WCB vs THT

BUSH BIN LADEN

JF-Expert Member
Joined
Mar 16, 2019
Posts
8,447
Reaction score
19,425
Habarini ndugu wana jukwaa!

Nimefuatilia sana kuhusu hii trend ya baadhi ya media kutopiga nyimbo za baadhi ya wasanii na mara zote nakosa majibu kwa kuwa hakuna media inatoa sababu za kwanini imefikia maamuzi ya kutopiga nyimbo za m/wasanii husika.

Kwa kesi ya Clouds media na kutokupiga nyimbo za WCB kidogo naweza kuhisi sababu japo sina ihakika ila nahisi yatakuwa mambo ya biashara. Nahisi hivi kwa sababu wamiliki na viongozi wa WCB ndio wamiliki wa Wasafi Media kampuni iliyo kwenye industry moja na CMG hivyo Clouds FM au TV kupiga nyimbo za Wcb itakuwa kama kuipromote brand nyingine kitu ambacho hakiwezekani. Yaani ni sawa Pepsi wachore chupa ya sparletta kwenye magari yao.

Clouds kwa hili naweza kuwaelewa lakini nisiowaelewa ni media zingine hasa East Africa(redio na TV ) na E(FM na TV ). Hawa nao hawachezi nyimbo za WCB japo kwa upande mwingine wanacheza kazi za wasanii wa THT.

Nisichokielewa ni vp unagoma kucheza nyimbo za Wcb(inayomilikiwa na wenye Wasafi media) ila unacheza nyimbo za Tht(inayomilikiwa na Clouds media).

Je kuna makubaliano ya kibiashara kati ya CMG na hizi media nyingine kuhusu kucheza nyimbo za THT ambayo hayapo kati ya Wasafi media na kucheza nyimbo za WCB?

Je inawezekana East Africa na Efm & Etv wanapigana vita ya Clouds bila kujua kama ilivokuwa kwenye ugomvi wa Ruge(r.I.p) na Makonda au tuamini aliyowahi kusema Kusaga kwamba anamiliki vyombo vya habari vingi hapa Tz so huenda na hizi redio na TV mbili kuna mkono wa kusaga ndo maana wanafanya karibu kila kitu anachokifanya Clouds.

Nina maswali mengi ya kuuliza kuhusu WCB na THT, ni vp media house isiyo CMG au Wasafi Media iamue kupiga/kutokupiga nyimbo za moja kati ya lebo hizi za muziki Tanzania!

Naomba kuwasilisha na naomba mchango wenu katika hili.

Note: mambo ya timu hapa hayahitajiki
 
Huyo Msanii Wenu Na Mameneja Wake Wana matatizo na Media nyingi tu, hata Kabla hawajawa na hiyo Media yao..

THT ni Kama Chuo, Mkuu Wao hana Noma na Media Zingine

WCB ni Label, Mkuu Wao na Mameneja wake ndo Wenye Matatizo..
Mnyama mkali Leo umeongea point
 
Kwanza kabisa elewa tu .mondi yeye hana shida na MTU. Ila ma manager wake na management nzima ndo tatizo
 
Wasafi media na WCB ni vitu viwili tofauti kabisa.Suala hapa sio umiliki bali ni bland.Kila bland inajitegemea.Mbona eatv na ea radio hawapigi nyimbo za wasafi lakini radio one na itv wanapiga licha ya kuwa zote ni mali ya ipp chini ya mzee mengi???

tht ni tht na sio clouds hata awe mmiliki mmoja kila bland itatembea kivyake.

Halafu sababu ya tofauti ya Diamond na clouds chanzo ni Diamond kugoma wasanii wake kutumika kwenye matamasha ya clouds kama fiesta kwa bei ndogo ndipo wakaamua waache kupiga nyimbo za wasafi kama ilivyo kawaida yao wakigombana na wasanii.

Eatv chanzo ni Diamond na wasanii wake kuamua kutoshiriki katika tuzo walizoandaa mwaka 2016.
Sina uhakika sana kwa tve na e fm japo nadhani inaweza fanana na clouds.

Ukweli ni kwamba Diamond alitambua thamani yake na kuacha kutumika kuwatengenezea faida wengine ndo maana leo wasafi media ipo juu kwa sababu yake.
 
Hata sielew[emoji848]
Mkuu soma tena. Kiufupi nataka kujua kwanini East Africa na Efm wanacheza nyimbo za wasanii wa THT(wanaomilikiwa na wenye Clouds) ila hawachezi nyimbo za WCB(wanaomilikiwa na wenye Wasafi media)
 
Huyo Msanii Wenu Na Mameneja Wake Wana matatizo na Media nyingi tu, hata Kabla hawajawa na hiyo Media yao..

THT ni Kama Chuo, Mkuu Wao hana Noma na Media Zingine

WCB ni Label, Mkuu Wao na Mameneja wake ndo Wenye Matatizo..
ulitaka awe anajinyenyekeza kama Kiba??? mondi anatambua thamani yake na anajua kuitumia
 
So sababu kuu ni mmiliki wa WCB kugoma kuwasindikiza watu wakawe matajiri?
 
Mimi pia najiuliza kwanini ITV na Radio One wanacheza nyimbo za Wasafi lakini EATV na EA Radio hawafanyi hivyo wakati wote wapo chini ya IPP
 
Huyo Msanii Wenu Na Mameneja Wake Wana matatizo na Media nyingi tu, hata Kabla hawajawa na hiyo Media yao..

THT ni Kama Chuo, Mkuu Wao hana Noma na Media Zingine

WCB ni Label, Mkuu Wao na Mameneja wake ndo Wenye Matatizo..
Mkuu unaposema WCB na management yake ina matatizo halafu usiyaelezee unakuwa hujatutendea haki
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…