Wazungu wana akili, wameweka mtego, wakifanikiwa hili la mimba mashuleni wanakuja kwenye lengo lao hasa, Ushoga!

nijuavyo mimi hii sheria imekuwepo toka kitambo, ni ujuha wa mtu mmoja alieropoka majukwaani mpaka ikapelekea wazungu kusikia na kuanza kutujadili, mara oohh sisi ni matajiri, kujitapa pasipokua na mpango ndio yanaletezea haya, kwa hio tukubaliane tu hamna namna!
 
Hyo sheria ilitungwa mwaka gani? Hao akina Zitto wako bungeni miaka nenda miaka rudi leo ndo wanaiona baadfa ya Magufuli kudhibiti mianya yao ya kutuibia?
Usiwe nakichwa chepesi kusahau ,ccm miaka yote ndiyo wagonga meza ...utawalaumu akina zito waliokua watatu pengine ,sema bunge LA ccm.sio LA jamhuri yamuungano tz almaarufa LA Tanganyika

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hatulazimishwi na wazungu kuwa mashoga.

Kama unataka kuwa shoga hata leo hakuna anayekukataza.
Wala hayuko polisi anayepita vyumbani mwa watu kutafuta mashoga.

Leo hii ukiamua kuwa shoga, hukamatwi, na huna kisingizio cha kusema umelazimishwa na wazungu.

Kama ni suala la kukosa mkopo kwa kutojua madhara ya kupangilia maneno kabla ya kusema, basi tukubali kwamba hili ndilo tatizo letu.

Mwambieni mzee Meko aongee kwa staha na heshima kwa jamii, vinginevyo haya ndiyo madhara yake.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hawa ndio wanaharakati wa Tanzania, Sasa jiulize mtu Kama huyo akija kuwa Rais siku moja ujue kabisa tumekwisha.
Nadhani huyu mtu sio bure kuna faida fulani anaipata kwa kufanya haya anayo yafanya.
 
Mkuu naomba nikukumbushe tu kwamba, WB hawakuzuia mkopo kwasababu heti Rais amesema kuwa hasomeshi wajawazito bali huyu anaye jiita mwana harakati mh Zitto kaandika barua kwa WB akiwaomba kuzuia mkopo kwasababu anataka watoto wenye mimba waruhusiwe kusoma.
Sasa kwanini kaandika barua hiyo ya kuomba kuzuia huo mkopo? Ni kwasababu Rais alisema? Kama ni hivyo yeye Zitto haukuwa anajua hii sheria kuwa ipo siku nyingi Kama kujua baada ya Rais kusema??
Je mh Zitto ni kweli kuwa anaunga mkono mimba mashuleni??
Au lengo lake ni nini hasa kumkomoa Rais??
 
Usipotoshe wingi wa wabunge bungeni ndo inawakosti hivyo ,njia zikonyingi
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nji hii tajiri tena ina hela za kutosha hatubabaiki na kimkopo cha tilioni moja mabeberu watembee mbere kama tumenunua madreamliner manane cash. Hatuwezi kukosa tilioni moja ya kusomesha wanyonge
Mhanga wa mimba za shuleni.
Umeshajifungua??

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Maoni: Serikali ianzishe Mimba Girls secondary school. Shule iwe na clinic ndani, malimao, maembe mabichi yawepo pamoja na ambulance ya kuwapeleka wajawazito hospitali.
Kisha mabeberu waje wafungue na watoe ufadhili.
Walimu wote wa shule hizo wawe wanawake watu wazima pekee.
 
Hakuna aliyesema mimba ziruhusiwe mashuleni bali mtoto hapaswi kupewa adhabu ya kukosa elimu kisa tu amepata mimba akiwa shuleni.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Basi watulie waache kulilia misaada kwanza wameshasema Tanzania ni donor country.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwa hiyo mimba zianze kuruhusiwa shule za msingi na sekondari? kutakuwa na maadili kweli? Hao WB wana maslahi gani na watoto kupata mimba shuleni, baada ya hapo litakuja na la ushoga tusubiri tuone..
 
Basi watulie waache kulilia misaada kwanza wameshasema Tanzania ni donor country.

Sent using Jamii Forums mobile app
By the way tume-donate by implication Tril 400+ kwa kumsamehe Barrick;
Airtel nao walituibia mwaka jana tukakaa nao mezani tukasamehe tukasonga mbele.

Hatutakufa kwa kukosa mkopo wa Tril 1 amvayo ni sawa na makusanyo ys TRA ya mwezi mmoja, ni sawa na deal ya akina Kangi kama isingebuma.

Tanzania is a sovereign state. Suala la mabinti wenye mimba kutokuendelea na masomo ni la siku nyingi..ila kwa kuwa mabeberu ndiyo marefa na wamepata ma-activist wanaotegema grants toka kwao huko huko; ngoja watunyime baada ya nguzo ya muda tutakuwa na akili zaidi ya nini cha kufanya.
Kama tunakumbuka; Mwai Kibaki baada ya kunyimwa misaada 2007-2012; Kenya iliweza kubuni vyanzo vya mapato na utegemezi kwa mabeberu ulipungua sana tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…