Wazungu wasitishe misaada nchi za Afrika mpaka pale rushwa na ufisadi vitakapoisha

Wazungu wasitishe misaada nchi za Afrika mpaka pale rushwa na ufisadi vitakapoisha

Mwamuzi wa Tanzania

JF-Expert Member
Joined
Apr 7, 2020
Posts
15,486
Reaction score
45,256
Tangu nikiwa mdogo nasikia bilioni kadhaa zimetolewa na Uswizi kama msaada kwenda nchi fulani ya Afrika.
Mara Marekani imetoa msaada bilioni mia 4 kwenda nchi fulani.

Lakini hizi nchi zinazoongoza kupokea misaada hali ya maisha bado ingalipo.

Mpaka leo si vyama tawala au vya upinzani kipindi cha uchaguzi wanatoa ahadi za kujenga zahanati, mara kujenga barabara n.k.

Vitu hivi kama rushwa na ufisadi vingekoma Afrika vingekuwa vimeshatatuliwa na sasa tungekuwa tunazungumza ahadi za usalama wa wananchi na mambo mengine .

Misaada ikome haraka. Tutumie pesa zetu tu huenda tutadhibiti rushwa na ufisadi
 
Halafu wao watapata wapi Utajiri?

Utajiri wao unakuja kwa kutoa misaada. Kwa kufanya hivyo wanakwepa kulipa kodi kwao.

Watoa Rushwa ni wao. Watoroshajji wa fedha-capital flight-zinafanywa na wazungu hao hao, according to Pandora papers report.

Tanzania tulikuwa na Raisi aliyekataa hiyo misaada yenye masharti- mkaanza kusema "tunajitenga"

hebu fikiria kwanza-Unatoa msaada kwa masharti? Huo ni msaada ama ni mkopo?

Kama haitoshi, rushwa na Ufisadi umeletwa na wazungu. Kwamba wao ndio watoa rushwa wakubwa na wachochezi wa Ufisadi katika bara la Afrikam

Waache, hakuna anaye walazimisha. Halafu tuone huo utajiri wao wa kutoa misaada utafikia wapi.

Aluta Continua.
 
Back
Top Bottom