Wazungu wana akili, wameweka mtego, wakifanikiwa hili la mimba mashuleni wanakuja kwenye lengo lao hasa, Ushoga!

Wazungu wana akili, wameweka mtego, wakifanikiwa hili la mimba mashuleni wanakuja kwenye lengo lao hasa, Ushoga!

TataMadiba

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2014
Posts
9,866
Reaction score
5,747
Ndiyo wanajua kuna Watanzania Majuha wanawaunga Mkono . Najiuliza hivi hawa Watoto wanaopata ujauzito Mashuleni wameanza kuzuiliwa kurudi awamu hii? Nakumbuka wakati nasoma kuna wanafunzi walikuwa wakipata ujauzito, wanachukuliwa na gari la shule chini ya ulinzi wa Matron wa shule na Polis hadi anakabidhiwa kwa wazazi wake kijijini na inakuwa ndiyo nitolee.

Hiini aibu kwa taifa kabisa. Naogopa nifiche wapi uso wangu. Lazima watoto wetu wakiume nao wataomba ushoga uhalalishwe na wataanzia kuomba huko huko Mashuleni, tutafanyaje? itabidi tukubali tu.Aibu.

Mungu chukua roho za hawa vibaraka wanaonunuliwa kwa vipande vya fedha za Wazungu ili Taifa lipate kupona.

Leo akina Zitto wanajifanya wakati wanasoma hawakuona hizi Sheria za Shule zikifanyakazi kweli? AIBU

2.PNG

3.PNG
 
Nji hii tajiri tena ina hela za kutosha hatubabaiki na kimkopo cha tilioni moja mabeberu watembee mbere kama tumenunua madreamliner manane cash. Hatuwezi kukosa tilioni moja ya kusomesha wanyonge
 
TataMadiba,

Uongozi wa nchi siwalikubali warudi mashuleni lakini si shule za serikali?
Sasa kama serikali ilnawakataa, iweje waruhusu shule binafsi kuwapokea
 
Akati zito na wezake wakipiga kelele huko ,njooni nampango wakutisha watu kisheria .huwezi tunga masheria yaajabu akati huna mipango mathubuti kwajili ya watotot mashuleni

Sent using Jamii Forums mobile app
Hyo sheria ilitungwa mwaka gani? Hao akina Zitto wako bungeni miaka nenda miaka rudi leo ndo wanaiona baadfa ya Magufuli kudhibiti mianya yao ya kutuibia?
 
Mzee wa Jalalani kishadai kuwa hawabaguliwi na next month akitua Gineva atawasomesha... Sasa sijui unataka Mabeberu wafanikiwe mara ngapi kwa hili...!!?
 
Uongozi wa nchi siwalikubali warudi mashuleni lakini si shule za serikali?
Sasa kama serikali ilnawakataa, iweje waruhusu shule binafsi kuwapokea
Zamani walikuwa wanarudi hizo shule za Serikali? Magufuli kawaweza kwelikweli mnatapatapa hovyo
 
Nadhani ka hilo ndio limempeleka Zitto huko na aende zake huko akawaombe WB watunyime huo mkopo. Mimi si mtetezi wa serekali ila nasema; Kama sharti la kuupata huo mkopo ni lazima kubadili sheria na kuruhusu mimba mashuleni, basi na tuukose.
Sheria hii haikuanza leo, imekaa nasi tangu uhuru, ndo maana wanawake wengi wakasoma. Sasa kama mnaanza kuruhusu huu mchezo shuleni nadhani mnamaliza kabisa kaelimu ketu haka ka kuungaunga.
We msichana; Huwezi kutumikia mabwana wawili. Huku shule huku mtoto na jioni ukitoka uende kumtumikia bwanako pia kwani yeye ndiye atakuwa anakulipia shule mahitaji yako yote. Uwezo huo unao??
Najua wapo mtakaosema; Mbona wanaojiunga na pprivate schools huwa wanafanya vyema?? Sawa, lakini wachunguze mapito wanayo yapitia. Leo mkiruhusu huu upuuzi ndo mtajua mlikoenda.
Tusikubali ujinga huu. Heri tukose mkopo huu ku;liko aibu inayo fuata
 
Hili la watoto wa kike kupata mimba limekuwepo kwenye sheria za shule toka enzi za mchonga.

Ni malimbukeni wa kujikomba kwa mabeberu ndio wanadhani wataendelea kula grants in the name of social justice and human rights advocacy.

Kuna watu wanapata moto as if ni JPM ndiye kaasisi utaratibu huu mashuleni. Kwanza ikumbukwe enzi tunasoma, kosa la uasherati tu ( hata kama mimba haijaingia) ilikuwa ikithibitika watu walikuwa wanapugwa.

Umasikini mbaya sana. Unakopa kwa ajili ya shule, yet anaekukopesha kwa kuwa wao moral decay is the "culture" in their communities wanataka na sisi tulegeze msimamo, walete tabia huria za hivyo kwenye jamii zetu.

Mambo haya, mbona mabeberu hawayatiliii maanani kwa nchi kama Saudia?

Poverty is very very expensive

Sent using Jamii Forums mobile app
 
TataMadiba, Kuna Mtu aliwahi kuniambia kuwa kama kuna Taifa linaloongoza kwa kuwa na Raia Wanafiki duniani basi ni Tanzania na sasa naamini.
 
TataMadiba,

Watanzania tunapoteza muda mwingi kujadili uongo kama nilivyosema. Kuna nchi nyingi sana Duniani zinapinga ushoga kama nchi za kislamu sasa kwanini mikopo na misaada huko inaenda katika nchi za Africa Misri ndiyo inaongoza kwa misaada kule ushoga hauruhusiwi.

Kila kitu kilitokea Tanzania tunasingizia ushoga. Marakani yenyewe ushoja sio watu wote wanaukubali sema tu mahakama imepiga marufuku kubagua kwa namna yeyote hata kama mtu ni shoga mfano huwezi kumpiga mtu mawe au kumpiga kwa kisingizio cha ushoga.

Hili ni tatizo tofauti na mimba za watoto. Watoto ni wetu na hawapewi mimba na wazungu! sisi na utamaduni zetu nyingine wanaruhusu kuolesha watoto, wengine bado hawana akili ya kiutu uzima hivyo wanadanganywa na ndiyo maana watoto wanatakiwa kuangaliwa na watu wazima kwasababu bado hawana uwezo mkubwa wa kufikiria.

Huwezi tu kusema tunafukuza shule watoto wakati 67% ya Watanzania wote ni chini ya miaka 24 na umri wa kati Tanzania ni miaka 17.5 tu. Tuache tabia ya kulaumu wazungu kwenye kila kitu.

Miaka ya 1950-1960 wazazi walikuwa wanalazimishwa kupeleka watoto shule na sehemu zilizopeleka watoto shule zimekuwa na maendeleo zaidi hivyo tusikokuwa waangalifu tutaumiza watoto masikini.

Tujue mtoto wa kike wa tajiri atasoma tu hata kama ana mimba lakini kwa watoto wa masikini ambao wengine inawezekana hata mimba wamepata kwa kubakwa ndiyo wanaoumia.

Je serikali imehoji kwamba ni wangapi wamebakwa?
 
Back
Top Bottom