- Source #1
- View Source #1
- Source #2
- View Source #2
Kumekuwepo na chapisho linalosambazwa katika mitandao ya kijamii, hususan Facebook na Instagram, likiwa na nukuu inayoambatana na video inayodaiwa kuwaonesha waandamanaji wakishambuliwa kwa risasi nchini Afrika Kusini. Chapisho hilo linadai kuwa tukio hilo linahusiana na hali ya hivi karibuni ambapo raia wa kigeni wanadaiwa kushambuliwa na kulazimishwa kuondoka nchini humo.
- Tunachokijua
- Hadi Kufikia Aprili 2026, Afrika Kusini imeshuhudia tena ongezeko la wa chuki dhidi ya wageni, huku mamlaka zikiahidi kuchukua hatua kali dhidi ya matukio ya vurugu yanayolenga raia wa kigeni, hasa kufuatia matukio yaliyotokea katika eneo la KwaZulu-Natal.
Kumekuwepo na chapisho linalosambazwa katika mitandao ya kijamii, hususan Facebook na Instagram, likiwa na nukuu inayoambatana na video inayodaiwa kuwaonesha waandamanaji wakishambuliwa kwa risasi nchini Afrika Kusini. Chapisho hilo linadai kuwa tukio hilo linahusiana na hali ya hivi karibuni ambapo raia wa kigeni wanadaiwa kushambuliwa na kulazimishwa kuondoka nchini humo.
Katika mojawapo ya machapisho hayo, imeandikwa:“Kundi la waandamanaji huko Afrika Kusini lilikumbana na mapambano makali yaliyohusisha matumizi ya silaha za moto mara baada ya kuingia katika mojawapo ya mitaa maarufu inayokaliwa kwa wingi na raia wa kigeni, wakiwemo kutoka bara la Asia na Ulaya.”
Vilevile, chapisho jingine katika mtandao wa Instagram linaeleza:“Video iliyosambaa inaonesha Waafrika Kusini wenye asili ya Kiafrika wakikimbia kuokoa maisha yao baada ya kusukumwa nyuma na Waafrika Kusini wenye asili ya Ulaya kufuatia mapambano ya vurugu. Hali hii inadaiwa kutokea wakati wa mashambulizi yenye chuki dhidi ya wageni yaliyofanywa na baadhi ya Waafrika Kusini dhidi ya raia wa kigeni nchini humo.”
Hata hivyo, uchunguzi wa kina kwa kutumia nyenzo ya utafutaji wa maneno muhimu umebaini kuwa video hiyo si ya matukio ya sasa. Badala yake, inahusiana na vurugu zilizotokea mwezi july mwaka 2021 nchini Afrika Kusini kufuatia kufungwa kwa rais wa zamani, Jacob Zuma, baada ya kukaidi amri ya mahakama.
Katika vurugu hizo, inakadiriwa kuwa zaidi ya watu 72 walipoteza maisha na wengine zaidi ya 200 kujeruhiwa.
Hivyo basi, video hiyo haiakisi matukio ya sasa nchini Afrika Kusini, ambako kumekuwepo na taarifa za ubaguzi na shinikizo dhidi ya raia kutoka mataifa mengine ya Afrika kuaondoka katika nchi hiyo