kavulata
JF-Expert Member
- Aug 2, 2012
- 13,778
- 14,214
Nani ameturoga? Kumfungia mwamuzi bila kudhibitisha pasipo kuacha mashaka kuwa mwanafuzi amekosea kwa makusudi na siyo kwa bahati mbaya ni kuonyesha namna tunavyodharaulika duniani.
Ni nani ana ushahidi kuwa waamuzi wetu wamekosea kwa kudhamiria? Hata sisi watazamaji tunategemea fursa ya kutazama picha za marejeo ya matukio uwanjani kubaini makosa ya waamuzi tunayotumia kuwahukumu waamuzi.
Wazungu wana marefa bora kabisa duniani wanaolipwa vizuri sana kuliko hawa wetu lakini wameona bado wanakosea hadi ikabidi watumie VAR, sisi tuna waamuzi ambao wana mafunzo ya kubabaisha na malipo ya hovyo kabisa lakini tunataka wasikosee uwanjani.
Nani katuroga? Kumfungia mwamuzi kwa kosa la kudhania sio weledi. Tufunge VAR basi ili tuwasaidie kupunguza makosa ya kibinadamu.