WCB watembelewa na Waziri wa mambo ya ndani


Naona ' Mhangaikaji ' anavyojitahidi kujitengenezea mazingira ya kujichanganya na Makundi mbalimbali ya Watu nchini Tanzania ili aweze kuja Kugombe Urais wa nchini Tanzania 2020 au 2025. Kaanza na kujikita ndani ya Klabu ya Yanga na tayari kwa mikakati yake ameshaanza kukubalika na sasa amehamia kwa Wanamuziki kisha ni imani yangu baadae atahamia kwa Wamachinga, Wakulima na Wavuvi huku akiwaacha Wasomi kwani anajua fika kuwa hakubaliki kwao.

JPM Wahenga hawakukose waliposema ile kauli kuwa " KIKULACHO KI NGUONI MWAKO ". Kila la kheri!
 
Jamaa ana kiu ya 2025 sasa anajaribu kila namna kusikika kila siku
 
Kuajiri watu 50 na kulipa iyo ml40 kodi sio sababu ya msingi kuna msingi unaowapapeleka huko
 
Hata miye ningekuwa mwanasiasa ningeenda ofisin Kwa diamond. Diamond ni icon ya Vijana maskini wanaotaka kufanikiwa. Kosa wanalofanya wanasiasa wa upinzani ni kuignore vitu km hivi. Litakuwa ni jambo jema kwa kubenea naye akamsalimie diamond mwananchi wake au mdee. Diamond anatukumbusha kufanikiwa hakuhitaji utokee familia ya kitajiri. Vijana wenzangu Tanzania kuna amani sana km tukiweza kuunganisha nguvu tutafika mbali sana. But tukiendelea na brah brah za wanasiasa uchwala kutoboa tusahau.
Diamond ni icon Kwa wanasanii wote, wafanyakazi na wafanyabiashara. Nina ndoto ya kuwa NGOs kubwa, insurance company na kampuni ya kusupply kubwa. Ntafanikiwa tu Mungu ni mwema.
Mh. Mwigulu karibu sana.
 
Umeongea ukweli mkuuu.
 
Ulitaka afanye nini ili ujue ana kazi ya kufanya? WCB wanachangia pato la taifa kiasi gani kwa mwaka ukilinganisha na pato unalochangia wewe? Unajua WCB imeajiri vijana wangapi wenye familia zinazowategemea?
Wachana na kiroboto ndugu
 
Hapa kuna kitu zaidi ya muziki. Kwan wasafi ndio watu wa kwanza kuwa na ofisi za muzik Tanzania? Ofisi sio lazma iwe jengo la kupendeza, kuna studio ngap wanamuzik wanamilik hatuhawah kushuhudia viongoz wanaenda huko. Kuna bongo records, mj record na zngne hzo ni ofisi zawasa ii hakuna kiongoz tuliyewah kumuona akitembelea.ukitumia akili ya ziada kuwaza hili unaona kuna kingne kinaendelea sema ndio hvyo huwa hawapost mazungumzo tunakuja kuoneshwa picha wakat kingne kishajadiliwa. Kama ni muziki kwanini wasiende viongoz wenye dhamana na muziki peke yake? Ila tumeshuhudia waziri wa mazngr na leo waziri wa mambo ya ndani. Wanahusikaje hapo sasa na mziki? Time will tell lets wait and see
 
Mwaka huu TRA Walimchomoa m 200+ .... mtu km mond serikali inamuangalia kwa jicho la upekee sana.
 
Naona picha kama ya fuvu la kichwa hapo mezani kushoto au macho yangu Simoni vizuri,

Wajuzi wa mambo nijuzeni ndio nembo yenyewe.?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…