Nilikuwa nimeajiri watu 12 kwenye duka la kubadilishia hela. Nikaporwa na biashara kufa.
Kule kusini,kwenye korosho,niliajiri Watanzania 177. Biashara imekufa kwa kuingiliwa na watu waishio Dodoma wasiojua "a" wala "b" ya korosho.
Uwakala wangu wa vinywaji uliajiri watu 32. Leo hii kutokana na nguvu ya manunuzi ya Watanzania kupungua sana,nimebakisha wafanyajazi 14 tu.
TADB wameninyima mkopo ambao ungeajiri Watanzania 262 kwenye hekari 1800.
Hapo bado unaamini bila serikali kukuwekea mazingira mazuri,jitihada zako pekee zitafanya "utoboe"!?