WCB mfumo wa uongozi mikataba n.k

Maana kuongoza watu kwenye tasnia ya burudani ni shida maana wengi hawajui ethics za kazi na ndio maana mtu akiondoka sehemu anaondoka na maneno mengi sijui kule hali ilikuwa vile wakati tasnia ya burudani ni ajira kama zilivyo ajira nyingine ambapo ukipigwa chini unaondoka kimya kimya tena ukiomba kazi sehemu nyingine wala huzungumzi mabaya ya mwajiri wako..kuepusha shari kuna watu kama kina Kifesi kwa nafasi zao unawapa mkataba wa miaka michache michache ili kama wakizingua unawabwaga
 
Haijawahi tokea kwa sababu hawataki kufanya hivyo na sababu ya kutokufanya hivyo nimeeleza pale juu kama nawewe ulivyoieleza ni hofu upande wa lebo kwamba watakimbiwa na msanii.

Lakini tukija kwa upande mwingine mikataba mifupi ina manufaa makubwa kwa msanii leave along hiyo miwili au mmoja itaonekana michache basi kwanini isiwe minne au mitatu kwani albamu haikamiliki kwa muda wa miaka mitatu?

Ila Mavoko ameingia mwaka 2016 leo unataka kutoka angekuwa na mkataba wa miaka mitatu ungekuwa unaisha mwakani ni rahisi kuvumilia
 
Tukitumia neno "wanahofu watakimbiwa na wasanii....!" nadhani hiyo phrase sio sahii sana kwa sababu it sounds too personal wakati ukweli ni kwamba, it's all about business... na hiyo no popote pale utakapoenda!

Na popote utakapoenda, mikataba yao ni ya muda mrefu unless kama Msanii ni mkubwa mno compared na Lebo! Leo hii Pozi kwa Pozi Entertainment inaweza kukubali kumsaini Diamond hata kwa miezi 6 kwa sababu PKP inamuhitaji zaidi Diamond kuliko Diamond anavyoihitaji PKP!

Anyway, nimeeleza mengi kwenye post ya kwanza, sioni sababu ya kurudia tena hapa labda niende moja kwa moja kwa issue ya Rich Mavoko!

Kama Rich Mavoko alisaini mkataba wa hovyo katu siwezi kuwalaumu WCB! Mavoko ni mkongwe kwenye game!! Mavoko anazifahamu fika fitina za tasnia ya burudani, au angalau tasnia ya muziki! Mavoko alishawahi kuwa hadi kwenye management ya nje ya nchi! Maelezo yote hayo yanathibitisha jambo moja tu: Rich Mavoko ni mzoefu wa haya mambo!

Sasa ikiwa pamoja na yote hayo, kwanini basi alisaini mkataba wa hovyo?
1. Labda ni mpumbavu!! Sio mjinga bali ni mpumbavu kwa sababu mjinga ni yule asiyejua! Kwanini alisaini mkataba wa hovyo wakati yeye ni mzoefu wa haya mambo? Alilazimishwa? Jibu HAPANA, so WHY? Because--

2. Huenda Mavoko alifahamu fika kwamba mkataba ni wa hovyo lakini alitaka kuitumia WCB kumrudisha kwenye game! Hata kama kuna baadhi ya watu wanaodai WCB ilikuwa inampoteza Mavoko lakini ukweli ni kwamba Mavoko alienda WCB wakati ameshaanza kupotea kwenye game!

Hivyo basi, inawezekana kabisa alifahamu mkataba haukuwa mzuri lakini akaamua tu kusaini huku akitegemea, akisharudi tu kwenye chati, basi anatafuta way out!!!

Smart, right?! Yes or no!

Atakuwa amecheza smart endapo tu wakati anasaini tayari alishaona loophole kwenye mkataba vinginevyo, it's nice try lakini kachemka! Kachemka kwa sababu BASATA hawawezi kumsaidia kwenye mkataba usio na kasoro! Hata kama alisaini miaka 50 huo mkataba huwezi kuita una kasoro UNLESS kama kuna sheria ya nchi inayosema mkataba kati ya msanii na lebo hautakiwi kuzidi miaka xyz!

Au, BASATA wanaweza kumsaidia Mavoko ikiwa WCB wamekiuka terms za mkataba na mkataba una kipengele cha "free way out" ikiwa lebo imekiuka terms fulani fulani!

But for what I know, napata shaka ikiwa WCB wanaweza kutoa mkataba wenye kasoro... those guys hawakwenda shule but wana smart people nyuma yao!!!!!

Lakini kwa upande mwingine, kwa umaarufu wa Mavoko, hata kama alishaanza kupotea bado alikuwa na uwezo wa ama ku-negotiate better terms au hata kukataa!!!

Lakini kwanini mambo kama haya yanatokea sana?!

Nishawahi kusema mara kadhaa hapa kwamba, Tanzania tuna Wanasheria lakini hatuna Wanasheria wa Burudani; yaani Entertainment Lawyers. Anyway, hilo la Entertainment Lawyers lipo juu ya uwezo wetu lakini angalau tungekuwa na Wanasheria wanaoifahamu vyema tasnia ya burudani!!! Narudia, kuifahamu tasnia ya muziki na sio kuufahamu muziki!

Hii tasnia (ya burudani) ingawaje watu wanaichukulia poa lakini ipo very complex!!

Leo hii unaweza kusaini mkataba kwa sababu tu umeangalia basic benefits bila kufahamu kuna benefits zingine kadhaa ambazo kwa level uliyokuwa nayo, huwezi kuziona kwa sababu zinaibuka kadri unavyozidi kuwa mkubwa!!

Kwa mfano, ikiwa mkataba kati ya Harmonize na WCB umeangalia tu mapato yanayotokana na shows, streaming, digital and cd sales na endorsement! Halafu leo hii, WCB wanaamua ku-print TShirt za KWANGWARU halafu zinauzika ile mbaya!

