WCB naona Nyimbo juu ya Nyimbo, Kuna nini?

Juzi nimesikiliza hiyo ya kofgi olomide nikabaki nacheka tu

Yani inasikitisha sana kwa kizazi ambacho tupo unamlipa msanii aje afanye colabo halafu akifika studio nagu bezz gwake anaanza kuimba "yachee yapchee"

Wakati huo umemlipia cost za hotel mpaka safari.
 
Sikufichi na sitaki kua mnafki, diamond angepata bahati ya kuwa msanii kwenye nchi ambayo watu wengi wako conscious asingekuwa wack angeimba mziki logical

Naimani diamond saizi hata aingie booth asukiwe beat lolote na lazier kisha alimalize beat kwa kukohoa tu mwanzo mwisho bado watu wataipaisha hiyo nyimbo na kuiweka katika list ya nyimbo yenye viwango bora

Juzi katuimbia "kachukua kaweka waah", jana kaja katuimbia "yesa yesa yesa"

Bet kesho atakuja na single ipi?

Hiyu jamaa ni wack sitaki kua mnafki hata kama anamake mkwanja hiyo haimaanishi anachokifanya ni kizuri, maana kuna watu wana make billions of dollar kwa drugs lakini hiyo haitoi kibali kua biashara ya drugs ni nzuri

If you gonna call me hater for what I said, you gonna be hater too for criticizing my opinions
 
Kwa kuimba matusi jamaa wako vzr aisee.
Tulipoingia kizazi kipya tulimkataa mista nice kwa nyimbo zake zile za "kuku kapanda baiskeli bata kavaa laizoni" now tuko 2020 tukielekea 2021 eti msanii anaingia studio anatuimbia "kachukua kaweka waah", "yesa, yesa yesa"

Kuna mwenzake mmoja sijui nani nyimbo nzima kaishia kuimba "sexy, sexy lady sexy, irene uwoya sexy, sijui nani sexy"

Hizi ndio nyimbo ambazo nash mc alituambia tuzime, unarekodi single unataja taja tu watu majina halafu kwa nje ya cover unaandika wimbo.. Neno wimbo linatumika hovyo nowdays
 
Msanii ni kioo cha jamii hivyo kila kazi unayoifanya ni lazima ukumbuke nyuma yako kuna kundi la watu wameweka matazamio yao kwa kupata faida ya maarifa mapya kupitia kazi zako

Ubora wa wimbo ni mashairi na hapa namaanisha lryical

Halafu kwa bongo hapa tayari mziki umeathiriwa kwa trend na mazoea, na ndio maana watu saizi huangalia WCB kama ndio source kuu ya mziki mzuri.

So hata leo diamond akiingia studio kisha akarekidi mluzi wa dakika 3 kisha akatupia youtube tayari watu watau-view huo mluzi na kwasababh watu washajiwekea mazoea watatoa kongole tu kua mwana ngoma hiyo kaua na kama ilikua ni kolabo kuna mdau mwingine alihusika kupiga kolasi ya mluzi watu wataeema tu kua jamaa kapotezwa na simba

Hii ndio tanzania ambayo tupo, msanii anaingia studion anaimba sexy, sexy, sexy lady sexy na anapasua views zaidi ya milion wakati huo kuna ngoma kali za vijana wadogo tu ambazo zina make sense hazisikilizwi wala hazina views

Mwishoni hapo nimesikitika sana ulivyo mtusi jamaa kwa kumtukania mzazi wake as if mshkaji una hisa pale wcb
 
Hahaha hivi nikichomeka socket ya umeme nikawasha kisha nikawa naikojolea mkojo nini kitatokea?
 
Hahaha hivi nikichomeka socket ya umeme nikawasha kisha nikawa naikojolea mkojo nini kitatokea?
Kwamba unachomeka kikojoleo kwenye socket, au unachomeka nini? Vyote unavyo, jaribu utupe mrejesho!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…