Haijawahi tokea kwa sababu hawataki kufanya hivyo na sababu ya kutokufanya hivyo nimeeleza pale juu kama nawewe ulivyoieleza ni hofu upande wa lebo kwamba watakimbiwa na msanii.
Lakini tukija kwa upande mwingine mikataba mifupi ina manufaa makubwa kwa msanii leave along hiyo miwili au mmoja itaonekana michache basi kwanini isiwe minne au mitatu kwani albamu haikamiliki kwa muda wa miaka mitatu?
Ila Mavoko ameingia mwaka 2016 leo unataka kutoka angekuwa na mkataba wa miaka mitatu ungekuwa unaisha mwakani ni rahisi kuvumilia
Tukitumia neno "wanahofu watakimbiwa na wasanii....!" nadhani hiyo phrase sio sahii sana kwa sababu it sounds too personal wakati ukweli ni kwamba, it's all about business... na hiyo no popote pale utakapoenda!
Na popote utakapoenda, mikataba yao ni ya muda mrefu unless kama Msanii ni mkubwa mno compared na Lebo! Leo hii Pozi kwa Pozi Entertainment inaweza kukubali kumsaini Diamond hata kwa miezi 6 kwa sababu PKP inamuhitaji zaidi Diamond kuliko Diamond anavyoihitaji PKP!
Anyway, nimeeleza mengi kwenye post ya kwanza, sioni sababu ya kurudia tena hapa labda niende moja kwa moja kwa issue ya Rich Mavoko!
Kama Rich Mavoko alisaini mkataba wa hovyo katu siwezi kuwalaumu WCB! Mavoko ni mkongwe kwenye game!! Mavoko anazifahamu fika fitina za tasnia ya burudani, au angalau tasnia ya muziki! Mavoko alishawahi kuwa hadi kwenye management ya nje ya nchi! Maelezo yote hayo yanathibitisha jambo moja tu:
Rich Mavoko ni mzoefu wa haya mambo!
Sasa ikiwa pamoja na yote hayo, kwanini basi alisaini mkataba wa hovyo?
1. Labda ni mpumbavu!! Sio mjinga bali ni mpumbavu kwa sababu mjinga ni yule asiyejua! Kwanini alisaini mkataba wa hovyo wakati yeye ni mzoefu wa haya mambo? Alilazimishwa? Jibu HAPANA, so WHY?
Because--
2. Huenda Mavoko alifahamu fika kwamba mkataba ni wa hovyo lakini alitaka kuitumia WCB kumrudisha kwenye game! Hata kama kuna baadhi ya watu wanaodai WCB ilikuwa inampoteza Mavoko lakini ukweli ni kwamba Mavoko alienda WCB wakati ameshaanza kupotea kwenye game!
Hivyo basi, inawezekana kabisa alifahamu mkataba haukuwa mzuri lakini akaamua tu kusaini huku akitegemea, akisharudi tu kwenye chati, basi anatafuta way out!!!
Smart, right?! Yes or no!
Atakuwa amecheza smart endapo tu wakati anasaini tayari alishaona loophole kwenye mkataba vinginevyo, it's nice try lakini kachemka! Kachemka kwa sababu BASATA hawawezi kumsaidia kwenye mkataba usio na kasoro! Hata kama alisaini miaka 50 huo mkataba huwezi kuita una kasoro UNLESS kama kuna sheria ya nchi inayosema mkataba kati ya msanii na lebo hautakiwi kuzidi miaka xyz!
Au, BASATA wanaweza kumsaidia Mavoko ikiwa WCB wamekiuka terms za mkataba na mkataba una kipengele cha "free way out" ikiwa lebo imekiuka terms fulani fulani!
But for what I know, napata shaka ikiwa WCB wanaweza kutoa mkataba wenye kasoro... those guys hawakwenda shule but wana smart people nyuma yao!!!!!
Lakini kwa upande mwingine, kwa umaarufu wa Mavoko, hata kama alishaanza kupotea bado alikuwa na uwezo wa ama ku-negotiate better terms au hata kukataa!!!
Lakini kwanini mambo kama haya yanatokea sana?!
Nishawahi kusema mara kadhaa hapa kwamba, Tanzania tuna Wanasheria lakini hatuna Wanasheria wa Burudani; yaani Entertainment Lawyers. Anyway, hilo la Entertainment Lawyers lipo juu ya uwezo wetu lakini angalau tungekuwa na Wanasheria wanaoifahamu vyema tasnia ya burudani!!! Narudia,
kuifahamu tasnia ya muziki na
sio kuufahamu muziki!
Hii tasnia (ya burudani) ingawaje watu wanaichukulia poa lakini ipo very complex!!
Leo hii unaweza kusaini mkataba kwa sababu tu umeangalia basic benefits bila kufahamu kuna benefits zingine kadhaa ambazo kwa level uliyokuwa nayo, huwezi kuziona kwa sababu zinaibuka kadri unavyozidi kuwa mkubwa!!
Kwa mfano, ikiwa mkataba kati ya Harmonize na WCB umeangalia tu mapato yanayotokana na shows, streaming, digital and cd sales na endorsement! Halafu leo hii, WCB wanaamua ku-print TShirt za KWANGWARU halafu zinauzika ile mbaya!
Now tell me, wewe Harmonize unaenda kudai share ya mauzo ya tshirts kwa kutumia grounds zipi ikiwa mkataba wako hausemi chochote kuhusu hilo, whether directly or indirectly? Mbaya zaidi (na mara nyingi inakuwa hivyo), unaweza kukuta nyimbo zako ni mali ya lebo... refer Saida Karoli vs FM Studio (Mzee Mutta)!!
Halafu hizi lebo hizi' we acha tu! Zina invisible costs kibao ambazo baadae zinageuka kuwa kitanzi kwa msanii!!! Na hizi costs lebo wanaziingiza makusudi ili "balance sheet" ya msanii always iegemee upande wa debit!!!
Hata hivyo, kwa Mavoko sitarajii kama hazifahamu janja janja kama hizi unless kama ni stupid!!!!