Now tell me, wewe Harmonize unaenda kudai share ya mauzo ya tshirts kwa kutumia grounds zipi ikiwa mkataba wako hausemi chochote kuhusu hilo, whether directly or indirectly? Mbaya zaidi (na mara nyingi inakuwa hivyo), unaweza kukuta nyimbo zako ni mali ya lebo... refer Saida Karoli vs FM Studio (Mzee Mutta)!!

Halafu hizi lebo hizi' we acha tu! Zina invisible costs kibao ambazo baadae zinageuka kuwa kitanzi kwa msanii!!! Na hizi costs lebo wanaziingiza makusudi ili "balance sheet" ya msanii always iegemee upande wa debit!!!

Hata hivyo, kwa Mavoko sitarajii kama hazifahamu janja janja kama hizi unless kama ni stupid!!!!
 
Hata kama ukitudanganya sisi tutajuaje?
By the way, si hadithi tamu
 
Huyu jamaa ninachomshauri akomae mwenyewe, tunaweza tukawalaumu WCB, wakati yy mwenyewe mavoko ana matatizo, kwa nini nasema hivyo?

Jamaa kaanza kuwa managed na Papaa Misifa, mpaka Papaa akampeleka mahakamani kwa kukiuka mkataba na akataka alipwe mil 50, sijui walimalizana vipi. Baadaye kakimbilia Kenya kwenye label ya King Kaka ya Rabbit wakazinguana na King kaka akavunja mkataba now ni WCB nao kazinguana nao, japo hatujauona mkataba lkn mavoko bado namuona ana matatizo.

Alafu maswala haya ya mara nyingi mikataba yake ni ya muda mrefu, Kanye kazinguana na Jay Z lkn bado yupo chini ya Roc Nation, Lil Wayne pamoja na kazinguana na birdman bado yupo chini ya Cash money na hawa wote wapo ktk label zao zaidi ya miaka 10, njoo kwa nick minaj na Drake wana miaka zaidi ya 9 ktk label ya young money, njoo kwa kendrick lamar, yupo chini ya Dr dree zaidi ya miaka 5.

Wanafanya hivi sababu label wanawekeza hela ndefu sana na ndio maana wanafanya mikataba ya mda mrefu ili hela yao irudi.Ila kwa wenzetu ulaya mkataba unabainisha kama labda label itasimamia distribution ya nyimbo online, kwenye maredio pamoja na promotion, ring tones nk au vyote kwa pamoja lkn msanii kama akiwa na ishu zake kama yy mwenyewe kuwa na label au kuwa na biashara yake ambayo haikubainishwa ktk mkataba basi hela yote ni ya msanii sasa sijajua mkataba wa mavoko unasemaje.

Ila WCB naona kama wamemfanyia favor kwani Baraka da prince, kiss Daniel, wizkid hawa walinyang'anywa mpaka acc zao za YouTube baada ya kuvunja mkataba na label zao. Ila naona muda umefika kwa wasanii kuwa na wanasheria wao na wao wenyewe waiheshimu mikataba ila nimesikia mkataba umepelekwa wizara ya michezo kwa kuangaliwa zaidi, sasa ngoja tusubiri.
 
Mkuu mimi sitofautiani na wewe naona Mavoko hakuwa makini kusaini mkataba wa aina hiyo. Kwa sababu sioni sababu ya msanii ambaye alikuwa ameshatoka kama Mavoko kuingia mkataba wa muda mrefu hivyo. Angalau basi ingekuwa miaka miwili, mitatu au minne hiyo inatosha kwa msanii ambaye hahitaji nguvu nyingi kumtoa.

Kwa harmonize kwa kuwa alikuwa hajatoka kimuziki nadhani kwake mkataba wa miaka mitano au Sita ungetosha sana. Lakini mkataba miaka 10 kama leseni ya kitalu cha madini siyo reasonable kwa dunia ya sasa aisee! Muongo mzima?

Pia ameenda serikalini sijui BASATA nadhani anaogopa kwenda mahakamani maana utakuta hata cause of action hana. Wanasheria watakuwa wamekaa naye wakaona njia ya kumsaidia ndiyo hiyo. Huwezi ukaenda mahakamani eti ukadai mkataba halali uliofuata sheria na utaratibu zote eti "ni wa kinyonyaji"? How?

Kwenye sheria za mikataba tunasema consideration need not to be adequate but sufficient. Haijalishi hata kama gari la milioni 100 ukaliuza kwa milioni 10 kwa kuwa umekubali kwa hiyari yako hiyo anaitwa sufficient consideration japokuwa siyo adequate na hiyo haifanyi makubaliano yenu kuwa batili unless sasa kuna vitiating factors zingine zimekufanya uaccept terms hizo.

Kama ni mahakamani atatakiwa awe na cause of action ya kueleweka na siyo eti " wa kinyonyaji" hizo ni hoja za kisiasa. Kama nawaona wazee wa matamko hapo hata Mr Kangi atatamani atie neno ili mradi tu matamko.
 
Hili ni tatizo kubwa tulilonalo wa africa wengi, tukiajiriwa tunashindwa kuweka nidhamu katika kazi badala yake tunatamani kuwa wale waliotuajiri, mfano umeajiriwa na kampuni ya ujenzi kama foreman, badala ya kuweka nguvu yako kwenye kazi wewe unawaza kuwa kama mmiliki wa kampuni, Mfano Mavoco kabla ya kuingia WCB hakuwa na wazo kama anaweza kuwa kama Diamond, kaingia huko anataka awe kama Diamond, na akishamalizana na WCB akawa na kazi zake mtaona kama atakua na mafanikio yoyote
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…