WCB na mikataba ya ajabu: Ndio maana muziki wa Tanzania hauendelei

Kanye West hajasainiwa na Roc Nation bali waliingia ubia [partnership] ya kumanage kazi za Kanye West.


Mkuu jaribu kuja na evidence, unaposema kitu ni forged ebu leta original tukione.
 
Bado yuko pale sababu mkataba haumnyonyi.

Jiulize kwa nini Lil Wayne aliondoka?
Tangu nimeanza kumsikia Nicky Minaj mpaka leo bado yuko YMCM tu. 15 years sio kitu, kama anaona mkataba haumlipi anavunja maisha yanaendelea.
 
Ngoja wale vilaza Wama team waje
 
Ndio mikataba ya kitanzania. Sii mnasikiavm bungeni wanavyo lalamika? Tatizo la kuweka mikataba bila ya wanasheria. Sasa mnalalamika juu ya ujinga wetu
 
Kanye West hajasainiwa na Roc Nation bali waliingia ubia [partnership] ya kumanage kazi za Kanye West.


Mkuu jaribu kuja na evidence, unaposema kitu ni forged ebu leta original tukione.
Unaona sasa matatizo yako, sijamtaja kokote Kanye na Rock nation ila Rihanna na Rock nation.
.
Kanye west ana mkataba na EMI wakufanya muziki maisha yake yoteeee na hawa ndio waliomtoa mpaka leo hii unamjua Yeezy.
.
 
Hapo kwa Eminem ongeza ana label yake ya Shady na Detroit..
 
Watajua wapi?

Mikataba ya wenzetu haiwabani kuwa lebo zao ila hapa bongo unapigwa ban hata kufanya collabo na msanii fulani na fulani.
 
Unaona sasa matatizo yako, sijamtaja kokote Kanye na Rock nation ila Rihanna na Rock nation.
.
Kanye west ana mkataba na EMI wakufanya muziki maisha yake yoteeee na hawa ndio waliomtoa mpaka leo hii unamjua Yeezy.
.
EMI ilimsaini Kanye 2003 kabla hajatoa album yake ya The College Dropout. Mkataba wake ulikuwa wa miaka 7 saba tuu na uliisha 2010.

Tatizo lako unatetea mikataba ya muda mrefu wakati huko mambele wanaikimbia na hawaitaki kwa sasa.

Kanye West huyohuyo ana kesi na Roc-a-Fella Records, UMG Recordings, Def Jam, and Bravado International Group.

Ndio maana nasema na bongo pia mikataba ni ya kinyonyaji ndio maana wasanii kutwa kujitoa kwenye lebo zao.
 
Kuna mahala nilicomment kuhusu hizi contract za muda mrefu sana. Katika contract za wanamuziki wa kimarekani nilizosoma online huwa zinadumu kuanzia miezi tisa hadi miaka mitatu kwa shuruti kuwa katika kipindi hicho awe ametoa album kadhaa.Contract hizo ni za kusambaza album hizo za wanamuziki, lakini haiwaingilii kwenye maonyesho yao ya majukwaani. Wanamuziki huridhika kuendelea kurenew contract hizo hata kwa miaka kumi au zaidi kwa kuridhishwa na usimamazi wa usambazaji wa albuma zao. Lakini Contract za Bongo (niliwahi kusoma ya Mr Nice kwani iliwekwa hadharani) inaonekana kuwa huwa zinawabana sana wanamuziki hata kwenye tour wanazopata au hata matangazo ya biashara wanayoingia na makampuni mbalimbali kwa muda mrefu sana tena kwa asilimia kubwa sana.

Kwa sasa hatujui Contract ya kijana huyu, ila ule urefu wake ni swali la kujiuliza.

Katika kesi ya Kanye West dhidi ya EMI, utaona kuwa mkataba wa kwanza ulianza mwaka 2003 na ulikuwa na term ya miaka mitatu, lakini walifanya extentions kadhaa baada ya hapo. Malalamiko ya West ni kuwa mwaka ulikuwa unaweza kuzidi miezi 12 kwa vile walikuwa wanahesabu kuwa mwaka mmoja ni pale atakapokamilisha kutoa idadi ya album walizokubaliana. kwa hiyo akichelewa kutoa Albuma basi mwaka unaweza kuwa zaidi ya miezi kumi na mbili
 

