Wazungu walipokuwa watumwa wa waarabu?

Wazungu walipokuwa watumwa wa waarabu?

Red Giant

JF-Expert Member
Joined
Mar 9, 2012
Posts
15,657
Reaction score
20,967
Kati ya mwaka 1500 na 1800 kulitokea biashara ya utumwa ambayo inaitwa barbary slave trade. Hii ilifanywa na watu wa Morocco, Tunisia, Libya na Algeria ambao walikuwa wanafanya wazungu watumwa.

Inaonekana katika kipindi hicho kati ya wazungu 1m hadi 1.25m walifanywa watumwa huko Afrika ya kaskazini. Hawa jamaa walichokuwa wanafanya ni kuvamia meli za wafanyabiashara na kufanya mateka kuwa watumwa. Pia walikuwa wakivamia vijiji vya ufukweni mwa Italy, Spain, Ureno, Ufaransa, Uholanzi, Uingereza, Ireland hadi iceland. Biashara hii ilikoma pale wamarekani, waingereza-waholanzi kwa nyakati tofauti walipoipiga miji ya Algiers na Tunis kwa mabomu

barbary-slave-trade.jpg
a977837c2bab8f50931d952be353319c.jpg
2c3a331fdee12ef367a93e3796499b44.jpg
 
mkuu mada nzuri sana hii "" ila naona kama umeinyima Nyama hivi nahisi kuna mambo mengi ulipaswa kutuhabarisha zaidi ya hayo uliyo tuonjesha...

Palantir
Malcom Lumumba.
zitto junior
yah, kuna mambo mengi yanayohusika. Mfano Jinsi ilivyoanza, majadiliano ya kuikomesha, vita vya kuikomesha, Kukomboa watumwa, kazi za watumwa. Ngoja wadau waje na mimi nikipata muda mzuri ntaongezea nyama.
 
Kati ya mwaka 1500 na 1800 kulitokea biashara ya utumwa ambayo inaitwa barbary slave trade. Hii ilifanywa na watu wa Morocco, Tunisia, Libya na Algeria ambao walikuwa wanafanya wazungu watumwa.

Inaonekana katika kipindi hicho kati ya wazungu 1m hadi 1.25m walifanywa watumwa huko Afrika ya kaskazini. Hawa jamaa walichokuwa wanafanya ni kuvamia meli za wafanyabiashara na kufanya mateka kuwa watumwa. Pia walikuwa wakivamia vijiji vya ufukweni mwa Italy, Spain, Ureno, Ufaransa, Uholanzi, Uingereza, Ireland hadi iceland. Biashara hii ilikoma pale wamarekani, waingereza-waholanzi kwa nyakati tofauti walipoipiga miji ya Algiers na Tunis kwa mabomu

barbary-slave-trade.jpg
a977837c2bab8f50931d952be353319c.jpg
2c3a331fdee12ef367a93e3796499b44.jpg

Binadamu wote Dunia hii washawahi kuwa Watumwa, sema tofauti ni kwamba sisi ndo watu pekee ambao tunauzwa Utumwa mpaka leo hii!
 
Ni kweli. sababu kubwa ni kuwa utumwa wa mtu mweusi umekomeshwa hivi karibuni ndiyo maana hadi leo effects zake zipo kwetu. Imagine eti watu weusi tulikuwa watumwa hadi wa waethiopia? Ethiopia wamekomesha utumwa miaka ya 1930s tu hapo. Kwahiyo athari za utumwa wa mtu mweusi hadi leo zinaonekana.
 
Utumwa wa mtu mweusi haujakomeshwa bado kwani Maurtania, Chad huko bado watu wanauzwa!
 
Kwenye nchi hizo kisheria utumwa umekomeshwa. Sema wale vizazi vya watumwa vinaamua kuwa watumwa kwa ridhaa yao na ugumu wa maisha. Wanaona hawawezi kuishi bila ma master wao.
 
yah, kuna mambo mengi yanayohusika. Mfano Jinsi ilivyoanza, majadiliano ya kuikomesha, vita vya kuikomesha, Kukomboa watumwa, kazi za watumwa. Ngoja wadau waje na mimi nikipata muda mzuri ntaongezea nyama.
anhaaa"" ngoja nikae Kitano sawa "" sasa
 
Utumwa wa mtu mweusi haujakomeshwa bado kwani Maurtania, Chad huko bado watu wanauzwa!
ukiwaga nje ya jukwaa la siasa huwa unaitumia akili yko vyema "" kama vile una genes za alliance""
 
UTUMWA MBAYA ZAIDI NI UTUMWA WA KIFIKRA. KUAMINI CCM AU CHADEMA NDO WENYE UWEZO WA KULETA MAENDELEO TANZANIA
 
Yes ni ule wakati hao waarabu kutoka Afrika kaskazini wakishirikiana na watu weusi wakijulikana kama Moors walitawala Portugal,Spain na Italia. Hayo maeneo damu ya watu weusi bado ipo ndo maana waitaliano wa kusini mwa italia hasa Sicily wengine sio weupe kama wale wa kaskazini. Hata Sicily italia, Ureno na Hispania hawa Moors walitawala kwa miaka takriban 200.
Hadi leo bendera ya Sardinia kule Italia ina alama ya mtu mweusi Moor aliekua malkia wa Ufalme wa Aragones kule Spain ambao Sardinia ilikuja kua chini ya Aragones.
 
Yap baada ya hao moors kufukuzwa Hispania kwenye recoquista wakaelekea Afrika kaskazini. Huko ndiyo wakawa mapirates wa kukamata watumwa wakizungu. Walishaonja wazungu kuwa chini yao
 
I agree to disagree!
Ila jamaa anataka kutuaminisha kwamba mtu mweusi alifanya utumwa bila pingamizi yoyote. Anapotosha. Kwenye historia kuna muafrika mtumwa alijifunza kusoma. Akaanzisha uasi wa watumwa. Alipata mafanikio madogo mwanzoni lakini alishindwa na madhara yalikuwa mabaya sana, kuna stori pia ya watumwa walioteka meli iliyowabeba. Pia huko uarabuni kuna kitu kinaitwa Zenj rebellion. Ni watu weusi watumwa walioasi.

Mtu mweusi hakuwa weak bali Teknolojia ya bunduki na ile kuvushwa mto mkubwa(Kunta kinte aliita bahari ya atlantiki mto mkubwa) mbali na nyumbani, unaenda ugenini huelewi kitu kuhusu nchi hiyo, ukifanyishwa kazi ngumu , watumwa wenzako wako mbali kwenye plantation nyingine na adhabu kali zikitolewa ni ngumu kujitetea
 
Back
Top Bottom