haidhuru basi mgombea aliyebaki angepigiwa kura za ndiyo au hapana.

Inavyoonekana wananchi tumeshindwa kuindoa kadhia hii kwa midomo yetu, hivyo tutalazimika kuomba msaada nje ya boksi.

Msaada tunaouomba ni wazungu kutusaidia:
1. Kupaza sauti zao dhidi ya aina hii ya demokrasia ambayo ina viashiria vibaya huko mbeleni.
2. Kuwazuia wote waliopita bila kupingwa na familia zao kuingia kwenye nchi zenye demokrasia
3. Kutoa elimu ya demokrasia kwa Afrika

Hapo tutakuwa tumesaidiwa sana kuliko kusubiri hadi mambo yamezorota kabisa.

Naona mnataka kuturudisha kwenye Ukoloni na Utawala wa mabeberu,Wapaze sauti kwa lipi?
Wagombea wasiojua kujaza form wataweza kuongoza wananchi?
 
umeandika kutoka moyoni?
 
Back
Top Bottom