Attachments

Msanii kumbrand hadi arudishe pesa ambayo umeinvest si rahisi kibongo bongo ambapo shows ndio zinamatter kwenye kipato cha labels. Angalia the industry kwa Rosalee, mkataba mfupi umewacost na sidhani hata kama ulirudisha pesa zao

Pia Huyo Harmo ni average guy kimuziki na nguvu aliyoitumia diamond kumpromote hadi akubalike inastahili kupata marejesho ya maana. Mimi naona ni sawa tu maana hata Harmo aliridhia

By the way mimi bado sijaamini hili sakata zima la Harmo kujitoa WCB maana naona hata WCB wanatumia nguvu kubwa kuwaaminisha watu which feels like a cooked up story. Sijui lakini
 
@Khaligraph Jordan pita hapa upate kuelewa mikataba ya wenzetu inavyokuwa sio unabisha tuu with no evidence.
 
Watajua wapi?

Mikataba ya wenzetu haiwabani kuwa lebo zao ila hapa bongo unapigwa ban hata kufanya collabo na msanii fulani na fulani.
Tatizo la watanzania ni lile lile umaskini na kutokuwa na elimu na kuleta ujuaji baadae tunakuja kulalamika
Mkataba hauwezi kuwa valid kama haujaridhiwa na pande zote mbili,Hivi Harmonize alilazimishwa ku-sign huo mkataba unaouita wa kinyonyaji ?

Pia kwa mujibu wa uongozi wa Wasafi ,Harmonize amesema atalipia gharama za kuvunja mkataba,sasa hizi kelele sijui zinatoka wapi wakati mhusika kasema atalipa gharama za kuvunja huo mkataba.
 
Mzee miaka ya 1990s uko
 
Kuna hali mbili wakati wa kusaini mkataba. Ukibanwa na njaa huwa usomi mkataba vyema we unaangalia figure kiasi gani.
Hali ya pili ni wakati wa utendaji ndo unagundua ulichofanya ulikosea.
Mie si mjuzi wa sheria, ila kama amekubali kulipa pongezi kwake. Maana anaweza akajivunia barafu juani
 
Kipindi diamond ana invest kwa huyu mmakonde hela nyingi ikiwa huyu mmakonde Hana nyuma Wala mbele hata hela ya kulipa nauli ilikuwa shida kwake unafikiri hela zinaokotwa inabidi huyo mmakonde arudishe investment iliyowekezwa kwake na pia wakati anasign huo mkataba si aliamua yeyemwenyewe au alilazimishwa?yaani haya maneno unayoongea utazidi kumuaribia huyo dogo.
 
Hapo ndipo lilipo tatizo, hutakiwi kuinvest kwa mtu bali kazi zake. Mkataba unatakiwa uwe wa kusapoti kazi zake na si kumsapoti yeye sababu unapoinvest kwa mtu unatumia gharama kubwa unnecessary.
 
Hapo ndipo lilipo tatizo, hutakiwi kuinvest kwa mtu bali kazi zake. Mkataba unatakiwa uwe wa kusapoti kazi zake na si kumsapoti yeye sababu unapoinvest kwa mtu unatumia gharama kubwa unnecessary.
We jamaa unichekesha unataka kuniambia wcb walikuwa hawawekez kwenye kazi zake unafikiri wasingekuwa hawainvest kwenye kazi zake angefika kwenye level hizo?hizo connection za international artists si alipata kupitia wcb video ya kwanza tu ya harmonize ililipwa mil 30.siku nyingine usipende kuandika thread kwa miemuko Bila kufikiri ndo maana 99% wamekupinga na inaonesha umeanza kumfuatilia harmo kipindi ana mafanikio ujawahi kumfuatilia kipindi akiwa Hana chochote na WCB wamefanya kazi kubwa kwake kumbuka harmo alikataliwa bss pia msanii aliyepigwa Vita Sana Bila ya WCB kusimama kidete harmo asingefika hapo.sijaona mantiki yako yakuwalaumu WCB ulitakiwa kuwashukuru.Uzi wako utazidi kumfanya harmo achukiwe Sana na fans wa music especially wanaompenda diamond Sana.
 
Liko wazi hilo mkale, ndio alihusika na kifo chake kwa 100% sema ndio hivyo jamaa alikuwa amevishika vyombo vya ulinzi kwelikweli pia ndio alihusika katika kifo cha BIG...
Hapa ndo nmekuona hujui lolote kuhusu 90's hiphop culture
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…