WCB, wadau hamuwatendei haki Ben Pol, Belle 9 na wengineo

WCB, wadau hamuwatendei haki Ben Pol, Belle 9 na wengineo

Kuna watu wanaweza lakini kuna genge la mafia pale WCB. Mtu kama Rama Dee yaani bonge la msanii sijawahi kusikia katoa ngoma mbovu basi tu sijui kwanini. Kweli unaweza kumfananisha Harmonize sijui na Rama, kwa ngoma gani, basi promo tu nyimbo zake zote kawaida tu hakuna jipya.
 
Inavyosemwa ni kwamba 2june Rich Mavoko naye anajiunga WCB!

Namuamini sana Rich, naamini uwezo wake wa kuimba, lakini kwa nini ameamua kwenda pale WCB!?

Tusipanic waungwana, si kila jambo likizungumzia WCB basi tuliletee Uteam flani!! Tujadili kwa pamoja kwamba ni kwa nini wanamuziki wazuri kama Ben Pol, Belle 9, Baraka da Prince na weengi wengineo kuwataja tutakesha hawatoboi inavyowastahili!?

Yaani mimi naamini uwezo wao ni mkubwa sana kulinganisha na malipo wayapatayo kutokana na kazi zao!! Yaani hakuna show kubwakubwa wanazopata na zenye malipo stahili kulingana na uwezo wao!!

Tunakoelekea muziki au kazi ya burudani inaelekea kuhamishiwa WCB,
Sasa na Rich nae akisain watakuwa wasaniii wanne tayari pale na kama show zinaelekezwa pale watakuwa wanagawana wao tu!!

Weekend kunakuwa na matukio makuu ya burudani kama mawili matatu kwa mfano nchi nzima! Nazungumzia matukio makubwa!! Sasa kwa matukio matatu au manne huku anaenda Harmo, huku Ray na kule Rich tayari wengine watatumbuiza Dar live!! show zisizo na mkwanja wa maana!!

Nachopendekeza sisi kama mashabiki tuangalie ni nini tunaweza kufanya kuondoa hali hii ili wanamuziki tuwapendao nao waone thamani ya kazi yao!

Sasa hii haitaki hasira, simaanishi tuanze kuleta chuki kwa wanaofanikiwa hapana, tuwasaidie kitaalamu na si kutumia chuki na vita vya kimwili kwani imeonekana si njia sahihi!!

Inasikitisha kuona msaniii kama PNC siku hizi anatumbuiza sehemu ambayo kiingilio ni kinywaji!!
 
Nimeliona hili na nikaona si mbaya kushea na wanajamii!!

Tanzania tumebarikiwa vipawa vya wanabongofleva vya kutosha na maridhawa kabisa!!

Tumekuwa na wanamuziki wazuri hasa na kwa uchache nimewataja hapo juu kwenye head!!

Kiufupi naona soko la muziki hapa kwetu Tanzania linaelekea kushikwa na wachache na kuwaacha WAKALI wengine wakipiga miayo au kuishi maisha ya chini tofauti na vipaji vyao!!

Diamond pekee tayari ana show nyingi mno hapa nchini na kimataifa hali ambayo si nzuri kwa wanabongofleva wengine!!

Kuna wasanii hawapigi show mpaka kusubiri vitu kama FIESTA wakati wachache kila wiki ni wao tu majukwaani!!

Ujio wa HARMONIZE na huyu RAYMOND unakuja kuongeza njaa kwa wanamuziki wetu wazuri kabisa kama Chegge, Matonya, Q chillah na weengi siwataji!!

Naona show nyingi sasa zitaelekezwa WCB kwa kuwa kila promota anataka pale!!

Media, mitandao ya kijamii na karibia promo zote mjini zinazungumzia WCB kwa ziada!!

Niwaombe wananchi wenzangu tuwathamini na hawa kina Mirror, Matonya, Belle 9 na weengi wanaojua kuimba!!

Nawakubali sana WCB lakini ni lazma tuwajali wote wanaojua hii kazi ili nawao wafeel kipato cha jasho liwatokalo.

Ni hayo tu!!
muziki ni biashara na biashara inahitaji akili kubwA,hpo ndipo utakapo kubali kua diamond na team yake ni visionary.....hao jamaa wajiongeze tu so as to give a beat down WCB otherwise wataishia kulalamika tu.

huu mchezo unahitaji akili.
 
Waangalie chibu kafanikiwaje mpaka kufika hapo then nao wapite njia alizopita chibu tu........kama wanaona vipi basi wakajiunge na lebo ya PKP ya ommy dimpoz hili wakamuinue nao wawe juu
 
Sema industry ya bongoflava Kiujumla bado haijakaa sawa kabisa So inabidi tuwasapoti wasanii wetu kwa nguvu zetu zote.
 
Moyo mashine
Heshima kwako been Paul tunaojua mziki diamond atasubili sana kwako kijana keep it up unajua

Na kama ipo ipo tu time will tell

Unajua mkuu hapa ishu sio kujua!!

Woote tunakubaliana kwamba kuna wanaojua hasa huu mziki kuliko watoto wa WCB!!
Kujua pekee haijawa msaada kwa hawa wanamuziki wetu tuwapendao!!

