WCB, wadau hamuwatendei haki Ben Pol, Belle 9 na wengineo

WCB, wadau hamuwatendei haki Ben Pol, Belle 9 na wengineo

Kuna watu wanaweza lakini kuna genge la mafia pale WCB. Mtu kama Rama Dee yaani bonge la msanii sijawahi kusikia katoa ngoma mbovu basi tu sijui kwanini. Kweli unaweza kumfananisha Harmonize sijui na Rama, kwa ngoma gani, basi promo tu nyimbo zake zote kawaida tu hakuna jipya.
Kwani nani kakatazwa kufanya promo?
 
Nimeliona hili na nikaona si mbaya kushea na wanajamii!!

Tanzania tumebarikiwa vipawa vya wanabongofleva vya kutosha na maridhawa kabisa!!

Tumekuwa na wanamuziki wazuri hasa na kwa uchache nimewataja hapo juu kwenye head!!

Kiufupi naona soko la muziki hapa kwetu Tanzania linaelekea kushikwa na wachache na kuwaacha WAKALI wengine wakipiga miayo au kuishi maisha ya chini tofauti na vipaji vyao!!

Diamond pekee tayari ana show nyingi mno hapa nchini na kimataifa hali ambayo si nzuri kwa wanabongofleva wengine!!

Kuna wasanii hawapigi show mpaka kusubiri vitu kama FIESTA wakati wachache kila wiki ni wao tu majukwaani!!

Ujio wa HARMONIZE na huyu RAYMOND unakuja kuongeza njaa kwa wanamuziki wetu wazuri kabisa kama Chegge, Matonya, Q chillah na weengi siwataji!!

Naona show nyingi sasa zitaelekezwa WCB kwa kuwa kila promota anataka pale!!

Media, mitandao ya kijamii na karibia promo zote mjini zinazungumzia WCB kwa ziada!!

Niwaombe wananchi wenzangu tuwathamini na hawa kina Mirror, Matonya, Belle 9 na weengi wanaojua kuimba!!

Nawakubali sana WCB lakini ni lazma tuwajali wote wanaojua hii kazi ili nawao wafeel kipato cha jasho liwatokalo.

Ni hayo tu!!
ben pol na bell wazur sana
 
Belle 9 toka ameanza game hajawahi kuwa na skendo ya demu, unategemea nini kwa hii game ya bongo?
Aende bongo movie atapanda chart! awe selective tuu alichukue ngungu moja limpe jina kama wenzie....
 
Mwisho wa siku wasanii wote watataka wasainiewe WCB ili walau wapatize chochote kitu na wao...WCB miaka ya mbele kutakuja kuwa na jam sana ya wasanii pale,na media zote takribani Signature itayokuwa inasikika kila dakika ktk kila ngoma inayochezwa ni "waaaahsafiii"(wasaf record).
I also see this coming, kwa upande wangu singependa iwe hivyo kwa kweli, so something should be done ASAP, to neutrolize the power of WCB, before its to late, ili kuleta chachu katika tasnia ya bongo fleva.
 
Kuna watu wanaweza lakini kuna genge la mafia pale WCB. Mtu kama Rama Dee yaani bonge la msanii sijawahi kusikia katoa ngoma mbovu basi tu sijui kwanini. Kweli unaweza kumfananisha Harmonize sijui na Rama, kwa ngoma gani, basi promo tu nyimbo zake zote kawaida tu hakuna jipya.
Ni kweli kabisa uyasemayo, lakini kinachowafelisha hao wanaojua kuimba ni kubweteka, mtu anatoa nyimbo hata kuitangaza mwenyewe tu anaona uvivu, huu uvivu huwezi kamweeeee kuukuta pale WCB, NGOMA KABLA HATA YA KUTOKA INATANGAZWA MFANO HAKUNA, SI ALIYETOA sio MADANSA, MASHABIKI, MPAKA NDUGU WA FAMILIA AMBAO HAWAFANYI MZIKI UTAWAONA WAKITANGAZA, sasa ngoma yenyewe itoke utadhani kuna sherehe ya Kitaifa maana hizo shamra shamra huko kwenye mitandao ni hatari, na ndio maana unakuta nyimbo nyingi kutoka WCB zinavutia viwers wengi, hii kitu me nimeiona kwa DIAMOND TUUUU! lakini wengine hutoa nyimbo then wanaiacha itembee yenyewe na iende inapotaka kwenda yenyewe, SOKO halitaki ubwetekaji wa namna hii, mfano mzuri ni yule aliyetoa wimbo wa "KAMA UTANIPENDA" huu wimbo ungetokea WCB ungekuwa wimbo wa taifa, lakini mwenyewe waalaaaa hana habari nao, na juzi kaulizwa kwenye Enews kwanini katoa hit song lakini yeye katulia kama maji mtungini, ajichojibu......... kamuulizeni sami misago mtazimia. Sasa wasanii kama hawa wakipigwa bao na WCB walama zinaelekezwa kwa DIAMOND, mara anawabania wengine wasitoboa, anataka awe juu yeye tuu. Anawazibia blah blah blah! Kumbeeee kuna watu mpango wa kutoboa wala hawana, wao wakishaimba wakarelizi ngoma there enough!
 
WCB hakutaweza kuwa na jam hata kidogo, maana WCB kwasasa ina wasanii watatu, mondi, harmo na Raymond.. Bado wasanii wawili tu ili watimie watano basii.. Jumla ya wasanii watakaokuwa chini ya wasafi ni watano tuu.. Na tarehe 2 June watamtambulisha rich mavoko kama msanii wao wanne, na msanii wa tano ataebakia atakuwa ni msanii wa kike
wakusambaza ngada bondeni...
 
Mbona hulalamiki Bakhressa kila sehemu amekaba mpaka sasa kwenye Media?! Kifupi muziki ni biashara , ukienda Marekani YMCB(Birdman) wamedorminate katika Hip Hop, Nigeria Marvins (Don Jazz) etc

Kingine wasanii uliowataja hawajui kuji'Brand japokuwa ni waimbaji wazuri pia wanafanya muziki wa mazoea.

BTW, Kaangalie show ya RayVanny(msanii wa juzi) na Belle9, utapata majibu who are serious with industry.
 
wangetafuta kik kwa mijimama ya bongo movie kama wengine wangetoka mara moja mbona
 
Back
Top Bottom