WB: Takribani nusu ya wanaoishi katika umasikini mkubwa chini ya Jangwa la Sahara wanapatikana kwenye nchi tano Tanzania ikiwemo

Alafu tunajengea marais wastaafu mahekalu huku mamilioni ya wanaanchi wa kawaida wanaishi katika lundo la umasikini.
Usishangae hilo. Shangaa chama cha Chadema kinachofikiria kushika dola na kuwaletea maendeleo Watanzania huku chama chenyewe hakina hata ofisi!
 
..au tunatumia billion 495 kununua ndege tusizozihitaji.

..fedha hizo zingeweza kujenga vyuo 49 vya ufundi na kubakisha chenji.

Mbona mmeshindwa kujenga ofisi za chama chenu pamoja na kupokea ruzuku ya millioni zaidi ya 300 kila mwezi? Je, hapo chenji haibaki?
 
Yaah! Nimefurahi kusikia hivyo ili niendelee kupambana zaidi ili kuitoa nchi yangu kwenye hiyo list.

Naamini Jitihada zangu ndo zitafanya maisha yangu kuwa mazuri au mabaya hayo mengine yaliyobaki Niya watu wazembe na watu wa kulia lia.
Nilikuwa nimeajiri watu 12 kwenye duka la kubadilishia hela. Nikaporwa na biashara kufa.
Kule kusini,kwenye korosho,niliajiri Watanzania 177. Biashara imekufa kwa kuingiliwa na watu waishio Dodoma wasiojua "a" wala "b" ya korosho.
Uwakala wangu wa vinywaji uliajiri watu 32. Leo hii kutokana na nguvu ya manunuzi ya Watanzania kupungua sana,nimebakisha wafanyajazi 14 tu.
TADB wameninyima mkopo ambao ungeajiri Watanzania 262 kwenye hekari 1800.
Hapo bado unaamini bila serikali kukuwekea mazingira mazuri,jitihada zako pekee zitafanya "utoboe"!?
 
Ukiitendea mabaya Jamii uikomoi Jamii bali umeharibu image ya uzao wako ile laana ya hatia ya maovu dhambi ulizoitendea Jamii zitaiandama kizazi chako milele.
Kizazi cha Iddi amini, bokasa, mobutu kwenye interview ya ajira thamani yake si sawa kiuzito na familia ya Mandela.
Ukiitendea mema Jamii umeiwekea hazina ya kudumu kizazi chako
 
Ukiitendea mabaya Jamii umeharibu cv ya uzao wako
 
Usitake kupinga mtazamo Wangu kwa kuleta hoja za propaganda hapa.
Hapo 99% ulichoandika ni propaganda tu.
 
Usitake kupinga mtazamo Wangu kwa kuleta hoja za propaganda hapa.
Hapo 99% ulichoandika ni propaganda tu.
Usifikiri kila mtu anafanya ufanyacho jamaa.
Ningekuwa huko TZ, ningekuita mahala uone hali halisi.
Usininukuu tena tafadhali,kama u timamu.
 
Tanzania tuna unafuu sana na hii ni sababu ya sera nzuri na mikakati katika kuzisaidia kaya maskini lakini uwepo wa miradi mingi ya maendeleo ambayo imeweza kuzalisha fursa za ajira na kuchochea uchumi haya yote ni kwasababu ya usimamizi mzuri wa JPM.

October 28th tutakwenda kumchagua kwa KISHINDO Magufuli.

JPM ANATOSHA
CCM KWA MAENDELEO YA TANZANIA
Jamani nyie mnaotmebeq huku na kule,,givi maisha ya kawaida ya Mtanzania ukilinganisha na ya Mganda,Rwanda,Zambia, Malawi, Msumbiji..wapi kunaunafuu wa umasikini?
 
Hii hutasikia Akina Polepole wanasema. Unfortunately hata waandishi wetu wa Habari hawatauliza... Ila kwenye mideal income kelele zake haziishi. Hawajui hata Zambia na Zimbabwe waliingia huko Siku nyingi. Ndiyo maana Mkapa (RIP) alitaka $3000.
Maono ya mzee Mkapa binafsi nimeyaheshimu sana. Kila ukisoma reforms alizozifanya na malengo yake unagundua alikuwa na maana bora sana kwa nchi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…