Tunataka wote tujadili na ikiwezekena tuje na majawabu ni kwa nini mafundi wa hizi kazi kama RAMA D muziki hauwalipi ipasavyo!!?
Tukipata majawabu basi tuwasaidie au tusaidie kugeuza hili game linakoelekea!!

Tusaidie game limlipe kila anayeweza kazi!!

Tukisema tu kuwa time will tell tutakosea kwa sababu jua halisimami! au Dunia haisimami, au muda HAUSIMAMI!!
 
Unajua mkuu hapa ishu sio kujua!!

Woote tunakubaliana kwamba kuna wanaojua hasa huu mziki kuliko watoto wa WCB!!
Kujua pekee haijawa msaada kwa hawa wanamuziki wetu tuwapendao!!

Tunataka wote tujadili na ikiwezekena tuje na majawabu ni kwa nini mafundi wa hizi kazi kama RAMA D muziki hauwalipi ipasavyo!!?
Tukipata majawabu basi tuwasaidie au tusaidie kugeuza hili game linakoelekea!!

Tusaidie game limlipe kila anayeweza kazi!!

Tukisema tu kuwa time will tell tutakosea kwa sababu jua halisimami! au Dunia haisimami, au muda HAUSIMAMI!!
Mtu kama Rama D affiliation yake na wale vinega imemcost big time. Media kama cloudz imechangia kuua ndoto za wasanii wengi.
Lingine nafikiri ni lack of creativity na poor management.
 
Mtu kama Rama D affiliation yake na wale vinega imemcost big time. Media kama cloudz imechangia kuua ndoto za wasanii wengi.
Lingine nafikiri ni lack of creativity na poor management.

Lakini kuhusu ugomvi na media kuna mtu kama NURUELI huyu hajawahi kuwa na beef na media yeyote!! Naamini jamaaanajua sana kuimba lakini mkondo ni uleule game halijawatendea haki!!
 
Mziki sio kujua kuimba pekee, hata mbele tunaona madogo kibao wanavipaji vya kuimba vya kutisha kwenye mashindano ya x-factor, American idol n.k ila wakitoka humo hawasikiki, the same to bongo star search hapa kwetu...

Kutengeneza bidhaa inayohitajika zaidi na kutumiwa kwa kiasi kikubwa na wateja wako ni bora kuliko kutengeneza bidhaa bora (ukiachilia mbali marketing strategies) Kwa hili hata kwa Afrika mziki wa RNB umefeli kwa sasa, haufanyi vizuri kama Afropop coz watu wanataka melody ya kuchezeka zaidi...
 
Wasanii wengi hawana plan ya pili .. kuna mchangiaji humu kasema kuna kujua mziki na kujua soko la mziki,tumezoea kuwasikia wasanii wetu wakivuma kipindi Fulani tu then wanapotea,ni kwasababu wengi hawana management nzuri, hawana management ambazo zinaweza zikakaa na ku-plan mwelekeo wa msanii kwa miaka kadhaa ijayo!!! ... tena hawa wanamuziki wetu pendwa wasipobadilika wote baadae watasainiwa chini ya label ya #WCB sababu ndipo mahali pekee penye future kwa sasa!
Ni wakati sasa wa management za wasanii wengine kujipanga na kuwa na mipangao endelevu kwa wasanii wao ili basi tuone changamoto na ladha mbali mbali katika muziki wetu.
 
Jibu ni moja tu soko la mziki wa tz limeshikwa na wajanja wa janja naposema wajanja naimanisha wale watu ambao shule hakuna taluma ya masoko hakuna wao fitna husda ndio siraha yao

Kwaiyo wanashindwa upeleka mziki kitaalamu wao kazi zao kubania wengine figisu figisu kibao

Ndio maana unambiwa wasanii wa Uganda wapo vizuri kuliko wetu sababu moja tu mziki wakule wadau wakuu si wajanja wajanja naposema wadau wakuu naimanisha producer mameneja nkTE="Ngonepi, post: 16352330, member: 147931"]Unajua mkuu hapa ishu sio kujua!!

Woote tunakubaliana kwamba kuna wanaojua hasa huu mziki kuliko watoto wa WCB!!
Kujua pekee haijawa msaada kwa hawa wanamuziki wetu tuwapendao!!

Tunataka wote tujadili na ikiwezekena tuje na majawabu ni kwa nini mafundi wa hizi kazi kama RAMA D muziki hauwalipi ipasavyo!!?
Tukipata majawabu basi tuwasaidie au tusaidie kugeuza hili game linakoelekea!!

Tusaidie game limlipe kila anayeweza kazi!!

Tukisema tu kuwa time will tell tutakosea kwa sababu jua halisimami! au Dunia haisimami, au muda HAUSIMAMI!![/QUOTE]
Jibu
 
Belle 9 toka ameanza game hajawahi kuwa na skendo ya demu, unategemea nini kwa hii game ya bongo?
Masogange kawa star kuliko yy anapiga collabo na kina davido lakn bele kabaki mchangani wakati alikuwa video queen wake
No skendo na airtime no hit labda ukomae Kama kiba
 
Naliona game la bongoflava mahali ambapo si salama kwa wasanii wengi kwa kweli!!
 
Back
Top Bottom